Isimu

MAKALA KUHUSU AINA
MBALIMBALI ZA LUGHA YA
MAZUNGUMZO.
UTANGULIZI:
Lugha ya mazugumzo ni maongezi ya watu wawili au zaidi bila kutumia maandishi. Lugha ya mazungumzo ambayo ndiyo lugha kongwe zaidi ya lugha ya maandishi ina dhima kubwa ya kufanikisha mawasiliano miongoni mwa watu au kikundi fulani. Lugha hii ya mazungumzo ilianza punde tu binadamu alipoanza kukabiliana na mazingira yake, hivyo kimsingi lugha ya mazungumzo ndiyo nguzo kuu ya kufanikisha shughuli zote za kibinadamu kutokana na nafasi yake kimatumizi.
Lengo la kuandaa makala haya ni kuonesha aina mbalimbali za lugha ya mazungumzo kwa kuzingatia mazingira rasmi na yale yasiyo rasmi, utambulisho wa kijamii kama vile: matabaka, hadhi yake, mshikamano na mwachano. Pia tutatalii jinsi gani utambulisho wa kimuktadha unavyoweza kuzalisha aina tofauti tofauti za lugha ya mazungumzo kwa mfano; lugha ya siri na yenye mipaka, michezo ya vitendo, kucheza na maneno, uganga kama miviga na utani kama miviga.
Hebu sasa tujipe wasaa kwa kutalii kipengele kimoja baada ya kimoja kama vilivyoorodheshwa katika utangulizi wetu.
Aina ya lugha ya mazungumzo kwa kuzingatia mazingira rasmi na yasiyo rasmi:
Mazingira rasmi: kwa mujibu Kihore (2004) haya ni yale mazingira yanayoendana na kaida za kijamii, kisheria na kiutamaduni ambazo huhusisha matumizi ya lugha iliyosanifu. Huu ni muktadha unaohusisha ushirika wa upande mmoja, kama vile msamiati wa kiufundi na adabu maalum. Mfano wa mazingira rasmi ni kama vile ofisini, mahakamani, bungeni, kanisani, msikitini na katika elimu. Katika mazingira rasmi tunapata aina mbili za lugha ya mazungumzo ambazo ni jagoni na rejesta.
Jagoni: ni aina mojawapo ya lugha inayotumika katika taaluma fulani mahususi kama vile fasihi, isimu, sheria, sayansi, uhandisi, biashara nakadhalika. Hii ina maana kwamba, lugha hii itafahamika na wale tu walioko katika taaluma husika au wenye maarifa ya taaluma hiyo. Kwa mfano wanaisimu hutumia maneno kama vimadende, vitambaza, vipasuo kwamizi nk. wakirejelea jinsi ya utamkaji wa aina fulani za sauti katika lugha. 
Rejesta: Halliday (1989), anafasili rejesta kama mtindo wa lugha kutegemeana na kazi au shughuli. Vilevile fasili hii inaendana na fasili ya Habwe na Karanja (2007).
Kwa ujumla tunaweza kufasili rejesta kama mtindo wa lugha kutegemeana na kazi fulani, muktadha wa matumizi, lengo na uhusiano wa wanaowasiliana. Katika muktadha rasmi rejesta hurejelea upande mmoja kama vile, msamiati wa kiufundi, adabu maalum na matumizi ya lugha fasaha, mfano katika elimu, mahakamani nakadhalika. 
Mazingira yasiyo rasmi: haya ni mazingira ambayo hayafungwi na kaida, sheria na tamaduni za kijamii. Mazingira haya hutumia msamiati ambao si rasmi yaani lugha isiyokuwa sanifu. Katika mazingira haya tunapata aina zifuatazo za lugha ya mazungumzo: misimu, agoti, rejesta na lahaja. 
Misimu: Msanjila na wenzake (2009:19) wanafasili dhana ya misimu kuwa ni aina ya misemo katika lugha ambayo huzuka na kutoweka. Sifa kuu ya misimu ni kwamba haidumu muda mrefu na sio lugha sanifu, na watumiaji wa misimu huwa ni kikundi cha wazungumzaji wa lugha katika jamii ambao kimsingi huishi katika eneo moja.
Ngure (2003:147) anaonekana kukubaliana na Msanjila kwa kiasi kikubwa isipokuwa yeye anaweka mkazo zaidi hasa pale anapodai kwamba, uzukaji wa misimu ni wa ghafla na wakati fulani hufuatana na mambo au matukio maalum ya wakati au msimu huo. Anaendelea kufafanua kuwa misimu huzuka/huibuka na kutokeweka kufuatana na hali mbalimbali za kimazingira. Hata hivyo baadhi ya misimu hudumu na kuwa sehemu ya lugha. Kwa mfano neno matatu (Kenya) au daladala (Tanzania) ni neno lililotumika kurejelea nauli iliyolipwa miaka ya sitini. Hivi leo limekuwa neno linalomaanisha aina fulani ya magari ya usafiri. Katika muktadha wa mazungumzo misimu inachukuliwa kama ni aina mojawapo ya lugha ya mazungumzo itumiayo maneno yanayozuka kutokana na matukio mbalimbali ya kijamii, ambayo hiibuliwa na makundi mbalimbali katika jamii, hivyo misimu hutofautiana baina ya kundi moja na jinguine. Kwa mfano, misimu wanayotumia vijana ni tofauti na wanayotumia wazee au yanayotumia wanaume ni tofauti na wanayotumia wanawake.
Vilevile hata mazingira inamotumika misimu si mazingira rasmi kutokana na maneno yake kuzuka na kutoweka na hayatumiwi katika mazingira rasmi.
Agoti: ni lugha itumiwayo na kundi fulani la wahalifu au watu ambao wanaficha uovu wao usifahamike katika jamii wanamoishi. Mara nyingi lugha hii hutumiwa katika mazingira yasorasmi na kikundi kidogo cha watu kama vile, madereva wa magari, watumiaji wa madawa ya kulevya (mateja), majambazi, vibaka na wahuni wa mtaani. Mfano wa agoti inayotumiwa na watumiaji wa madawa ya kulevya ni kama vile, ndumu – bangi, sherehe ilikuwa na waalikwa wengi – soko la madawa ya kulevya lilikuwa na wateja wengi. Rejesta: Katika mazingira yasiyo rasmi, rejesta hutumia msamiati usio rasmi, matumizi ya misimu na ukatizaji wa maneno pamoja na udondoshaji wa baadhi ya vipashio katika maneno. Mfano, rejesta inayotumika katika mazingira yasiyorasmi kama vile mgahawani au hotelini ni kama vile nani wali ng’ombe? Ikiwa na maana kwamba nani aliyeagiza wali na nyama ya ng’ombe.
Utambulisho wa kijamii, Katika kipengele cha utambulisho wa kijamii tunaangalia namna aina ya lugha ya mazungumzo inavyoweza kujidhihirisha miongoni mwa watumiaji wake au kuwatambulisha na kuwatofautisha wanajamii husika. Lugha ya mazungumzo huweza kutambulika kutokana na aina zake, kwani katika jamii kila mtindo wa lugha ya mazungumzo una utambulisho wake katika jamii, kwa mfano agoti katika utambulisho wa kijamii unajulikana kama ni lugha ya wahalifu, jagoni ni lugha ya wanataaluma nakadhalika. Pia katika utambaulisho wa kijamii tunaangalia vile ambavyo mtu hutambulika katika jamii kulingana na namna anavyoongea kulingana na hadhi, tabaka, na jinsi ambavyo mtu huyo anavyoweza kusababisha mshikamano au mwachano katika mazungumzo. Kwa mfano jamii itamtambua mwanajamii kuwa ni msomi kulingana na mtindo wa lugha ya mazungumzo anaoutumia.
Nafasi yake: Katika kipengele hiki tunaangalia nafasi ya aina mbalimbali za lugha ya mazungumzo katika jamii husika. Je aina hizi za lugha ya mazungumzo kama vile agoti, rejesta, jagoni, lahaja na misimu zina nafasi gani katika nyanja mbalimbali za maisha ya mwanadamu? Kwa mfano, kiuchumi, kisiasa, kielimu na kiutamaduni. Tukianza na kiuchumi, kwa mfano rejesta, ina nafasi kubwa sana katika maendeleo ya kiuchumi kwa mtu binafsi na taifa kwa ujumla. Hii ni kutokana na kwamba, kwa mujibu wa King’ei (2010:94) madhumuni makuu ya mawasiliano katika biashara ni kuwavutia wateja na kuwafanya kuamini kuwa bidhaa ama huduma wanazouziwa ni za kiwango cha juu na ni thamani bora kwa pesa zao. Hivyo lugha ya biashara (rejesta), kwa kawaida ni lugha ya kutangaza uzuri wa bidhaa au huduma, huwa na sentensi au vifungu vifupi, mfano “Okoa mapesa chungu mbovu” pia huwa na lugha ya kupumbaza na kuaminisha, mfano “Kunywa XYZ kufumba na kufumbua afya yako itakurudia”.
Pia inasaidia sana kurahisisha mawasiliano miongoni mwa wazungumzaji katika masuala mbalimbali ya kibiashara na hata katika huduma mbalimbali za kijamii. Mfano hospitalini “mbili mara tatu”, hotelini “kuku wali tafadhali”, sokoni “kata nusu” na maeneo mengine. Baadhi ya rejesta na misimu hutumika kupunguza idadi ya maneno hivyo kufanya mazungumzo yawe mafupi na yanayoeleweka kwa urahisi mfano msimu “Daladala” kwa Dar es salaam linaweza kueleweka kwa urahisi zaidi kuliko kusema magari madogo yanayotumika kuchukua abiria chini ya 50 kutokea eneo moja hadi jingine kwa nauli ya shilingi 300. 
Pia rejesta za hotelini kama vile:- Muuzaji: wapi ng’ombe? Mteja: hapa Muuzaji: wapi chai chapati? Mteja: hapa. Si katika uchumi tu bali hata katika elimu rejesta ina nafasi muhimu sana, kwani zipo rejesta ambazo zinatumika katika maeneo rasmi kama vile shuleni katika kutolea elimudunia. Hapa rejesta inayotumika huwa rasmi na yenye kudhihirisha nidhamu. Mfano hutumika katika kuwanukuu watu wanaohusika katika maandishi ya kitaaluma, kama vile “kwa mujibu wa Pamphily, A. J. (2012) anafafanua kwamba…” 
Pia katika kutolea elimu ya dini kanisani na msikitini rejesta ina nafasi kubwa katika kujenga maadili. Vilevile rejesta na misimu ina nafasi ya kupamba mazungumzo, wazungumzaji wengi wanapozungumza hapa na pale hupenda kutumia maneno tofautitofauti kama vile misimu ili kufanya mazungumzo yawe ya kuvutia. Pia baadhi ya watu wanaona kuwa matumizi ya mitindo ya lugha ndio ujuzi wa lugha, hivyo hupenda sana kutumia mitindo hii ya lugha ili kuweza kurahisisha mawasiliano. Hivyo ina pendezesha lugha wakati wa mazungumzo. Mfano mazungumzo miongoni mwa vijana: 
Kijana 1: Jo? vipi tena mbona zii? Kijana 2: Poa Jo. Kama kawa… mambo mwaaa! Si rejesta na misimu tu, hata jagoni ina nafasi kubwa sana katika maendeleo ya kitaaluma, kwani wanataaluma mbalimbali hufanikisha malengo ya taaluma zao kupitia aina hii ya lugha ya mazungumzo. Mfano wahadisi, wahasibu, wanasayansi na washeria kila mmoja ana jagoni yake ambayo humsaidia kurahisisha mawasiliano miongoni mwao. Nafasi ya rejesta haiishii katika elimu au taaluma tu, bali hupea hata kuvuka mipaka ya kielimu na kutamalaki katika uwanja wa kisiasa. Hapa wanasiasa kama vile wanasayansi na wanasheria nao wana namna yao ya kutumia lugha. Mfano hupenda kuteua msamiati wenye kuleta mvuto na ushawishi katika jamii. Mfano maneno ya nasaha, kauli za kifalsafa mfano; “tumethubutu, tumeweza na tunasonga mbele” na uradidi wa vifungu mbalimbali vya maneno, hii yote inalenga katika kumfikirisha au kumpumbaza mtu kisiasa. Mbali na nafasi yake katika siasa, lugha ya mazungumzo kama ilivyo misimu, jagoni na rejesta agoti nayo ina nafasi yake miongoni mwa watumiaji katika jamii. Mfano wa nafasi ya agoti katika jamii ni kama vile: hutumika katika kujihami, kuficha na kuhifadhi siri za kikundi. Pia tusisahau kwamba mitindo mbalimbali ya lugha kama vile misimu inayo nafasi kubwa sana katika kukuza lugha hasa kwa kuongeza msamiati wa lugha husika, hasa misimu. Kwa mfano misimu iliyosanifishwa na kuingizwa katika lugha sanifu ni kama ifuatayo:- Daladala Basi la mtu binafsi linalotumika kusafirisha abiria mjini, linatumika zaidi Tanzania, jina lililotokana na nauli yake hapo mwanzo kuwa sawa na thamani ya shilingi tano ambayo ilikuwa ikijulikana kama dala kama msimu ilioibuka kipindi hicho. Kasheshe Hali ya kutoelewana inayotokana na watu kutokubaliana na jambo fulani.
Kwa kifupi tunaweza kusema kwamba aina zote hizo za lugha ya mazungumzo zilizojadiliwa hapo juu zina nafasi kubwa sana katika kikundi husika kinachotumia mtindo huo na katika jamii nzima kwa ujumla. Mfano wa nafasi yake katika matumizi ni kama vile kujihami, kujitetea, kukosoa, kurekebisha mienendo isiyokubalika, kukejeli, kutoelea maarifa, kurahisisha mawasiliano, kuficha au kuhifadhi siri za kikundi fulani, kupamba lugha na kutambulisha jamii husika au kikundi husika. Mfano wa rejesta zenye uficho ni kama vile:- Maneno ya mitaani maana katika lugha sanifu Demu msichana Kanyoosha goti kafariki. Kula kona ondoka. Mfano wa agoti zenye uficho:
Maneno ya madereva wa daladala maana katika lugha sanifu. Maiti Askari au mwanajeshi. (abiria asiyelipa nauli) Mchawi Gari linalokuja nyuma. Bibi Titi Askari mwanamke.
Matabaka, kwa mujibu wa kamusi ya Oxford (2004) ni kundi la watu wenye hali moja linalotokana na jamii yenye mfumo wa kiuchumi ambao hugawa watu.
Katika kipengele hiki cha matabaka, tutaangalia lugha kama kitambulisho cha jamii huwa na mitindo mbalimbali ya uzungumzaji ambayo huweza kuitwa aina mbalimbali za lugha ya mazungumzo. Aina hizi yaani rejesta, lahaja, jagoni, misimu na agoti ndizo zitakazo tudhihirishia uwepo wa matabaka mbalimbali miongoni mwa wanajamii. Njia mojawapo ambayo huweza kutumika katika kuonesha matabaka au tofauti za kijamii ni lugha azungumzayo mtu. Hii huweza kumtambaulisha kwamba yeye ni wa tabaka la juu au la chini, tabaka la wasomi au la wasiosoma, tabaka tawala au tawaliwa, tabaka la wenye nacho au la makabwela (wasio na kitu/masikini). Hivyo basi tujipe fursa ya kutalii matabaka haya huku tukihusianisha na aina ya lugha ya mazungumzo.
Tabaka la juu, yaani hili ni tabaka la watu ambao wana hadhi fulani katika jamii kama vile mamlaka au cheo. Tabaka hili katika uzungumzaji wao hutumia lugha rasmi, fasaha na yenye staha, uteuzi mzuri wa msamiati na miundo sahihi ya tungo, kwa lengo la kulinda hadhi na mamlaka yao na kujitofautisha na tabaka la chini. Mfano wa lugha inayotumiwa na kundi hili ni rejesta rasmi. Tabaka la chini, yaani watu wasio na hadhi au mamlaka yoyote katika jamii. Matumizi ya lugha katika tabaka hili si fasaha kutokana na muktadha waliomo. Kwani shughuli zao kwa kiasi kikubwa huzifanya baina ya wao kwa wao pasipo kuchangamana na tabaka la juu. 
Hivyo aina ya lugha ya mazungumzo itakayopatikana katika tabaka hili ni rejesta isiyo rasmi pamoja na lahaja. Tabaka la wasomi, hili ni tabaka la watu wenye taaluma fulani, mfano wadaktari, waalimu, wahasibu, wahandisi na wengineo. Aina ya lugha itayotumiwa na tabaka hili kulingana na taaluma zao ni lugha rasmi kama vile jagoni na rejesta rasmi. Tabaka la wasiosoma, hili ni tabaka pana sana ambamo ndani mwake mna makundi mbalimbali ya wazungumzaji kama vile makuli, wamachinga, wapiga debe, vijana wa vijiweni, mfano mateja, vibaka na majambazi. Kundi hili ni kundi ambalo lipo katika mazingira yasiyo rasmi kutokana na shughuli wazifanyazo. Hivyo ni wazi kwamba hata lugha wazungumzayo si rasmi. Mfano wa lugha ipatikanayo katika tabaka hili ni agoti pamoja na misimu.
Ieleweke kwamba, mgawanyo wa matabaka haya haimaanishi kuwa mzungumzaji wa tabaka fulani hataweza kuzungumza aina ya lugha au mtindo wa lugha wa tabaka jingine lahasha! Mzungumzaji wa tabaka lolote anaouwezo wa kuzungumza mtindo wowote wa lugha isipokuwa jagoni, kwani hapa mzungumzaji asiye wa taaluma hiyo hataweza kuzungumza mpaka awe na ujuzi wa taaluma husika. Hivyo mzungumzaji mmoja ataweza kuzungumza aina mbalimbali za lugha ya mazungumzo kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo; umri, mada ya mazungumzo, mahusiano baina ya wazungumzaji, muktadha na hadhira. Pia katika mazingira mengine mzungumzaji anaweza kujinasibisha na aina fulani ya lugha ya mazungumzo inayopewa hadhi ya juu kama vile rejesta rasmi, misimu au jagoni kwa lengo la kutaka aonekane kana kwamba naye ni watabaka la juu au la wasomi.
Hadhi; Msanjila na wenzake (wameshatajwa) wanaeleza kuwa lugha yenye hadhi ni lugha iliyosanifishwa na kutumika katika mawasiliano yote rasmi, kwa mfano shuleni, kanisani au shughuli za kiserikali, katika kipengele cha hadhi hapa lugha ya mazungumzo inazingatia nafasi aliyonayo mtu katika jamii yake. Kwa hiyo hadhi ya lugha huendana na hadhi ya wazungumzaji wa lugha husika, kwa mfano mwalimu, askofu, ustadhi au kiongozi wa serikali katika mazungumzo yake hutumia lugha yenye hadhi ambayo ni lugha rasmi ambayo imesanifiwa na kukubalika kutumika katika mawasiliano yaliyo rasmi. Hadhi ya lugha huweza kuibua mitindo mbalimbali ya lugha ambayo ni kama vile rejesta na jagoni. Kwa mfano rejesta za shuleni hutumia msamiati wa lugha yenye hadhi ambayo ina msamiati ulio rasmi, kwa mfano msamiati utakaozungumzwa na mwalimu ni msamiti rasmi kulingana na hadhi yake na hadhi ya lugha inayotumika katika mazingira yote ya shuleni. Vile vile msamiati utakaozungumzwa na Askofu, padre au mchungaji atazingatia hadhi yake na hadhi ya lugha anayoitumia katika mazingira ya kanisani. Msamiati utakaotumika ni msamiati wa lugha yenye hadhi. Vilevile katika mtindo wa jagoni tunaweza kupata msamiati ulio rasmi na unaotumika na watu wenye hadhi fulani katika jamii. Kwa mfano:-
Jagoni za kikemia. Msamiati wa kawaida wa kiswahili. H2O Maji O2 Oksijeni Co Hewa ya ukaa. Jagoni hizo huzungumzwa na watu wenye ujuzi wa kemia.
Jagoni za wanaisimu msamiati wa kawaida wa Kiswahili. Uwandani Mafunzo kwa vitendo Ndaki Vyuo vikuu. Ndiva Bwawa kubwa la kuhifadhi maji. Jagoni hizi huzungumzwa na wasomi. Kwa hiyo hadhi ya wazungumzaji wa lugha hufungamana sana na hadhi ya lugha waitumiayo katika mazungumzo. Kulingana na utofauti wa kihadhi walionao wazungumzaji katika jamii ni wazi kuwa utofauti huu utapelekea kutokea kwa mambo kadhaa, kama vile: • Upekee katika mtindo wa mawasiliano, mfano hotuba, mahubiri, mawaidha nakadhalika. • Adabu katika mazungumzo. • Upekee katika uteuzi wa msamiati kulingana na hadhi. Hivyo aina ya lugha itakayopatikana kulingana na hadhi ya mzungumzaji itakuwa ni rejesta rasmi. Hii ni kutokana na kwamba mazingira ya mchungaji, ustadhi, ofisa na viongozi wa serikali ni mazingira rasmi na ndio maana hata rejesta inayotumika ni rasmi. 
Msikamano na mwachano: katika utambaulisho wa kijamii dhana ya mshikamano katika aina mbalimbali za lugha ya mazungumzo, Crastal anfafanua dhana ya mshikamano kuwa inamaanisha mfanano wa uzungumzaji uliopo katika watu, familia, jinsi, tabaka moja, watu wenye hadhi sawa au shughuli sawa au makabila sawa. Kwa hiyo watu hawa watakuwa na mshikamano (mfanano) katika namna ya utamkaji wa vipashio mbalimbali katika maneno na pia watakuwa na mshikamano katika msamiati. Mfano, walimu, madaktari, machinga, wahandisi na kadhalika.
Dhana ya mwachano: katika lugha ya mazungumzo dhana ya mwachano inamaana kwamba ni ile hali ambapo wazungumzaji wa lugha moja hutofautiana katika baadhi ya vitamkwa katika maneno na pia hutofautiana katika baadhi ya msamiati. Mfano, Mhandisi na Daktari huweza kuwa na mwachano katika baadhi ya msamiati, kwa mfano, daktari anaweza kutumia msamiati kama vile “bomba” akimaanisha kifaa kinachotumika kwa ajili ya kudungia sindano wakati huohuo mhandisi atatumia neno hilohilo akimaanisha kifaa kinachotumika kusafirishia maji kutoka chanzo chake hadi kwa watumiaji, hivyo hali kama hii huweza kusababisha mwachano. Mwachano huu uliopo baina ya wazungumzaji huweza kusababishwa na mambo yafuatayo:
 • Elimu; Yule (1985) anasema kwamba hata wazungumzaji wasomi walio na usuli sawa wa elimu, mfano waliomaliza shule miaka ya hivi karibuni watakuwa na mwachano na wale wanaoendelea kusoma.
Shughuli/kazi; Yule (ameshatajwa) anasema kwamba shughuli au kazi wanazozifanya watu katika jamii watakuwa na kiasi fulani cha athari kwa kila mzungumzaji, hii ni kwa sababu kila kazi ina kiasi fulani cha jagoni ambacho hakihusiani na shughuli nyingine, hivyo itapelekea kutokea kwa mwachano.
Matabaka ya kijamii; Labov (1972) katika utafiti wake alioufanya katika jiji la New York aligundua kwamba kunamwachano mkubwa kati ya tabaka la chini na la juu, anasema kwamba sauti /˄/ kama katika neno sun /s˄n/ inatumiwa na tabaka la juu wakati tabaka la chini wanatumia sauti /ʊ/ katika neno hilo hilo, vilevile kiambishi tamati –ing katika neno kama vile coming kinatamkwa na tabaka la juu wakati tabaka la chini wanatamka kwa kuishia na kiambishi –in katika neno hilo hilo.
Umri; Yule anasema mwachano au mshikamano unaweza kusababishwa na umri wa wazungumzaji. Anasema kuwa hata katika tabaka fulani katika jamii, mwachano huweza kudhihirika kutokana na kigezo cha umri wa wazungumzaji, kwa mfano vijana waishio katika eneo fulani watatofautiana na wazazi wao katika namna yao ya kuzungumza.
Jinsi; hii pia hupelekea mwachano katika uzungumzaji, Yule anasema wasichana wanapenda kutumia miundo ya lugha ambayo inahadhi ya juu katika jamii, tofauti na wanaume ambao wote wana usuli sawa wa kijamii. Miundo kama I done it na he ain’t hutumiwa sana na jinsi ya kiume katika mazungumzo yao na miundo kama I did it na he isn’t hupatikana sana katika mazungumzo ya jinsi ya kike. Pia tofauti hujitokeza katika namna ya kutamka neno, matamshi hutofautiana namna wanavyotamka jinsi ya kike na jinsi ya kiume. 
Tukio; mwachano mwingine hutokea katika hali ya mzungumzaji kulingana na tukio lililoko mbele yake. Mfano, mzungumzaji anayekwenda kufanya usaili wa kazi atazungumza na katibu mhutasi: “samahani, meneja yumo ofisini? Nina miadi naye”. Mzungumzaji huyo huyo anapomuuliza rafiki yake juu ya rafiki yake mwingine atasema: oya, huyo mjinga bado amelala? Nataka kuonana naye juu ya jambo fulani. Kwa hiyo kutokana na tofauti hizi wazungumzaji wengi wana uamuzi wa kuchagua mwachano upi au mshikamano upi wafuate, mfano anapokuwa na mchumba wake, mpenzi wake, watoto, bosi, daktari, mchungaji, padri, au sheikh.
 Kwa ufupi David Crystal anasema kwamba, mwachano na mshikamano huonekana kwa urahisi pale ambapo meneja wa biashara fulani anapotumia lugha rasmi anapokuwa ofisini na kuhamia lugha isiyo rasmi anapokuwa nyumbani. Pia mhadhiri anapotoa mhadhara atatumia lugha rasmi na fasaha lakini anapokuwa na wahadhiri wenzake atajadili hoja hizo hizo katika lugha isiyo rasmi. Kimsingi dhana hizi mbili yaani mwachano na mshikamano ndizo hupelekea kutokea kwa aina za lugha kama lahaja, jagoni, rejesta, agoti na misimu.
Utambulisho wa kimuktadha. Katika kujadili kipengele hiki tutaangalia aina za lugha zinazojitokeza katika lugha ya siri na yenye mipaka, michezo ya matendo, kucheza na maneno, uganga kama miviga na utani kama miviga.
Lugha ya siri na yenye mipaka, ni lugha inayotumiwa na watu wawili au zaidi kwa kuzungumza lugha ambayo hubagua baadhi ya hadhira iliyopo. Lugha itumikayo haitoweza kueleweka kwa wale wasiolewa msamiti unaotumika, madhumuni ya kutumia lugha ya uficho ni kutaka mazungumzo hayo yawe siri baina ya wazungumzaji peke yao. Mara nyingi watu wanapotumia lugha ya uficho aghalabu misimu huzuka.
Mfano katika jamii ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kuna baadhi ya maneno yanatumika chuoni peke yake, iwapo maneno hayo yatatumika nje ya mazingira hayo ya chuo hayataeleweka kwa wanajamii wa nje ya chuo. 
Hivyo basi suala la mipaka ya kijiografia huingia katika suala hili. Mipaka ya kijiografia hutumika kuangalia jinsi msamiati kadhaa unavyotumika katika jamii bila kuvuka mipaka, kwa maana hiyo tunaweza kusema kuwa katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam kuna msamiati ambayo huwa na mipaka, haiwezi kutumika nje ya chuo.Mfano wa masamiati kama vile madesa, neno hili lina maana ya kitini, kitini hiki huweza kuwa na ukubwa wowote. Kwa mwanafunzi yeyote wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam msamiati huo wa madesa ni msamiati ulio vichwani mwao na kueleweka. Lakini iwapo msamiati huu utatumika nje ya chuo (nje ya mipaka ya chuo) utakuwa ni msamiati mgumu kueleweka kwa walio nje ya chuo mfano msamiati huu ukizungumzwa maeneo ya Tabata, Mbagala au Tanga wananchi wa maeneo hayo hawataelewa. 
Pia katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam kuna msamiati mwingine unaotumika ambao ni “darasa la saba” wanachuo waonapo askari huwaita darasa la saba neno hili linaweza kuwa na maana sawa na msimu. Katika mipaka ya ndani ya chuo neno hili lina maana ya askari. Iwapo wanafunzi wawili kutoka chuoni wakiwa katika mazungumzo katika mazingira ya nje ya mipaka ya chuo huku wakiwa katika mazungumzo yao wakiwaona askari basi watasema, “…unawaona darasa la saba?....” wakimaanisha askari. Hivyo kama kuna wanajamii walioko pembeni yao hawatoweza kuelewa chochote kwani hii ni lugha yenye uficho na yenye uwezo wa kuwa na dhima ya misimu. Ruti, neno hili linamaanisha maandamano katika chuo cha Dar es salaam. Neno hili linaweza kuwa sawa na hadhi ya misimu iwapo litatumika nje ya mipaka ya chuo halitaweza kufahamika kwa hadhira hiyo. Wanafunzi wakitoka nje ya mipaka ya chuo na kusema “ ...kesho tunapiga ruti…” Watu hawataelewa neno hilo litakuwa gumu kuelewa kwa wanajamii na litakuwa na uficho kwa wanaomzunguka yule anayeongea. Vilevile kikundi cha wahalifu kama vile wavuta bangi, hawa pia wana lugha siri na mipaka ijulikanayo kama agoti. Kundi hili huitumia lugha ya siri na yenye mipaka pale wanapokuwa katika vitendo vyao vya kihalifu. 
Lengo la kutumia lugha hii ni kuficha uhalifu wao kwa watu walionje ya kundi hilo. Kwa mfano wanapomuona askari utasikia wakisema “…soo mwana…” yaani wakimaanisha hali ya hatari. Hivyo basi kwa ujumla tunaweza kuona jinsi gani lugha ya siri na yenye mipaka inavyoweza kuzalisha lugha ya mazungumzo.
Michezo ya matendo: ni michezo ambayo aghalabu huendana na vitendo kutendeka kuendana na mazungumzo yanayozungumziwa. Mtu azungumzapo maneno fulani, basi hufanya vitendo vinavyolandana na maneno anayotamka. Katika jamii yoyote ile hapakosekani michezo, michezo hiyo inaweza kuchezwa na watu wa rika fulani, mfano watoto wadogo hawa wana michezo yao, pia katika umri wa vijana wanaobalehe au kuvunja ungo. Kwa mfano, katika mchezo wa watoto wa kujificha unaoitwa kombolela, katika mchezo huo watoto wengi hutakiwa kujificha sehemu mbalimbali na kumuacha mototo mmoja kulinda kopo moja lisigongwe na watoto wengine waliojificha na kuwakomboa wenzake. Neno “kombolela” limetokana na neno komboa, pindi mtoto mmoja anapojitokeza na kupiga kopo lile husema “kombolela” yaani nimewakomboa wenzangu.
Hivyo katika mchezo huu tutaweza kupata rejesta kama vile kombolela na pia katika mchezo huu mtoto mmoja akionekana na mlinda kopo basi mlinzi huyo hutamka neno moja (jina) la mtoto aliyemuona mfano Juma, Aziza, Salome au Ndege hapa akimaanisha nimemuona Juma, Aziza, Salome au Ndege. Hivyo atamkapo jina moja inamaanisha kuonwa kwa mtoto. Hii ni mojawapo ya lugha ya mazungumzo katika mchezo huu.
Pia katika mchezo mwingine wa vitendo ni mchezo wa karata, mchezo huu huchezwa na watu wenye umri tofauti tofauti, hutumia kadi ndogo ndogo zipatazo 54. Katika mchezo huu aghalabu tunapata lugha ya mazungumzo ambayo ni tofauti na lugha itumikayo katika michezo mingine kama mchezo wa mpira wa miguu, pete au ule wa watoto wa kombolela, hapa tunaweza kupata maneno tofauti tofauti kama vile:- “Lamba” neno hili linamaanisha ongeza karata au muda mwingine wachezaji husema “inama” wakimaanisha chukua karata au kadi ya ziada. “Lasti kadi” mchezaji iwapo amebakiwa na karata ya mwisho basi husema lasti kadi kumaanisha amebakiwa na kadi ya mwisho inayoweza kumaliza mchezo na kuibuka mshindi. 
Pia kuna maneno kama vile cheza mavi, kopa au kisu mchezaji mwingine, ataelewa lugha hiyo wakati wa kucheza mchezo. Neno jingine ni “geuza mchezo” mchezaji mmoja akitamka neno hilo basi humaanisha mwelekeo wa mchezo kama ulikuwa uelekee kushoto basi mchezo sasa utaelekea kulia, pia kuna neno stop, mchezaji akimaanisha mtu fulani aliye karibu yake katika mchezo anapaswa kusubiri, yaani asicheze kwanza. 
Kwa ujumla mchezo wa vitendo kama huu huwa na lugha yake ya mazungumzo ambayo kwayo tunapata dhana ya misimu na rejesta. Kucheza na maneno, ni mbinu ya kifasihi ambayo kwayo, maneno yanayotumiwa yanakuwa na hoja kuu ya kazi. Kimsingi hutumiwa kwa ajili ya kuleta athari iliyokusudiwa au kuburudisha. Mara nyingi mchezo wa maneno huusisha sifa zifuatazo, kutoa tabia za majina, maneno na maana zake zisizoeleweka kwa urahisi, usemaji wenye ujanja wa kuficha maana ya moja kwa moja na sentensi ambazo zinakiuka miundo ya kawaida ya sentensi. Mifano ya michezo ya maneno inayotoa tabia za majina ni kama ifuatayo:- Dar es Salaam = Lala salama Afrika nzima = Wazimana Tanga = Wanatanga tanga Wakenya = Wanakenyana Tanzania = Wanazamia Naiorobi = Wanaibiana Arusha =Wanarushana rushana Wasukuma = Wanasukumana Uganda = Wanagandana Mfano miundo ya sentensi zisizo na mpangilio maalumu kwa lengo la kuficha maana ya moja kwa moja. Kuzungumza kwa kupindua maneno na kuwa kinyume:- “naku zimwi ndapamea nyekwe riga”. Maana yake ni, kuna mwizi amepanda kwenye gari. Mfano mwingine wa kucheza na maneno, “katibu kata wa kata ya makata alikataza katakata kukata miti iliyo katikati ya kata ya makata”.
Vilevile katika lugha ya kiingereza mchezo wa maneno huweza kujidhihirisha kama ifuatavyo: “Katai is a maasai, Katai can tie and utie a tie, if Katai can tie and untie a tie why can’t I tie and untie a tie like Katai?”
Utani kama miviga, utani kama miviga ni kipengele cha lugha ya mazungumzo kinachoweza kuibua mitindo mbalimbali ya lugha. Oxford, (2004) wanaeleza kuwa utani ni taratibu za kimila ambazo zinawafanya watu kuambiana au kutendeana jambo lolote bila ya chuki, maneno ya kutania, dhihaka na masihara. 
Ipara, na Waituru, (2006) Utani ni kufanyiana mzaha au masihara baina ya watu na makundi mbalimbali katika. jamii. Maana ya miviga. Ngure, A. (kashatajwa) nafafanua kwamba miviga, ni sherehe za kijadi ambazo zinajihusisha na kumpa mtoto jina, harusi, mazishi, matambiko, kutawazwa kwa viongozi, unyago, jando na kadhalika. Utani kama miviga una umuhimu wake katika jamii, umuhimu huo ni kama vile kukumbusha mambo muhimu katika jamii, hapa mambo muhimu ni yale ya kihistoria ya jamii husika, pia hufundisha na kuadilisha, mila na desturi, maadili na tamaduni mbalimali katika jamii. Pia utani kama miviga huwa na dhima ya kuburudisha jamii. 
Vilevile utani kama miviga husaidia kuonyesha uhusiano iliopo baina ya wanajamii, kujenga na kudumisha mahusiano bora katika jamii, pia hutumika kutoa onyo, kutahadharisha jamii kwa njia ya ucheshi. Utani pia hujumusiha vitendo maalumu kama vile kuimba, kurukaruka na kucheza ngoma. Hivyo basi, kipengele hiki cha lugha ya mazungumzo huweza kuibua mitindo mbalimbali ya lugha isiyo rasmi ambayo ni kama vile rejesta na misimu.
Uganga kama miviga: Oxford wanafasili uganga kuwa ni kazi ya kuponya wagonjwa, utabibu, dawa. Mkwera, (hakuna mwaka) anadadafua dhana ya uganga kwa kuhusianisha na waganga. Anaeleza kwamba kuna waganga wa aina sita, katika makundi mawili. kundi la kwanza ni la matabibu wa kweli, waganga waponyao magonjwa. Hawa ndio waganga wa mitishamba wa dawa ndogo ndogo (waganga wa kienyeji), madaktari na wauguzi (hawa ni watu waliosomea elimu ya magonjwa mbalimbali, aidha teknolojia na njia mbalimbali zilizo safi na halali za uponyaji), waombezi (hawa ni waliokirimiwa na Mwenyezi Mungu karama (uwezo) ya kuponya. Kundi hili halina ushiriki na kusalia miungu. Kundi la pili ni wale naofanya uganga kwa kujishughulisha na kujihusisha sana na majini mizimu, kama vile waganga wa kitamaduni wa maradhi, wajuzi wa mazingira, wataalamu wa kienyeji na kadhalika. Katika kundi hili la pili wamo: wapiga ramli, walozi na wachawi.
Hivyo basi katika kipengele hiki tutaangali kwa jicho pevu uganga kama miviga unaofanywa na waganga walio katika kundi la pili. Uganga kama miviga ni sherehe maalum zinazofanywa kwa lengo la kuponya maradhi, kuagua, kutuliza miungu na mizimu, kuondoa mikosi na kutakasa wanajamii. Mara nyingi uganga kama miviga huambatana na matendo mbalimbali yafanywayo na mganga pamoja na washiriki wake. Matendo hayo ni kama vile kurukaruka, kuimba na kucheza na kububujika vifungu vya maneno visivyo na mantiki wala kueleweka. Kwa mfano, Mganga anamwita mhemba wake, “Msondo”
“Labekha Bwana”, aliitika Msondo.
“Lete lile pembe langu la tunguli, ubani, na kisu cha kuchinjia”
“Ewala Bwana”.
Anaendelea kububujika maneno yeye peke yake;
“Ndiyo, ndiyo, Nieleze Ruhani, yalikuwaje?”… “Kwa nini hunipi mfupa wa taarifa yote; ni wapi yalitokea yote haya?”… “Nani alimtuma? Kwa kisa gani? Ni nini akitakacho?”… “Ahaa! bibi yake alikwenda Bubuye kwa mganga na kuliomba hilo kombe?”… Mfano wa wimbo wakati wa shughuli za uganga, “Ee changu, changu njoo! Ee changu, changu njoo! Ee changu, change njoo!
Mlete babu mwamba, mlete yeye ajue’ Mlete yeye aone, mlete yeye tumchinje, Mlete yeye tumkamate; mlete, mlete, mlete!
Mlete, mlete, mlete! Mlete, mlete, mlete! Eee ee hoo; ee ee hoo; ee ee hoo!
Cheza, soma, toroka, itika, imba! Eee ee hoo; ee ee hoo; ee eehoo!”
Haya ni baadhi ya maneno ambayo pindi yatumikapo mara moja mtu hugundua ni mazingira ya nama gani yanazungumziwa hapa. Katika hali ya kawaida mtu asikiapo maneno kama hayo hawezi kuhusisha na mazingira ya kanisani, bali atahusisha na mazingira ya maeneo ya kiganga na nguvu za giza.
Kwa ujumla kipengele hiki cha uganga kama miviga, tunaona jinsi kinavyoibua mitindo ya lugha ya mazungumzo kama vile rejesta isiyo rasmi, lahaja, misimu ambayo huibuliwa na kutumika na makundi haya ya waganga. Pia agoti hujitokeza kwa lengo la kuficha siri ili mteja (mgonjwa) wake asigundue ujanja wake. Ifahamike kwamba mazingira haya si rasmi kama ilivyo kwa waganga wa kundi la kwanza, hivyo hata aina ya lugha ya mazungumzo itumikayo haitakuwa rasmi.
HITMISHO:
Kwa kuhitimisha tunaweza kusema kuwa katika kukamilisha dhana nzima ya matumizi ya lugha, tumeweza kuona uhusiano mkubwa uliopo kati ya mitindo mbali mbali ya lugha ya mazungumzo na utambulisho wa kijamii na kimuktadha na jinsi mitindo hiyo inavyoweza kutambulisha na kutofautisha makundi mbalimbali ya wazungumzaji katika jamii.


MOFOLOJIA YA KISWAHILI
Mofolojia-ni uwanja mdogo ndani ya isimu.
Isimu-Ni taaluma inayochunguza lugha ya binadamu kisayansi.
Mwanaisimu-ni mwanasayansi achunguzaye lugha ya binadamu katika nafasi zake zote yaani muundo, matumizi yake na nafasi yake katika jamii.
Isimu ina nyanja na matawi yake.
            MATAWI YA ISIMU
-Fonolojia
-Sintaksia
-Mofolojia
-Isimu nadharia
Nyanja za Isimu hushughulika na jinsi maneno yanavyoundwa. Mfano; mofolojia, fonolojia
-Matawi ya Isimu huhusu mikabala ya kuchanganua taarifa mbalimbali za lugha. Mfano; Isimu nadharia huchunguza vipengele mbalimbali vya lugha.
              MATAWI YA ISIMU
ISIMU NADHARIA
-Taratibu zinazobuniwa kuwawezesha wachunguzaji fulani wa lugha kufuata taratibu fulani.
ISIMU FAFANUZI
-Hutoa uchunguzi wa sarufi za lugha na huhusu uchunguzi wa lugha na familia ya lugha fulani na historia ya lugha hiyo katika mazingira yaliyopo
ISIMU HISTORIA
-Huangalia jinsi lugha ilivyokua hapo awali. Hutumika kulinganisha lugha kulingana na jamii zake ukajua kama uhusiano ni wa umbali au wa ukaribu fulani.
ISIMU JAAMII/ANTHROPOLOJIA
-Inajielekeza kwenye lugha kama sehemu ya kijamii mbali na jinsia. Huhusisha matumizi ya lugha na watu kama walivyo.
ISIMU KOMPYUTA
-Huhusu lugha asilia katika matumizi ya kompyuta na kubadilisha kwenda katika lugha ya binadamu kama mfumo.
ISIMU HISABATI
ISIMU NUROLOJIA -Huhusu misingi ya ki………..
ISIMU NAFSIA -Huhusisha utendaji/kuona jinsi mtoto anavyojifunza lugha, anaanzaje na anaendeleaje.
MOFOLOJIA
-Ni nyanja ya Isimu inayochunguza maneno na muundo wake. Huchunguza vipashio vinavyohusika na taratibu zinazotumika katika uundaji wa maneno.
-Neno huweza kuelezwa kifonolojia, kimofolojia nk.
-Neno  hutenganishwa na maumbo mbalimbali. Kwa mfano; A-me-ingi-a
-Katika neno huweza kuwa herufi au sauti katika uundaji wa neno. Kwa mfano; „m“
-Baadhi ya herufi ambazo huweza kuunda maneno ni kama; ot-, ka-, ki-, pat-, kop-, tek-, chot-, tembe-, nk.
-Hapa vipande vingi vinatumika kuunda maneno na haviwezi kutenganishwa zaidi.
                        VIPANDE
-Ni silabi ambazo huunganishwa kwa pamoja ili kuunda neno zima.
                        MOFOLOJIA NA FONOLOJIA
-Miundo na taratibu zake hizo ndizo huleta tofauti kati ya dhana mbili hizo hapo juu.
Mfano; Umbo sauti na sauti- kuna sauti ambayo hutamkwa kwa pamoja ambayo hutoa silabi na kuna sauti ambayo hutamkwa kimoja kimoja  au mojamoja.
-Mfano; Sauti hutamkwa kwa pamoja –kifonolojia
-Sauti kimofolojia- neno sauti ina kipande kimoja ambacho hakiwezi kugawanywa.
Mfano;-jina Juma
Juma-silabi 2
         -Herufi 4
NB: Vipande huitwa hivyo kwa sababu huwezi kuvivunja zaidi katika uundaji wa neno.
JINSI YA KUCHANGANUA MUUNDO KIMOFOLOJIA
-Ili kuchanganua muundo katika lugha si lazima kujua lugha husika au lugha hiyo.
-Jambo la msingi ni kupata orodha ya maneno na kujua muundo wa maneno hayo na namna yanavyoweza kubadilika.
Mfano; kitabu- vitabu
 1. Hivyo msingi wa kuangalia umoja na uwingi ni msingi mojawapo katika kuchambua muundo wa maneno.
2. Kutazama njeo katika neno                                                                                    
-Husaidia kuona miundo inayojitokeza katika neno. Kwa mfano; analala, alilala,    atalala, lakini viambishi awali huweza kubadilika kulingana na mazingira yake.
 1. Uwepo wa aina ya neno ambalo linaweza kubadilika kuwa aina nyingine ya neno.
Mfano; chafu-kivumishi
             Uchafu-Nomino
             Chafua-kitenzi
-Katika msingi husika hapo juu, mabadiliko hayo huweza kuwa katika mazingira;
a)     Hali shuruti(condicional variation)
Ubadilikaji wa umbo moja hadi jingine hutokana na ushurutishi.
Mfano; Cup- Cups
             Tag- Tags
b)     Mabadiliko huru
Mabadiliko katika lugha mbalimbali zenye mazingira huru haufuati mabadiliko mengine kama vile kuangalia njeo.
Mfano; Zapote-Mexico
             Analala= (R-ahsyab)-lugha ya kawaida
                          = (R-ahsy-ing)-lugha ya exima
            Pigisha – Pigiza
            Kwamisha – Kwamiza
            Katisha – Katiza
Hivyo basi, mabadiliko ya hali shuruti ndio ya kawaida kuliko katika mabadiliko huru katika lugha mbalimbali ulimwenguni.
-Katika lugha yoyote tunaanza kuona mabadiliko katika vipande
-Kuchanganua umbo la neno ni kutaka kujua vipande vya neno, hili ndilo kusudi la kuchanganua muundo na maumbo ya maneno.
-Wakati mwingine kugawanya maumbo kwenye vipande ni vigumu kupata/kutatua tatizo. Mfano; neno promise na promised, swear na sworeàNeno hili ni vigumu kulitenganisha kwenye vipande japo ni tofauti na la awali, zaidi hutusaidia kupata ojeo mbalimbali na kubadilika kutoka neno moja hadi jingine.
-Kipande huweza kuchanganuliwa katika mazingira mengine. Kina umbo lake.
Mfano; be, is , are , were, was,
-Hapa “be” kuwa na “is” hutumika kuonyesha umoja, was- mtu mmoja wakati uliopita.
-Hayo mazingira yamebadilishwa na njeo pamoja na idadi, pia I na Me ni mazingira yaleyale.
-Baadhi ya maumbo yanayobadilika kivipande; Louse-lice, Mouse-mice, sing –sang
i) Vipande vinadhihirika
ii) Vipande vinabadilika
iii) Mabadiliko ya maumbo lakini hakuna nyongeza ya maumbo yoyote. (Ablauti)
Mfano; sing-sang-sung hii kitaalam huitwa ABLAUTI kunakuwa hakuna mabadiliko yoyote ya maneno.
MFUMO MSONGE WA MUUNDO WA MANENO
-Ni mfumo unaohusu uambatishaji wa vipande kuunda neno na inaweza kujitokeza kama ifuatavyo;    
                                   N
                                   / \
                                Happy-ness
                                     |
                                    V
                     Maelezo (ma-elez-o)
                                      N
                                     /  |   \
                               Ma  elez  o

Uimbaji (U-imb-a-ji)
U – Kiambishi cha hali kamili
IMB – mzizi
A – Kiambishi tamati maana
JI – Kiambishi cha tendo linalojirudia.
Mfano; Fasten- Un-fasten-ed
Un – inatangulia na ed inafuata, hii ndiyo dhana ya mfumo msonge wa maumbo
Uundaji wa maneno huhusu utaratibu zaidi ya viambishi awali na tamati, kuna taratibu nne (4);
1. Taratibu za viambishi kati. Una umbo ambalo kwa kawaida huwezi kuruhusu kipande cha neno kuingizwa katikati.
Mfano; Bona- Boine (kihaya)
Kiambishi kati kinapenyezwa katika mazingira ambayo haikuwa rahisi kuwepo kipande.
2. Uambatano
Maneno mawili huwekwa pamoja kuunda neno, mfano; Churchhyard, blackbird, mlalahoi, mwanajeshi.
3. Uradidi
Umbo fulani hurudiarudia kuunda neno jipya. Mfano; barajara, sawasawa, kumbikumbi
NB: Viini ni kipande kilicho  na umuhimu wa kubeba maana.
                  Viini katika mfomo msonge kwa mfano;
-Mwanajeshi-kiini ni jeshi
-Mwanaume-kiini ni Ume
                                 N
                              /     \
                     Mwana    jeshi
-Maumbo haya yana matatizo yake katika uchambuzi/uchanganuzi wake kivipande. (Matawi) mfano; vilevile- vile- vile, mbalimbali- mbali- mbali.
-Katika maneno haya tunakosa viini vyake.
-Kiini ni muhimu katika maumbo yote yanayohusishwa katika kuchanganuzi wa baadhi ya ya maumbo. Lazima kujua kiini cha neno.
Mfano; ice cream- hapa lazima kujua aina ya neno kama ni moja au uhusiano wake katika neno.
Pia kuna maneno kama churchyard, blackbird, Redwood, sittingroom nk
Maneno ya muhimu kujua hapa ni bird, wood, room, yard.

Neno- Un happy
             |         |
 Kiambishi    Nomino
                  HADHI YA MANENO
-Wakati mwingine kuna nyongeza ambazo hazina uhusiano katika kuunda maneno.
KIANGAMI-Ni neno/kineno ambacho hakisimami peke yake ila huning’inizwa mwanzoni au mwishoni mwa neno.
Mfano; Mamako
-Kuongezwa kwa kipande hicho hakileti hadhi ya kuwa neno na ko haina maelezo yake zaidi ya kueleza maana zaidi.
-Hivyo kiangami hakifanyi kazi ya kufanya umbo kuwa neno.
-Kwa kawaida katika lugha, sentensi  hazina kikomo lakini neno/manenoyana kikomo.i.e. inajikita zaidi katika kutofautiana.
MATATIZO YA UCHANGANUZI WA KIMOFOLOJIA
-Kuna taratibu ambazo hupelekea matatizo katika uchanganuzi kama ifuatavyo;
i) Mofimu kapa
-Ni umbo lisilo na alama Dairy huweza kujitokeza katika ngozi ya maneno au ngozi ya sentensi. Afamo;  Godoro- Magodoro
-Kuna kitu ambacho hakijadhihirika katika neno godoro kuonyesha umoja.
-Katika muundo wa sentensi kwa mfano; neno ONDOKA (nafsi ya Pili umoja) inamaanisha mtu fulani aondoke hivyo kutokujidhihirisha lakini kuna kitu kinaonekana kuwa kinatajwa.
ii) Mofimu tatizwa
-Kuna mofimu ambayo inaanza kisha ikaingiliwa kati na mofimu nyingine kisha ikaendelea baadaye kukamilisha maana.
Kwa mfano; absolutely – absobloodylutly

                  MOFOLOJIA NA TAIPOLOJIA
TAIPOLOJIA
-Ni taaluma ya kiisimu ya kuainisha lugha kwa misingi mbalimbali.
-Misingi mojawapo ni ule wa kuangalia mpangilio wa vipashio katika sentensi  kuwa kuna kiima na kufuatia na kiarifu, kiarifu na kufuatia kiima, pia kuanza kutambua kiima na kiarifu
Mfano; bad boys
            Wavulana wabaya
-Msingi wa kimofolojia unaweza kuainisha lugha katika namna mbalimbali.
Kwa mfumo wa kimofolojia hutupatia aina tatu (3);
1. Msingi wa lugha tenganishi (isolate language)
-Maneno katika lugha hizi huundwa na kipande kimoja kimoja, kipande hakitenganishwiki. Mfano, lugha ya kichina, Vietnam
2. Lugha ambishi bainishi
-Vipande vinawekwa pamoja na kila kipande kina kazi yake. Mfano katika lugha ya kiswahili.
Unganishi-unga
3. Lugha ambishi
-Jinsi vipande mbalimbali vinavyoungana na kuunda neno. Lugha ya kilatini mfano, Domus-Nyumba yangu.
            UPAMBANUZI WA UAINISHAJI WA MOFIMU
MOFIMU
-Ni kipashio kidogo kabisa amilifu katika umbo la neno.
Udogo si wa umbo bali hakuna ugawanywaji zaidi ukaendelea hapa na kupata vipande vingine amilifu. Yaani huwezi kupata maana.
-Kuna mofimu inayoweza kuwa na herufi moja au zaidi, pia kuwa na urefu au kuwa na sauti zaidi. Mfano; jembe
-Katika lugha mofimu hujitokeza katika namna tatu (3)
1. Kiini
-Mofimu ni mofimu yenye kubeba maana ya neno husika. Mfano; mti
-Hiki kiini huitwa mzizi.
2. Kiambishi
-Ni kipande kinachoambikwa/pachikwa kwenye umbo muhimu/neno kuleta maana.
3. Maumbo yasiyogawanyika.
-Kuna maumbo yasiyogawanyika, hayaambikwi wala kugawanyika. Mfano; jembe
-Utokeaji wa namna hiyo hutupatia aina mbili za mofimu;
a) MOFIMU FUNGE
-Ni kipande ambacho hakiwezi kusimama peke yake kisarufi.
Mfano; m-katika neno mti.
M-Ni funge katika mazingira haya ya lugha(sarufi hii) pia umbo t-halina maana, hali kadhalika i, ili kufanya kuwa neno ni  lazima yaungane pamoja.
b) MOFIMU HURU
-Ni maumbo yanayoweza kusimama peke yake kileksika na kisarufi.
Hivyo basi ni vyema kujua kinachoitwa mofimu na neno ili kutoa dhana inayoeleweka na kutofautisha.
Mfano neno OMBA
OMBA
-Lina silabi 2
-Lina herufi 4
-Lina sauti 3
-Lina mofimu 2
OA
-Lina herufi 2
-Lina mofimu 2
-Lina sauti 2
-Lina sauti 2
Hivyo basi kila sauti inaumbiwa sauti yake katika neno.

            TOFAUTI KATI YA MOFIMU NA NENO
-Kwa mujibu wa JOHN LION (1968) “An introduction to theoretical linguistics” Anaona kuwa neon linafafanuliwa au haliwezi kufafanuliwa kwa,
i) Kiotografia-namna neno linavyoandikwa.
ii) Kisarufi-kinachowakilishwa na umbo husika.
iii) Sauti-maana inayohusika katika neno husika.
-Kuna wakati maana na sauti hufanana na pia maandishi na sauti hutofautiana.
Mfano; enough-inafu
            Liuntenant
-Tafauti za maandishi na maana hufanya lugha kuwa ngumu kujifunza.
-Pia katika kiswahili kuna maneno ambayo huwa tofauti na yanavyoandikwa katika utamkaji wake.
Mfano; nje, mba, nge, mbu, ng’ungwe nk
-Pia kuna uwezekano wa maandishi na matamshi kufanana.
Mfano; kaa(hutamkwa kwa mpumuo)
 Ikiwa na maana mdudu, kuna dhana nyingi hutokea katika neno hili.
Hivyo basi neno huweza kufanana na kutofautiana kimatamshi, kimaandishi na pia kisarufi. Hivyo si kila neno ni mofimu.
-Zipo dhana mbili ambazo huhusishwa na mofimu ambazo ni;
a) MOFU
b) ALOMOFU
            MOFU
-Ni kipashio cha kimaumbo kinachowakilisha mofimu.
-Huweza kuwa sauti au herufi. Mfano huweza kuwakilishwa na herufi moja au zaidi, sauti, silabi moja au zaidi. Mfano;godoro-magodoro, kiti-viti
            ALOMOFU
-Ni viwakilishi viwili au zaidi vya mofimu moja lakini hujitokeza katika mazingira fulani / tofauti ya kimtoano.
Mfano neno mtu
/m/ limejitokeza kutokana na mazingira yake lakini katika mazingira ya m-wa neno /m/ litabadilika.
MOFIMU NA UTARATIBU WA UUNDAJI WA MANENO KATIKA KISWAHILI
-Utaratibu wa kawaida ni wa uambishaji wa viambishi katika mzizi.
-Uambishaji aidha uanze kabla au baada ya mzizi. Ila kwa kawaida viambishi hutanguliwa na mzizi.
Mfano; m-ti
             |    |-mzizi
        Kiambishi
-Katika kiswahili mara nyingi mzizi hutanguliwa na viambishi.
            Vivumishi
Mfano; zuri, baya
            Vitenzi
Mfano; pea, pevu
            Vielezi
Mfano; vizuri
-Vielezi vikiambishwa hutanguliwa na kiini.
                        UAMBISHAJI
-Mchakato wa ujumla wa uambishaji wa viambishi kwenye mzizi.
Mfano; promise-promised
            Connect - connection – connectivity
                 |                 |                        |
                 T                N                     V
-Uambishaji unahusu dhana mbili;
a) Unyambuzi
b) Uambatizaji
-Kila moja huhusika na utaratibu wa aina tatu;
*Kuunda mzizi mpya
Mfano; a-na-lala
    a-nafsi ya tatu umoja  na-njeo (Huu ndio uambatizaji)
-Neno lala-mzizi-lal
Unaweza kupata neno jingine
Mfano; lalia-lalika
               \            /
           Unyambatizaji
-Hupata maumbo mengine ya maneno
NADHARIA YA MOFIMU NA MOFOLOJIA YA KISWAHILI
-Mofolojia ni kiwango cha kimuundo kati ya fonolojia na kisintaksia.
-Inaeleza muundo wa ndani wa neno.
-Sintaksia inafafanua jinsi maneno yanavyowekwa pamoja katika sentensi.
NADHARIA YA MOFOLOJIA YA KISASA
-Inatazamwa katika pande tatu (3);
a) Inachunguza vipashio vya msingi vya muundo wa mofolojia.
b) Je vipashio hivi vimejidhihirishaje katika muundo wa kimofolojia?
(c)   Ni kigezo kipi kinatumika kuamua muundo wa kimofolojia?
-1940-1950 maswali yamepewa majibu mepesi.
-Miaka ya hivi karibuni suala la vigezo limewekwa kando na haya maswali yamejibiwa.

-Kati ya mwaka 1940-1950
Maswali mawili ya mwanzo yalipewa majibu. Katika miaka ya hivi karibuni suala la vigezo limewekwa kando na maswali mawili yamejadiliwa sana.
-1950 ilikuwa kipindi maalum cha uchunguzi wa kifonolojia.

-Hocheti (1954) alibainisha dhana tatu (3);
i) Kipashio na mpangilio (item and remarks)
ii) Kipashio na mchakato (item and process)
iii) Neno na kielezo cha mfumo (Word and paradigms)
-Dhana (1-2) ni dhana ambazo hueleza kipashio na mpangilio.
-Hapa muundo wa maneno huweza kufanana na maumbo mengine.
-Mfano; farmàfarm-er-s= farmers
              SingàSing-ing=singing
-Hapa umbo huongezwa mofimu moja na kuwa nomino.
-Vipashio ni vipande vya kisarufi vya kidhahania vyenye kufanana na vipande vinavyojitokeza katika kuunda maneno ambapo pengine maumbo yake ni tofauti kabisa.
-Dhana ya kipashio na mpangilio hutoa majibu kwa maswali mawili ya kwanza.
-Vipande vinavyojirudiarudia ndivyo huitwa MOFU.
-Uchunguzi wa kimofolojia katika kipashio na mpangilio ulihusisha;
i) Ubainishaji wa orodha ya vipashio
ii) Kubainisha mifuatano ya mofimu
iii) Kubainisha mofu inayojitokeza/inayodhihirisha mofimu (uhusiano mkati ya vipengele vya kisarufi vya muundo wa kimofolojia na kifonolojia)

Dhana hii ilikosolewa kwa namna mbalimbali;
-Kuwepo kwa maneno yasiyogawanyika katika mpangilio maalum.
-Kutokana na kukosolewa huku ndiko kulitokea na dhana hizi nyingine mbili;
Mfano; Penda-penzi (kuwepo kwa mabadiliko)
Mfano; zote hutamkwa katika eneo moja. Gomba- gombi
-Kuwepo kwa kipashio kimoja kunaweza kubadilisha umbo jipya.
Mfano; ogopa-ogofya

-Kipashio na mabadiliko minaanza kueleza mpangilio na kipashio.
Mfano; gomvi-gomba
            Fuata –mfuasi
i) Kubainisha umbo la msingi
-Kuona kitu kinachoongezwa katika umbo la msingi ambalo linaweza kuleta mabadiliko.
Mfano; sing – sang
-Kilichochochea mabadiliko ni kuwepo kwa wakati.

            Mabadiliko ya kimofofonimu
-Mabadiliko yanayohusu kimofolojia na kisauti.
-Kitu kinapokuwa katika mazingira fulani huchochea mabadiliko.
Mfano; mapenzi-mpendwa
             Penzi-pendo
-Kwa nini kumetokea mabadiliko ya “Z” na “D”

3) Dhana ya kielelezo cha mfumo.
-Dhana hii kimsingi inahoji kanuni ya alama tenganifu.
-Vipashio ambavyo vinaweza kutenganishwa na nafasi yake ikachukuliwa na kipashio kingine.
Mfano; Lugha ya kiitaliano
      UMOJA                            UWINGI
-Donna-Mwanamke                Donne-Wanawake
-Monte-Mlima                         Monti-Milima
-Raggazo-Kidole                      Dila-Vidole

-Katika Donna-Donne unaweza kutenganisha a na e
Je katika mazingira hayo ni nini unaweza kuhusisha  na umoja na uwingi?

Umoja (Mountenable) Uwingi (Mountenables)
              New horizons and linguistics

Mfano 2; Kiitaliano
-Kipashio kimoja kinaweza kuhusisha dhana kadhaa.
Mfano; Cantarrebbene- Kama wangeimba(nafsi ya 3 uwingi)
Hapa kunajitokeza sharti la nafsi ya 1
Rebberro (kubainisha sharti nafsi ya 3 uwingi kwa mazingira yapi?)

Sharti limo katika sauti rre na bbe

                re                                  bbe                           rro
            /  |       \                             |                      /     |       \
     Nafsi sharti wingi              Nafsi            wingi nafsi sharti 
   
-Dhana hii inakosolewa kwani  imejikita zaidi katika kutazama neno na kuvuka mipaka ya kimofolojia.
-Ni dhana ipi inaweza kutumika katika maelezo ya kimofolojia.
-Dhana ya kipashio na imeonekana kuwa ni mwelekeo zaidi kwa ujumla wake inakwenda mbele ya kipashio na mpangilio.

Dhana ya kipashio imekosolewa kwa viwango kadhaa.
-Kuchukuliwa kuwa na umbo la msingi
-Kuonekana kwa mabadiliko

            UNYAMBUZI/MICHAKATO YA KIMOFOLOJIA
-Katika ligha maneno mapya huingia kwa njia kuu mbili (2);
i)                   Kuingiza maneno kutoka katika lugha nyingine
ii)                 Kujenga maneno kimofolojia hasa maneno yaliyo katika makundi ya wazi.
-Kuongeza mofimu kwenye mofimu iliyopo (Unyambulizi)
-Mofimu nyambulizi huhitajika kwa namna inayotofautiana na mofimu ambatishi.
Mfano; Zuri (V) + M-Mzuri(V)
            Chek+aàCheka + esha àChekesha
            Chek + lea àchekelea
Hivyo basi tumetumia mzizi “M” kupata maneno mapya
         U-chek-esh-a-ji àUchekeshaji
-Mofimu nyambuzi huongeza msamiati na kuwasaidia watumiaji katika kuwapa uhuru wa kuzungumza.
-Kuwepo kwa mofimu nyambuzi katika lugha hakuhusiani na muundo wa sentensi.
 Mfano; establish + ment àEstablishment.

MAKUNDI YA MANENO
i) MAKUNDI YA WAZI
-Katika lugha kuna aina mbalimbali za maneno ambazo zina taratibu zake ambazo zinafanya ziwe wazi au zimefungwa hivyo tunaweza kupata makundi mawili.
ii) Makundi ya wazi na ii)Makundi yaliyofungwa
-Aina ya maneno katika lugha ambazo unaweza nkuyaingiza maneno mapya bila kizuizi.
Mfano; nomino, kitenzi, kivumishi, kielezi nk.
(iii) MAKUNDI YALIYOFUNGWA
Mfano; viunganishi kama vile “na, lakini, walakini nk ni maneno ambayo hayaruhusu maneno mapya kuingia kwa namna mbalimbali.
-Viingizi=Maneno yanayotangulia katika kuunda sentensi.
Mfano; Yesu na Maria.
-Uuundaji wa maneno mapya unahusu ubadilishaji wa maneno kuunda maneno mengine. Mfano; uchekeshaji-ucheshi-vichekesho- vyote ni nomino za aina moja.
-Unaweza kupata vivumishi kutokana na kivumishi, nomino, kitenzi nk
-Unaweza kunyumbua maneno ya aina mbalimbali, hapa tutaanza na unyambuzi wa vitenzi.
-Kitenzi ni maneno yanayotoa taarifa juu ya tendo linalifanyika au linalotendwa na kiumbe au kitu.
-Imefafanuliwa kwa kutilia maanani kama/kwa namna linavyotumika katika sentensi.

                        AINA ZA VITENZI
i)                   Kitenzi kikuu mfano; Analala
ii)                 Kitenzi kisaidizi mfano; Alikuwa analala
iii) Kitenzi kishirikishi mfano; Huyu ni mtoto.
-Msingi uliotumika katika kuunda aina za vitenzi ni wa kisintaksia sio kimofolojia.
-Msingi wa kimofolojia wa uainishaji wa sentensi ni kutazama umbo la kitenzi ambalo linaweza kupatikana katika kamusi.
Mfano; la-la
             Kul-a-la
             Kuj-a

            MAUMBO YA VITENZI
-Mizizi yenye sauti au herufi mbili
Mfano; Ol-a, On-a
-Jumla ya maneno
Mfano; Pon-a, lal-a
-Sauti tatu na herufi nne
Mfano; Teng-a, Pang-a
-Maumbo ya vitenzi yenye sauti tatu na herufi sita
Mfano; Shang-a, Chungu-a
-Sauti sita na herufi saba
Mfano; Tengam-a

-Katika kiswahili kiuna maneno yamekopwa kutoka katika lugha nyingine  mfano, rudi, adabu, hakiki nk
-Maumbo hayo pia hubeba maana fulani ambapo yanaweza kuwa na sifa mojawapo kati ya hizi mbili;
i) Sifa elekezi, huwa ndani ya mzizi.
-Kwa kawaida kitenzi hicho huambatana na yambwa nyingine kwa lazima.
Mfano; O na a, O- imeruhusu kuandamana na yambwa.
iii)    Si elekezi- Ni mizizi isiyolazimisha kitenzi kuambatana na kipashio kingine.

            VIAMBISHI NYAMBUZI KATIKA LUGHA YA KISWAHILI
i)     Kiambishi kitendwa. Hiki huwakilishwa na kiambishi “wa”
ii)    Kiambishi kitendeka. Huwa mna umbo la “ik”, “ek”
iii)   Kiambishi kitendeshi. Huwa na maumbo ya ish, esh, iz, ez
iv)    Kiambishi kitendea. Huwa na umbo la i/e, il/el
v)      Kiambishi kibadilifu (reversive). Huwa na umbo la o/u
vi)     Kiambishi kifungamanishi (static). Huwa na umbo la am
vii)   Kiambishi kishikanishi (contactive). Huwa na umbo la al
       viii)  Kiambishi kitenganishi (resprocal). Huwa na umbo la –an-
NB: Hivi ni viambishi tofauti na viambishi vingine tulivyoviona.
Mfano; Teng-a. a - ni kiambishi kuonyesha dhamira.
                          e - ni kiambishi chenye dhamira ya kimatlaba (kuonesha nia ya jambo) mfano; Niondok-e, nisem-e

SWALI: Jadili tofauti kati ya uamiliaji lugha na ujifunzaji lugha.

 DONDOO:
Utangulizi kwa ujumla. 
Maana ya lugha 
Maana ya uamiliaji lugha 
Maana ya ujifunzaji lugha 
KIINI: 
Utofauti uliopo baina ya Uamiliaji lugha na Ujifunzaji lugha.
HITIMISHO: 
MAREJEO:
Mwanadamu anapozaliwa anakuwa na bohari la sauti mbalimbali zisizo na maana yoyote, na mara anapoanza kuishi katika jamii ndipo huanza kuibua sauti hizo katika mazingira ya kinasibu (pasipo yeye mwenyewe kutarajia) na kuanza kuzitafutia maana sauti hizo. Uibuaji wa sauti hizo huendana sambamba na mambo yanayomzunguka pamoja na yale anayoyatumia.
Hii tunaona hata kwa watoto wachanga jinsi wanavyoanza kuongea, kwanza huanza kwa kutoa sauti zisizo na maana yoyote kisha kadiridi wanavyokuwa ndivyo sauti hizo zinaanza kubadilika mpaka zikaeleweka na watu wanaomzunguka. Yote haya ufanyika kutokana na msaada wa mazingira, muda pamoja na jamii inayomzunguka.
Hivyo basi tunaona kwamba dhana ya uamiliaji lugha huanza mara tu mtoto anapozaliwa kisha hufuatiwa na dhana ya ujifunzaji lugha. Pamoja na hayo yote wapo wataalam mbalimbali waliojaribu kuelezea dhana hizi mbili kwa mapana zaidi huku wakitoa tofauti mbalimbali kati ya uamiliaji lugha na ujifunzaji lugha.  
Kwa kuanza na maana ya lugha, wanaisimu wengi wamewahi kutoa fasili mbalimbali kuhusiana na dhana ya lugha, miongoni mwa wanaisimu hao ni pamoja na;
Trudgil (1974) ambaye amenukuliwa na Mgullu (1999). Anasema kuwa “Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zinazotumiwa kwa mawasiliano miongoni mwa watu wa jamii fulani yenye utamaduni wake.
Mtaalam mwingine ni Sapir (1921) ambaye anasema kuwa Lugha ni mfumo ambao mwanadamu hujifunza ili autumie kuwasilishia mawazo, maono na mahitaji. Mfumo huu hutumia ishara ambazo hutolewa kwa hiari.
TUKI (1990) inasema: Lugha ni mfumo wa sauti zinazotumiwa na watu wa jamii fulani wenye utamaduni unaofanana ili kuwasiliana.
Kwa mujibu wa Msanjila na wenzake (2011) wakimnukuu Massamba (2004:19) wanasema kuwa “Lugha , kwa upande wake, hufasiliwa kuwa ni mfumo wa sauti nasibu ambazo zimebuniwa na jamii kwa madhumuni ya mawasiliano kati yao”. Jambo la msingi la kuzingatia katika fasili hii ni kuelewa kwamba dhima kuu ya lugha ni kuwezesha mawasiliano miongoni mwa jamii yaweze kufanyika.
Hivyo basi katika fasili zote hizi tunaweza kusema kuwa wataalam hawa kimsingi wanakubaliana kuwa lugha ni mfumo wa sauti za nasibu ambazo zimekubalika zitumike miongoni mwa wanajamii kwa lengo la kuwasiliana.
Pia dhana ya uamiliaji lugha imefasiliwa na Garman pamoja na Fletcher (1986) kama walivyonukuliwa na Hickman; wanasema kuwa, Uamiliaji lugha hautokei katika ombwe (patupu) kadiri watoto wanavyoamili lugha wanaamili mfumo wa ishara ambazo zinaonesha uhusiano muhimu katika nyanja ya ubongo na nyanja ya jamii katika maisha.
Naye Stephen Krashen na Tracy D.T (1983) wamejaribu kuelezea dhana hii ya uamiliaji. kwa kusema kuwa uamiliaji ni mchakato unaotokea katika nafsi iliyofichika akilini mwa mtu ambayo ndiyo imuongozayo kuongea au kuandika kwa urahisi. Hivyo wao wanaona kuwa uamiliaji hujitokeza kwa mtu katika hali ya ung’amuzi bwete pasipo muhusika mwenyewe kujitambua.
Na katika ujifunzaji lugha, Krashen na Tracy (1983) wanadai kuwa ujifunzaji ni mchakato wa kiufahamu wa kiakili au utambuzi wa nafsi unaojionesha katika kujifunza sharia na kanuni na miuundo ya lugha. Hivyo basi katika dhana hii wao wanaona kuwa ujifunzaji ni tukio la kiutambuzi, yaani mtu ana kuwa anafahamu au anatambua kuwa anajifunza lugha hivyo atapaswa kuzingatia kanuni na muundo wa lugha.
Mtalaam mwingine ambaye anaonesha kukubaliana na akina Krashen na mwenzake ni Gleason (1989) ambaye naye anaona kuwa uamiliaji lugha ni sawa na tukio linalotokea katika ung’amuzi bwete wakati ujifunzaji hutokea katika ung’amuzi tambuzi. Katika kuthibitisha hilo anasema kuwa;
Ujifunzaji lugha unazingatia kujua vipengele muhimu vya lugha ambavyo si lazima kuvifuata au kuvijua katika uamiliaji lugha bali vinakuja vyenyewe pasipo utambuzi au pasipo kujua. Vipengele hivyo ni kama vile; fonolojia, mofolojia, sintaksia, semantiki na pragmatiki.
Baada ya kutazama fasili na mitazamo mbalimbali iliyotolewa na wataalam hao juu ya lugha, uamiliaji lugha na ujifunzaji lugha, zifuatazo ni tofauti zilizopo kati ya Uamiliaji lugha na ujifunzaji lugha.
Uamiliaji lugha hutokea katika ung’amuzi bwete yaani pasipo mtoto wenyewe kujitambua kiakili, anajikuta tu ana uwezo wa kuzungumza vizuri bila kujua kwa nini anazungumza hivyo, wakati ujifunzaji lugha ni tukio la kiutambuzi. Yaani mtu anajua fika kwamba anajifunza lugha.
Vile vile katika uamiliaji lugha si lazima kufuata sharia na kanuni za lugha au vipengele vya lugha lakini katika ujifunzaji lugha lazima mtu aelewe vipengele vyote muhimu vya lugha.
Pia katika ujifunzaji lugha lazima kuwepo na mwalimu ambaye ni mtaalam wa lugha pamoja na mazingira fulani muhimu ambayo yatamfanya yule mjifunzaji lugha kuweza kujifunza lugha kwa urahisi zaidi. Mfano wa mazingira hayo ni kama vile shule au taasisi maalum kwa ajili ya ujifunzaji lugha. Lakini katika uamiliaji lugha haitajiki mtaalam wa lugha wala mazingira maalum kama hayo.
Vile vile katika uamiliaji lugha utamaduni wa jamii husika hauzingatiwi sana lakini katika ujifunzaji lugha lazima mjifunzaji lugha aelewe na azingatie utamaduni wa jamii husika ili kuepuka makosa ambayo yanaweza kusababisha uhusiano mbaya na wanajamii husika.
Vile vile uamiliaji lugha ndiyo unaotangulia kisha hufuatiwa na ujifunzaji lugha. Yaani mtoto huanza kuzungumza pasipo kujua taratibu za lugha kama vile, muundo wa lugha, kanuni za lugha na utamaduni wa lugha husika. Baada ya kujua kuzungumza ndipo hufundishwa sharia mbalimbali za lugha husika.
Pia kwa mujibu wa Jean (1992:123) anasema kuwa katika uamiliaji lugha watoto wachanga wanakuwa makini katika lugha tangu wanapozaliwa. Wanaanza kutoa maneno yanayotambulika katika kipindi cha miezi 12-15 na kuanza kuyaunganisha maneno hayo kuanzia miezi 18. Anaendelea kusema kuwa watoto wote wasio na matatizo ya kimaumbile na baadhi ya wenye matatizo, wataanza kuongea ikiwa watasikia lugha ikizungumzwa katika mazingira walimo. Hii ni tofauti na ujifunzaji lugha kwani mtu hata waze kujifunza lugha kwa njia ya kusikia tu.
Tofauti nyingine ni kwamba uamiliaji lugha una kikomo lakini ujifunzaji lugha hauna kikomo kwani unaendelea katika umri wowote haijalishi kijana au mzee.
Hivyo basi ninaweza kuhitimisha kwa kusema kuwa mtu yeyote anao uwezo wa kujifunza lugha na kuifahamu ikiwa tu atakuwa na akili timami pamoja na ala sauti zote zinazohusiana na ujifunzaji lugha ambazo hazijaathiriwa au kuathirika sambamba na kupewa mazingira ya kijamii ya kujifunza lugha ingawaje hatafikia uwepo wa uamiliaji.
MAREJEO:
Aitchison, J. (1992). Teach Yourself: Linguistics. (4th ed). Hodder & Stoughton Ltd. Britain.
Berko, G.J. (1989). The Development of Language. A. Bell & Howell Information Company.
Fletcher, P. and Garman, M. (1986). Language Acquisition. Cambridge University Pess.
Krashen, Stephen D. and Tracy D. Terrell (1983). The Natural Approach. Language Acquisition in the Classroom: Pergamon Press. Oxford.
Mgullu, R.S. (1999). Mtalaa wa Isimu: Fonetiki, Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili. Dar es Salaam. Longhorn Publishers (T) Ltd.
Msanjila, Y.P. na wenzake. (2011). Isimujamii: Sekondari na Vyuo. TUKI. Dar es salaam
TUKI (1990). Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha: TUKI. Dar es Salaam.

SWALI:
“Kwa hakika hakuna tofauti kati ya vivumishi na vikumushi.” Hakiki kauli hii kwa mifano.
DONDOO:
UTANGULIZI
Maana ya vivumishi 
Maana ya vikumushi
KIINI:
Uthibitisho uonyeshao kuwa hakuna tofauti kati ya vivumishi na vikumishi.
Utofauti uliopo baina ya vivumishi na vikumishi.
HITIMISHO
 Wazo kuu katika ufanano na utofauti kati ya vivumishi na vikumushi.

Vikumushi na vivumishi ni dhana mbili ambazo zimekuwa zikileta mkanganyiko mkubwa sana katika taaluma ya isimu. Maneno haya huweza kufanana na kufanya kazi sawa, lakini kwa upande mwingine huweza kutofautiana. Kama inavyojadiliwa hapa chini.
Chuo kikuu cha Oxford (2005) wamefasili kikumushi kuwa ni neno ambalo linaweza kuwa kivumishi au kielezi ambacho kinaelezea neno au kundi la maneno mengine (tafsiri). Katika fasili hii maana ya kikumishi imetolewa kiupana kwa kiasi fulani, lakini bado kikumushi kinaweza kuwa zaidi ya kivumishi au kielezi, na kuwa kitenzi na aina nyingine za maneno.
Khamisi na Kiango (2002:58) wameeleza maana ya kikumishi kuwa ni maneno ambayo siyo vivumishi asilia, lakini hufanya kazi kama vivumishi, yaani kazi ya kukumusha (kuongeza sifa au taarifa muhimu) nomino. Wanaendelea kusema kuwa vikumishi siyo vipashio vilivyo katika kiwango cha neno tu, bali ni pamoja na makundi ya maneno ambayo yamo katika kiwango cha kirai au kishazi. Mfano; Kikumushi nomino baba watoto. Kikumushi kirai baba wa taifa. (KH) Kikumushi kishazi mtoto aliyeshinda.
Hivyo basi kutokana na fasili hizo mbili zilizotolewa tunaweza kusema kuwa kikumushi huweza kufasiliwa katika mawanda finyu na mawanda mapana.
Katika mawanda finyu; kikumushi ni maneno yanayotoa taarifa ya ziada kuhusu nomino. Mfano; watoto wangu, mtoto wa juma. Maneno wangu na wa Juma ni vikumushi vya nomino watoto na mtoto.
Katika mawanda mapana: kikumushi ni maneno yanayotoa taarifa ya ziada kuhusu aina nyingi ne yoyote ya maneno yaani nomino, kitenzi, kielezi. Mfano; aliyeimba kwa madaha, Mfano wa pili; Anacheza    vizuri sana. Neno kwa madaha  na vizuri sana yanakumumusha vitenzi aliyeimba na anacheza vizuri.
Kwa upande mwingine kivumishi kama aina mojawapo ya aina za maneno imefasiliwa na wataalamu kama ifuatavyo; Matei (2009:43) anasema kuwa “kivumishi ni neno ambalo hutoa maelezo zaidi kuhusu nomino au kiwakilishi cha nonimo. Ni neno ambalo huonesha sifa mojawapo ya nomino/kiwakilishi cha nonimo.” Fasili hii inajitosheleza kwani mara nyingi kazi kubwa ya kivumishi ni kutoa sifa juu ya nonimo au kiwakilishi. Mfano, Mtoto mzuri. Neno mzuri ni kivumishi kinachovumisha nomino mtoto.
Baada ya kuelezea fasili mbalimbali za maneno makuu, maelezo yafuatayo huelezea kwa kina ni jinsi gani kivumishi ni kikumushi.
Katika fasili ya kivumishi na kikumushi, huweza kuleta ufanano fulani kwani kivumishi hutoa maelezo zaidi kuhusu nomino. Pia kwa maana finyu ya kikumushi ni kwamba kinatoa taarifa ya ziada kuhusu nomino. Hivyo basi kivumishi na kikumushi huelezea juu ya nomino. Mfano, Kijana mtanashati, mchezaji mashuhuri. Kwa muktadha huu neno mtanashati na mashuhuri huelezea juu ya nomino, hivyo maneno hayo yote ni vikumushi au vivumishi kwani vivumishi na vikumushi vyote hufanya kazi ya kutoa maelezo ya ziada juu ya nomino. Kutokana na kufanya kazi sawa katika sentensi, tofauti inaweza isiwepo. Mfano, mwanafunzi msafi. Mwanafunzi aliyeugua amepona. Hivyo neno msafi katika sentensi ya kwanza ambayo ni kivumishi na aliyeugua katika sentensi ya pili ambayo ni kikumushi hufanya kazi sawa ya kutoa taarifa juu ya nomino.                                                                                                                   
Hata hivyo ufanano unaoonekana kati ya kivumishi na kikumushi ni pale tu kikumushi kitakapofasiliwa kiufinyu, lakini kikumushi kwa maana pana hudhihirisha tofauti kubwa sana kati ya kivumishi na kikumushi kama inavyooneshwa hapa chini.
Kivumishi huwa ni neno moja lakini kikumushi huwa ni neno moja au zaidi. Mfano; ng’ombe mweusi anakunywa maji. Neno mweusi ni kivumishi ambapo ni neno moja. Mwalimu aliyenipa kalamu ameondoka. Katika sentensi hii neno aliyenipa kalamu ni kikumushi chenye zaidi ya neno moja. Hivyo kivumishi ni neno moja tu lakini kikumushi huweza kuwa neno moja au zaidi, kirai au kishazi.
Kivumishi hutoa taarifa kuhusu nomino au kiwakilishi tu lakini kikumushi hutoa taarifa zaidi juu ya nomino, viwakilishi na aina zingine za maneno. Mfano; kiongozi muadilifu huongoza kwa busara, wewe ni msafi kuliko wote. Maneno muadilifu na msafi hutoa taarifa juu ya nomino na kiwakilishi. Mfano; anayetembea kwa maringo. Neno kwa maringo ni kikumishi kirai kihusishi ambacho hutoa taarifa juu ya kitenzi anayetembea.
Mara nyingi neno kivumishi hutumika kuelezea aina ya maneno hayo katika muktadha wa kimuundo na kileksika lakini kikumushi hutumika kuelezea maneno hayo hayo (ambayo ni kivumishi) na maneno mengine katika muktadha wa kidhima, huangalia kazi ya neno hilo. Mfano; mtoto mpole hulelewa vizuri. Neno mpole katika muktadha wa kimuundo ni kivumishi lakini katika muktadha wa kidhima ni kikumushi kwani hufanya kazi ya kutoa taarifa juu ya nomino mtoto. Mfano mwingine, mwanafunzi mtukutu hafaulu vizuri. Neno mtukutu ni kivumishi kimuundo na kikumushi kidhima.
Kivumishi huweza kuwa katika ngazi ya neno na kirai katika tungo. Mfano; mchezaji mashuhuri. Neno mashuhuri ni aina ya tungo neno ambalo ni kivumishi na ni aina ya tungo kirai ambalo ni kirai kivumishi. Hivyo kivumishi hakiwezi kuvuka ngazi hizo mbili za tungo, lakini kikumushi huweza kuwa katika ngazi ya tungo neno, kirai, kishazi na hata sentensi. Mfano; mwanafunzi anayesoma kwa bidii atafaulu mtihani. Neno mtihani limesimama kama kikumushi cha kitenzi atafaulu kama tungo neno. Kwa bidii ni kikumushi kirai, anayesoma ni kikumushi kishazi.
Utofauti mwingine hujitokeza katika dhana kwamba kila kivumishi ni kikumushi, lakini si kila kikumushi ni kivumishi. Hivyo basi kwa muktadha huu siyo dhahiri kuwa kivumishi ni kikumushi. Mfano; kijana mtukutu anaadhibiwa na mwalimu. Neno mtukutu ni kivumishi na ni kikumushi, lakini neno na mwalimu ni kikumushi na siyo kivumishi, hivyo ni kwa kiasi kidogo sana juu ya ufanano wa kivumishi na kikumushi.
Kwa kuhitimisha, kauli kuwa kivumishi ni kikumishi huthibitika tu endapo fasili ya kivumishi itakuwa katika muktadha wa maana finyu ambapo vyote huelezea juu ya nomino na hufanya kazi ya kutoa taarifa ya ziada juu ya nomino. Lakini kwa upande mwingine wa fasili ya kikumushi katika muktadha wa maana pana, kuna utofauti mkubwa kimuundo na kazi kati ya vikumishi na vivumishi. Hivyo basi kwa kiasi fulani vivumishi ni vikumushi na kwa kiasi fulani vikumushi si vivumishi
     MAREJEO:
Khamisi, A.M na John, G.K. (2002). Uchanganuzi wa Sarufi ya Kiswahili. TUKI. Dar es salaam.
Chou Kikuu cha Oxford (2005). Advanced Learners Dictionary. Oxford University Press. U.S.A.
Matei, A.K. (2008). Darubini ya Sarufi. Phoenix Publishers. Nairobi.
TUKI. (2010). English – Swahili Dictionary. (3rd Edition). MSM L.t.d. Mauritius.

SWALI:
Jadili kwa  mifano dhana ya ujalizaji na ukumushaji.
DONDOO:
UTANGULIZI:
Elementi za kidhima
KIINI:
Dhana ya ujalizaji
Dhana ya ukimushaji
Dhana ya ujalizaji na ukumushaji ni moja ya dhana zinazotumika katika kategoria za kidhima. Hivyo basi elemeti zilizopo katika kategoria ya kidhima ni kama vile, Kiima na Kiarifu, Chagizo, Shamirisho, Yambwa, Yambiwa, Kikumushi na Kijalizo.
Hivyo, dhana ya ujalizaji imetokana na istilahi Kijalizo. Kwa mujibu wa Matei (2008:219) anasema: “Kijalizo ni istilahi ambayo imetokana na kitenzi jaliza ambacho kina maana kamilisha au ongezea habari ili kukamilisha au kutosheleza maana”. Anaendelea kusema kuwa; “hivyo kijalizo ni neno au kirai ambacho hufuata kitenzi kishirikishi na ambalo huelezea zaidi kuhusu kiima au yambwa. Kijalizo huongezea maana au hukamilisha maana ya kipashio kingine katika sentensi.”                                                                                                                                 
Mfano; Lucas ni baharia. Baharia ni kijalizo kwa sababu hukamilisha kiima au maana inayoarifiwa na kitenzi kishirikishi “ni” ambacho kinauwezo wa kujibu swali ambalo linaweza kuwa, Lucas ni nani? Ni baharia. Mfano; Mwalimu amempa…. Katika mfano huu huweza kujiuliza kuwa Mwalimu amempa nani na amempa nini? Hivyo basi, kitenzi hiki kilichoandikwa kwa maandishi ya mlalo kinahitaji kijalizo ili kiweze kukamilisha na kutosheleza maana. Mwalimu amempa John kitabu.
Habwe, J na Karanja, P (2007:164) wao wanasema; “Kijalizo ni neno ambalo hukamilisha kiarifu wakati ambapo kuna kitenzi kisicho cha uarifishaji mkamilifu”   Mfano; Herriet ni mwerevu. Mwerevu hapa ni kijalizo kwani hukamilisha taarifa inayotolewa na kitenzi “ni”
Hamisi na Kiango (2002:14) wanasema, “Kijalizo ni elementi muhimu na ya lazima katika sentensi ambayo kwa mujibu wa sarufi mapokeo inahusika na ukamilishaji wa taarifa muhimu za tendo linalotajwa na kitenzi cha sentensi.” Wanaendelea kusema kuwa, “kwa hali hiyo basi Kijalizo ni elementi ya ujumla ambayo inajumuisha viambajengo kadhaa vya lazima vilivyo ndani ya kiarifu ukiondoa vitenzi.”
Fasili zilizotolewa na wataalamu hawa kuhusu dhana ya kijalizo zote ni nzuri kwani, wote wanakubaliana kwamba, Kijalizo ni kipashio ambacho hukamilisha maaana katika sentensi. Vile vile wametofautiana kidogo, kwa mfano katika fasili ya Matei yeye amesema, Kijalizo hutokea pale ambapo neno au kirai hufuatwa na kitenzi kishirikishi wakati Habwe na Karanja wao wanakubaliana na Kiango na Khamis kuwa, Kijalizo hutokea pale ambapo kitenzi hakitoi taarifa kamili.
Kwa hiyo tunaweza kuhitimisha kwa kusema kuwa, Kijalizo ni kipashio cha kidhima ambacho hutokea katika sentensi pale ambapo hakuna kitenzi cha uarifishaji, yaani kitenzi kinachotoa taarifa iliyokamili. Mfano; Mtoto analilia. Kitenzi “analilia” kinahitaji neno fulani ili taarifa hiyo ikamilike. Hivyo tunaweza kuweka neno “uji” katika kitenzi analilia na sentensi ikawa, Mtoto analilia uji. Hapa neno uji limekalimisha maana ya sentensi.
Hivyo basi, kwa kurejelea maana ya Kijalizo tunaweza kusema kuwa, ujalizaji ni mchakato wa kisarufi wa kuweka vipashio au maneno katika tungo ambayo inakitenzi ambacho hakitoshelezi taarifa ya tungo hiyo, hivyo kinahitaji vipashio vingine ili taarifa hiyo ikamilike. Vipashio hivi huitwa vijalizo.
Mchakato wa ujalizaji huweza kufanywa kwa kutumia aina mbalimbali za vijalizo ambavyo ni vijalizo katika ngazi ya neno, ngazi ya kirai, ngazi ya kishazi na ngazi ya sentensi.
Katika ngazi ya neno: kijalizo huwekwa mbele ya kitenzi ambacho hakikamilishi taarifa. Mfano; Mtoto anacheza mpira. Baba amempiga Dongo. Katika mifano hii nomino mpira na Dongo ni vijalizo, ambapo mpira hukamilisha taarifa ya kitenzi, kwamba mtoto anacheza nini, na Dongo hukamilisha taarifa ya kwamba baba amempiga nani.
Pia Kijalizo huweza kuwa katika ngazi ya Kirai: Kwa mfano; Mwalimu amempa Asha zawadi. Katika sentensi hii Asha zawadi ni kijalizo kirai, kwani hukamilisha taarifa ya mwalimu amempa nani na nini. Mfano mwingine  wa kijalizo kirai ni; Juma ni kiongozi stadi. Hapa kiongozi stadi ni kijlizo kirai ambacho hukamilisha taarifa juu ya Juma ni nani?
Kijalizo katika ngazi ya Kishazi: hapa ni pale ambapo kishazi hutumika kukamilisha taarifa fulani. Mfano; Mtoto mdogo alitaka kucheza mpira. Kucheza mpira ni kijalizo kishazi kinachokamilisha taarifa kuwa mtoto mdogo alitaka kufanya nini. mfano mwingine wa kijalizo kishazi tunaweza kusema, Huyu ndiye niliyekuwa nikikuambia habari zake. Maneno yaliyoandikwa kwa mlalo ndiyo kijalizo kishazi, kwani hukamilisha taarifa juu ya huyu ndiye nani.
Katika ngazi ya sentensi: sentensi hutumika kukamilisha taarifa fulani ambayo haijakamilishwa na kitenzi; mfano, Mwalimu aliagiza wanafunzi wanunue vitabu, Mwalimu amesema tusome na tuandike. Katika mifano hii maneno yaliyoandikwa kwa maandishi ya mlalo ndiyo vijalizo sentensi. Katika mfano wa kwanza hutoa taarifa juu ya mwalimu aliagiza nini, na katika mfano wa pili hutoa taarifa juu ya mwalimu amesema nini.
Hivyo basi, kwa kuzingatia mifano iliyotolewa hapo juu, kijalizo huweza kutokea kama yambwa, au yambiwa, chagizo au shamirisho kulingana na dhima inayofanywa katika tungo.
Baada ya kufafanua dhana ya ujalizaji sasa tuangalie pia dhana ya ukumushaji.
Ukumushaji ni dhana inayotokana na istilahi Kikumushi, ambayo dhana hii imefasiliwa na Khamisi na Kiango (2002:58) kuwa, “Vikumushi ni maneno ambayo sio vivumishi asilia, lakini hufanya kazi kama vivumishi, yaani kazi ya kukumusha (kuongeza sifa au taarifa muhimu) nomino.” Wanaendelea kufafanua, “Vikumushi siyo vipashio vilivyo katika kiwango cha neno tu, bali ni pamoja na makundi ya maneno ambayo yamo katika kiwango cha kirai au kishazi.”
Fasili hii imejikita katika kategoria moja tu ya neno ambayo ni nomino. Hivyo kwa mujibu wao nomino peke yake ndiyo huweza kupokea kikumushi.
Hivyo basi, kwa mtazamo wetu sisi tunaweza kusema kwamba, kikumushi kutokana na kwamba hutoa taarifa juu ya neno, basi huweza kutoa taarifa juu ya kategoria yoyote ya neno na siyo nomino pekee. Hivyo kwa kurejelea fasili hii tunaweza kusema kwamba, dhana ya ukumushaji ni mchakato wa kisarufi ambao unalenga kuongeza taarifa ya ziada kuhusu neno fulani.
Ukumushaji unaweza kujitokeza katika kategoria mbalimbali za maneno kama ifuatavyo;
Ukumushaji huweza kutokea katika Nomino: mfano, Mtoto wa juma ni mtukutu, Kijana Mtanzania amepatikana. Katika mifano hii miwili, maneno yaliyoandikwa kwa maandishi ya mlalo ndiyo vikumushi kwani hutoa taarifa juu ya nomino.
Vilevile ukumushaji huweza kutokea katika Kivumishi: kwa mfano; Nyumba ni nzuri sana, Twiga ni mnyama mrefu zaidi. Katika mifano hii miwili maneno yaliyoandikwa kwa maandishi ya mlalo ni vikumushi vya kivumishi nzuri na mrefu kwani hutoa taarifa juu ya uzuri wa nyumba na urefu wa twiga.
Kitenzi vilevile huweza kupokea ukumushaji: mfano; Juliana anacheza kwa maringo, Kobe anatembea polepole. Katika mifano hii miwili maneno yaliyoandikwa kwa maandishi ya mlalo ni vikumushi vya vitenzi anacheza na anatembea.
Kategoria nyingine ya maneno inayopokea ukumushaji ni Kielezi: kwa mfano; Msichana anakula polepole sana. Kijana anaendesha gari kwa kasi kubwa. Maneno yaliyoandikwa kwa maandishi ya mlalo katika sentensi hizi mbili ni vikumushi vya vielezi ambavyo ni polepole na kwa kasi.
Vilevile vikumushi huweza kutokea katika ngazi mbalimbali, ngazi hizo huweza kuwa nomino, kirai na kishazi: kwa mfano; katika ngazi ya neno kikumushi huonekana kwa umbo la neno moja; mfano, Mama watoto wamerejea. Mbwa mkali amekufa. Maneno yaliyoandikwa kwa maandishi ya mlalo ndiyo vikumushi katika ngazi ya neno.
Katika ngazi ya Kirai huweza kuwa: mfano; Polisi wa kike ni jasiri. Kitabu cha mwalimu ni kizuri. Hivyo maneno haya, cha mwalimu na wa kike ni vikumushi katika ngazi ya virai.
Vilevile kikumushi huweza kuwa ktika ngazi ya kishazi: hapa kishazi hufanya kazi ya ukumushaji. Kwa mfano; Mtoto aliyepata zawadi ameondoka. Nyumba iliyounguka imekarabatiwa. Katika mifano hii miwili maneno yaliyoandikwa kwa maandishi ya mlalo ndiyo vikumushi vya katika ngazi ya vishazi.
Hivyo basi kwa kuhitimisha tunaweza kusema kwamba, dhana ya ukumushaji ni dhana ambayo huonekana kuwa na maana inayofanana na kivumishi. Lakini dhana hizi mbili huweza kutofautishwa kwa kutumia mikabala ya kidhima/kikazi na kimuundo. Katika mkabala wa kidhima tunatumia istilahi kikumushi, lakini katika mkabala wa kiuundo tunatumia istilahi kivumishi. Hivyo basi ni vyema kutofautisha dhana hizi kulingana na mikabala husika.
MAREJEO:
Habwe, J na Peter K (2007). Msingi ya sarufi ya Kiswahili. Phoenix Publishers. Nairobi
Khamis, A.M na John G.K (2002). Uchanganuzi wa sarufi ya Kiswahili. TUKI. Dar es salaam.         
Matei, A.K (2008). Darubini ya Sarufi. Phoenix Publishers. Nairobi.

Swali:
Chunguza mifano ifuatayo kutoka katika lugha ya Pima ya  huko Arizona ya Kati na kisha ujibu maswali yafuatayo:

Na
NENO
MAANA
IDADI
NENO
MAANA
IDADI
i
Gogs
mbwa
umoja
gogos
mbwa
wingi
ii
Uvi
mwanamke

uuvi
wanawake

iii
Jiosh
Mungu

jijiosh
miungu

iv
Kun
mume

kuukun
waume

v
Piigo
shoka

pipgo
mashoka

vi
Toobi
sungura
umoja
totobi
sungura
wingi
(a)    Tenganisha mofimu zinazoonesha wingi katika maneno ya lugha ya Pima uliyopewa.
(b)   Je, unafikiri ni mchakato upi wa kimofolojia uliohusika katika uundaji wa maumbo ya wingi? Kwa nini?             
DONDOO:
UTANGULIZI:
Maana ya mofolojia.
Maana ya mofimu.
Maana ya neno.
Maelezo kwa ufupi kuhusu lugha ya Pima.
KIINI:
Uchanganuzi wa kimofolojia.
Michakato ya kimofolojia iliyotumika katika uundaji wa maumbo ya wingi.
HITIMISHO:
MAREJEO:
Kwa kuanza, tumetoa fasili za Istilahi mbalimbali zilizotumika katika swali. Katika kufasili dhana ya mofolojia, Habwe na Karanja (2004:71) wanadai kuwa mofolojia ni neno linalotumiwa kumaanisha utanzu wa Isimu unaoshughulikia muundo wa maneno. Wanaendelea kueleza kuwa “kimsingi mofolojia hushughulikia muundo wa neno.” Hii hutilia mkazo na kuonesha  kazi kuu ya mofolojia.
Fasili hii haiko mbali sana na ile ya TUKI (2004), ambapo wamefasili mofolojia kuwa ni tawi la Isimu linalojishughulisha na uchambuzi wa kanuni na mifumo inayohusu upangaji wa mofimu mbalimbali ili kuunda maneno yenye maana katika lugha. Fasili zote mbili zinajitosheleza kwani zimegusia mambo ya msingi kama vile, Isimu, muundo na uchambuzi wa maneno katika mofolojia.
Habwe na Karanja (2004), wanafasili neno kuwa ni kipashio cha kiisimu kinachoundwa na mofimu moja au zaidi. Mfano, “Baba” ni neno lililoundwa na mofimu moja, na “Anacheza” pia ni neno linaloundwa na mofimu zaidi ya moja. Kimsingi neno lazima liwe na maana fulani, pia liandikike, lisomeke na hata liweze  kutamkika ili kukidhi haja ya mawasiliano.
Besha, R.M. (1994), hufasili mofimu kuwa ni vipashio vya msingi vinavyounda maneno ya lugha. Anaendelea kueleza kwa kusema kuwa ni vipashio vinavyoonesha uhusiano uliopo kati ya sauti msingi za lugha na maana maalum katika sarufi ya lugha. Hivyo kutokana na mawazo haya tunaweza kufasili mofimu kiupana zaidi kwa kusema kuwa, mofimu ni kipashio kidogo kabisa amilifu cha kisarufi ambacho hakiwezi kugawanyika zaidi bila kupoteza maana. Mfano, neno “analima” linaundwa na mofimu nne ambazo ni A – na – lim – a. Mofimu hizi haziwezi kugawanyika zaidi ya hapo.
Lugha ya Pima ni lugha inayozungumzwa huko Arizona ya kati Marekani katika maeneo ya ardhi iliyoifadhiwa ya mto Gila na mto Salt. Hii ni kwa mujibu wa Riggle, J. (2003), katika makala yake ya “Infixing reduplication in Pima.” Anaendelea kueleza kuwa lugha ya Pima inatabia ya kuruhusu upachikaji wa viambishi katikati ya mizizi ya maneno.
Katika uchanganuzi wa maneno kimofolojia, kuna misingi ambayo hufuatwa. Misingi hiyo ni msingi wa njeo, ambapo kwa kuangalia njeo iliyotumika katika neno husaidia kubaini njia iliyotumika katika kuunda neno hilo. Msingi mwingine ni ule wa uwepo wa neno linaloweza kubadilika na kuwa aina nyingine ya neno. Na msingi wa mwisho ni ule unaofuata maumbo ya umoja na wingi.
Katika msingi wa maumbo ya umoja na wingi, tunaangalia neno lilivyo katika umoja na jinsi linavyokuwa katika wingi, mabadiliko yoyote yatakayojitokeza yatasaidia kubaini jinsi maneno hayo yalivyoundwa na michakato iliyotumika.
Katika data tuliyopewa inayoonesha maneno ya lugha ya Pima katika maumbo ya umoja na wingi na maana yake katika lugha ya kiswahili, tunaona kwamba kuna vipande au mofimu ambazo ndizo zinazoashiria au kuonesha maumbo hayo ya umoja na wingi. Tuchunguze data hizo.
Neno-Pima
Maana/Kiswahili
Idadi
Neno-Pima
Maana/Kiswahili
Idadi
Gogs
Mbwa
Umoja
Gogos
Mbwa
Wingi
Uvi
Mwanamke

Uuvi
Wanawake

Jiosh
Mungu

Jijiosh
Miungu

Kun
Mume

Kuukun
Wanaume

Piigo
Shoka

Pipgo
Mashoka

Toobi
Sungura

Totobi
Sungura

Katika data hii tuliyopewa tunaona kwamba katika maumbo ya wingi kuna vipande au mofimu kadhaa zimeonekana kujitokeza ambazo hazikuwepo katika maumbo ya umoja. Vipande hivyo tutaviona katika jedwali lifuatalo ambalo ndilo litaonesha mchanganuo wa vipande vinavyosababisha kutokea kwa umbo la wingi katika kila neno.

Neno katika wingi
Vipande/mofimu za wingi.
Gogos
Gog – o – s  
Uuvi
U – u – vi / U – u – vi
Jijiosh
Ji – ji – osh / Ji – ji – osh
Kuukun
Kuu – kun / Ku – uku – n
Totobi
To – t – obi
Pipgo
Pi – p – go
Katika maneno haya ya lugha ya Pima mwandishi ametumia michakato mbalimbali ya kimofolojia katika uundaji wa maumbo ya wingi kama ifuatavyo:-
Katika neno Gogos. Gog – o – s, mchakato uliotumika ni uchopekaji. TUKI. (2004), imefalisi neno chopeka kuwa ni kutumbukiza kitu majini au kuloweka. Maana hii ilichukuliwa katika muktadha huu wa kimofolojia ni ile ya kutumbukiza. Hivyo uchopekaji ni njia ya uundaji wa maneno ambapo viambishi huwekwa katikati  ya mzizi wa neno na kuunda neno lingine. Mofomu, -o- katika neno “Gogos” imechopekwa na kuonesha wingi.
Pia njia nyingine iliyotumika katika kuunda mofimu ya wingi katika neno “gog-o-s” ni uambishaji. Kihore, Y.M. na wenzake (2008:75), wakinukuu kutoka katika Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha (KSIL) (1990:3): Uambishaji ni “utaratibu wa kuweka kiambishi kabla, katikati au baada ya mzizi wa neno.” Kwa mujibu huo mofimu -o- imeambishwa katika mzizi wa neno “gogs” na kubadili neno hilo kuwa katika umbo la wingi.
Njia nyingine inayoweza kuwa imetumika katika kuunda maumbo ya wingi katika neno “gogos” ni njia ya uradidi. Wamitila, K.W (2003), anafasili uradidiaji kuwa ni “neno fulani hurudiwa baada ya mengine, yaani kuna maneno mengine katikati ya neno linalorudiwa.”  Hivyo tunaweza kusema uradidi ni urudiaji wa neno au kipande cha neno ambacho tayari kimekwisha tumika katika neno hilo hilo. Katika neno “gog-o-s” mofimu -o- yapili imerudiwa ili kuunda neno lenye umbo la wingi kwani tayari kipande hicho cha neno kilikuwa kimekwisha onekana mwanzoni baada ya herufi ya kwanza ambayo ni ‘g’
Katika neno “Uuvi” endapo mofimu ‘u’ ya kwanza ndiyo inayoonesha wingi, njia itakayokuwa imetumika ni uambishaji, ambapo mofumu “u” imeambishwa mwanzoni mwa mzizi wa neno. Lakini ikiwa mofimu -u- ya pili ndiyo inayoonesha wingi, basi njia itakayokuwa imetumika ni uradidi. Mofimu -u- itakuwa imerudiwa katika sehemu ya pili ili kuonesha wingi.
Pia ikiwa mofimu hiyo -u- ya pili ndio ya wingi,  njia iliyotumika kuunda neno hilo ni uchopekaji, ambapo mofimu -u- imepachikwa katikati ya mzizi wa neno “uvi” na kuunda neno “u-u-vi” katika umbo la wingi.
Katika neno “Jijiosh” iwapo mofimu ya kwanza -ji- ndio huonesha wingi, basi mchakato uliotumika katika kuunda maumbo hayo ya maneno ni uambatishaji/uambishaji ambapo mofimu -ji- imeambatishwa kabla ya mzizi wa neno hilo.
Na ikiwa mofimu -ji- ya pili ndio inayoonesha wingi, michakato itakayo kuwa imetumika ni uchopekaji na uradidi. Ni uchopekaji kwa maana kwamba mofimu -ji- imepachikwa katikati ya mzizi wa neno “jiosh” na kuunda neno lenye umbo la wingi “ji-ji-osh”. Pia ni uradidi kwa maana kwamba mofimu -ji- ya pili imejirudia baada ya mofimu “ji-” ya kwanza na kuunda umbo la wingi.
Neno “Kuukun” huweza kuwa na mofimu “kuu” ya kwanza kama umbo la wingi na endapo ndivyo, basi njia itakayokuwa imetumika kuunda maneno hayo ni uambishaji. Mofimu -kuu- itakuwa imeambishwa mwanzoni mwa mzizi wa neno “kuu-kun” na kuunda umbo la wingi.
Lakini ikiwa mofimu ya umbo la katikati -uku- ndiyo huonesha maumbo ya wingi, basi uundaji huo utakuwa umetumia mchakato wa uchopekaji kwa kuweka viambishi hivyo katikati ya mzizi wa neno hilo na kuonesha wingi.
Katika neno “To-t-obi” mofimu ya wingi ni -t- na michakato iliyotumika kuunda neno hili katika wingi ni uchopekaji ambapo mofimu -t- imechopekwa katikati ya mzizi wa neno “toobi,” pia mchakato wa uambishaji umetumika ambapo mofimu hiyohiyo -t- imeambikwa katikati ya mzizi wa neno na kuunda umbo la wingi.
Njia nyingine inayoweza kuwa imetumika ni uradidi ambapo mofimu -t- ya katikati imejirudia baada ya mofimu ya kwanza T- katika umbo la umoja na wingi.
Kwenye neno “Pi-p-go,” mofimu ya wingi ni -p- ya katikati na mchakato uliotumika kuunda umbo la wingi katika neno hili ni udondoshaji, uchopekaji, uradidi na uambishaji. Samuel, M. (2009:53) amefasili udondoshaji wa irabu kuwa ni “mchakato wa kifonolojia ambapo irabu inadondoshwa wakati ambapo jambo mojawapo kati ya yafuatayo”:- irabu inapofuatiwa na konsonanti ya kweli na irabu zinapofuatana. Kwa kifupi tunaweza kusema kuwa udondoshaji ni kitendo cha kuacha baadhi ya herufi zilizokuwepo katika neno la mwanzo, wakati wa kutamka au kuandika neno hilo.
Katika neno “Pipgo” huonesha wazi kuwa mofimu iliyokuwepo katika umoja ni -i- ambayo imedondoshwa na kujitokeza katika umbo la wingi kama -p- Michakato mingine kama uchopekaji imetumika ambapo mofimu ya wingi -p- ya pili haikuwepo katika umbo la umoja isipokuwa imepachikwa katika umbo la wingi ili kuonesha wingi wa neno.
Uambishaji wa kiambishi cha kati pia umetumika ambapo mofimu -p- imeambikwa katikati ya mzizi wa neno na kuonesha umbo la wingi katika neno “Pipgo”
Uradidi pia umetumika kwani mofimu -p- ya katikati inayoonesha wingi haikuwepo, isipokuwa imejirudia baada ya mofimu za mwanzo za neno “Pi-p-go.”
Kwa kuhitimisha, tumeona kwamba ni vigumu kubaini bayana kuwa ni njia au mchakato upi hasa unaotumiwa kuunda maumbo ya wingi wa maneno hayo ya lugha ya Pima. Ugumu huu unatokana na kwamba maneno hayo yanatumia uundaji wa zaidi ya mchakato mmoja katika neno hilohilo.
MAREJEO:
Besha, R.M. (1994). Utangulizi wa Lugha na Isimu. DUP. Dar es Salaam.
Habwe, J na Peter K (2007). Msingi ya sarufi ya Kiswahili. Phoenix Publishers. Nairobi.
Kihore, Y.M. na wenzake. (2003). Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu. TUKI. Dar es Salaam.
Riggle, J. (2003). “Infixing reduplication in Pima”. Wikipedia.
Samuel, M. (2009). “Kozi Tangulizi ya Fonolojia na Sintaksia ya Kiswahili.”
TUKI. (1981). Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Oxford University Press. Dar es Salaam.
Wamitila, K.W. (2003). Kamusi ya Fasihi: Istilahi na Nadharia. English Press. Nairobi.

SWALI:
Bainisha mofimu katika maumbo yafuatayo: Pendezesha, Chomelea, Usawazisho, Myeyusho, Bahatinasibu, Waogeleaji, Makumbusho, Msongamano, Usawazisho, Waogeleaji, Maombezi.
Neno mofimu ni neno pana ambalo wataalam mbalimbali wamekuwa na mawazo mbalimbali katika kueleza maana yake.Wafuatao ni baadhi tu ya wataalam walioeleza maana ya mofimu.
Massamba na wenzake (1999) uk 36 wanasema kuwa,Mofimu ni kipashio kidogo amilifu katika maumbo ya maneno.Hapa kipashio kina maana ya umbo la neno au umbo katika neno lisiloweza kugawanyika katika sehemu nyingine ndogo zaidi.
Ruth Mfumbwa Besha (1994), anafafanua kuwa Mofimu ni vipashio vinavyoonesha uhusiano uliopo kati ya sauti za msingi za lugha (fonimu) na maana maalum katika sarufi ya lugha.
Pia John Habwe na Peter Karanja (2004),wamemnukuu Hartman (1972) katika kitabu chake kuwa,mofimu ni dhana ya kidhahania iliyomo akilini mwa mtu na sehemu ya umilisi wa mzawa wa lugha husika na anaendelea kusema kuwa hii hudhihirika kiutendaji ama kimaandishi au kimatamshi.
Vilevile Massamba na wenzake katika kitabu chao cha Sarufi Miundo Ya Kiswahili Sanifu wanasema Mofimu ni kipashio kidogo kabisa chenye uamilifu wa maana katika maumbo ya maneno.
Assumpta K.Mtei naye anasema kuwa,Mofimu ni kipashio kidogo kabisa dhahania cha lugha chenye maana.Tunasema kipashio dhahania kwa sababu hakionekani wala haiwasilishwi kupitia uandishi imo akilini mwa msemaji.
Kwa mujibu wa James Salehe Mdee(1988) ametoa aina  mbili za mofimu ambazo ni, Mofimu huru na Mofimu tegemezi ambapo, Mofimu huru ni mofimu inayoweza kusimama peke yake na kuweza kutumiwa katika tungo bila kuwa na kiambishi chochote . Mofimu huru zina hadhi ya neno na zinaweza kuwa aina yoyote ya neno kama vile nomino,kitenzi ama kiwakilishi.
Licha ya wataalamu mbalimabili tulio waangalia katika kutoa maana ya mofimu, sisi wanazuoni wachanga tumeona kuwa”Mofimu ni kipashio kidogo cha lugha chenye maana kisarufi na kileksika” mfano kitenzi “anacheza” kinaweza kubainishwa na kuleta maana kisarufi yaani;
 A-        ni kiambishi awali nafsi ya pili umoja
-na-      ni kiambishi cha njeo cha wakati uliopo
-chez-   ni mzizi wa kitenzi
              -a-       kiambishi tamati maana
Kwa upande mwingine mofimu inaweza kuwa na maana ya kileksika mfano, maneno kama baba,mama,shangazi na mengineyo yanatupa maana moja kwa moja kikamusi, kiundani maneno hayo ndiyo tunayoweza kuyaita mofinu huru ambazo zikisimama peke yeke zinaleta maana na haziwezi kugawika zaidi.
Maumbo mbalimbili ya mofimu katika lugha ya Kiswahili na hata lugha nyingine huwa na maana na pia uhusiano wa vipashio ili kujenga maana sahihi iliyo kusudiwa katika maneno husika. Maumbo na uhusiano huo usipozingatiwa huweza hata kuathiri maana ya neno. Kwa hiyo uhusiano na mpangilio wa maumbo ya vipashio katika lugha ya Kiswahili ndio unaoweza kuleta maana zilizokusudiwa katika maneno.
Maumbo yafuatayo ya Kiswahili yamebainishwa mofimu zake na kuelezea uhusiono wa vipashio vinavyohusika.
(a) Pendezesha
 -Pend-   mzizi wa neno
 -ez-        kiambishi cha usababishi
 -esh-      kiambishi cha utendeshi
  -a-         kiambishi tamati maana
(b) Chomelea
-chom - mzizi wa neno
-e-    kiambishi nyambulishi cha utendea
-le-   kiambishi kinachoonyesha ukubwa wa tendo (linafanywa mara nyingi)
-a-    kiambishi tamati
(c) Usawazisho
-u-           kiambishi awali kinominishi
-sawa-     mzizi wa neno
-z-            kiambishi cha usababisho
-ish-         kiambishi cha usababisho
-o-            kiambishi tamati kinominishi
(d) Myeyusho
-m-     kiambishi awali kinominishi
-yeyu-  mzizi wa neno
-sh-       kiambishi cha usababishi
-o-         kiambishi tamati kinominishi
(e) Bahati nasibu
Hii ni mofimu huru ambayo imeundwa na mofimu mbili zenye maana tofauti ambapo zikiwekwa pamoja tunapata maana sahii iliyopo kwenye umbo letu(neno).
Kutofuata mpangilio na uhusiano wa mofimu hizo hautaleta maana iliyokusuduwa katika umbo hilo, mfano neno hilo likigeuzwa na kuwa nasibubahati hatutapata maana iliyokusudiwa. Kutokana na umbo hilo kila mofimu ikisimama peke yake yaani nasibu na bahati tunaweza kupata maana hivyo neno Bahati nasibu ni neno huru ambalo haliwezi kugawanyika.
(f) Waogeleaji
-wa-   kiambishi awali cha ngeli ya kwanza uwingi
-og-   ni mzizi wa neno
-e-     kiambishi cha utendea
-le-    kiambishi kinachoonyesha kiwango cha ukubwa wa tendo
-a-     kiambishi tamati kijenzi
-ji-    kiambishi tamati kinacho onyesha ujirudiajirudiaji wa tendo

(g) Makumbusho
-ma-        kiambishi kinominishi cha mahali
-kumbu- mzizi wa neno
-sh-         kiambishi kitendeshi au kisababishi
-o-           kiambishi tamati kinominishi.
(h) Msongamano
-m-       kiambishi awali kinominishi
-song-  mzizi wa neno
-am-     kiambishi cha uambatani (kiambishi tamati cha mwambatano)
-an-      kiambishi cha utendano
-o-        kiambishi kinominishi.
(i) Maombezi
-ma-    kiambishi awali cha ngeli ya wingi
-omb-  mzizi wa neno
-ez-      kimbishi tamati kitendeshi (-e- kiambishi cha utendea)
-i-         kiambishi tamati kinominishi (-zi- kiambishi kinominishi)
Kwa kuhitimishi ni kwamba kutokana na ubainishaji huo wa mofimu na uhusiano wake ni dhahiri kuwa uhusiano wa vipashio hutegemea mpangilio wa vipashio hivyo, yaani nafasi ya mofimu katika neno. Na kila mofimu ina kazi yake kutegemea mpangilio uliopo katika neno hilo.

MAREJEO
Besha,R.M (1994), Utangulizi wa Lugha na Isimu. Dar es salaam.DUP ltd.
Habwe,J na P.Karanje (2004), Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi. Printpak ltd
Kihore,Y.M na wenzake (2001), Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu. Dar es salaam. TUKI.
Matei,A.K (2008), Darubini ya Sarufi. Nairobi.Acme Press.
Massamba D.P.B na wenzake (1999), Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu. Dar es salaam.TUKI.
Mdee, J.S (1988), Sarufi ya Kiswahili. Dar es salaam. DUP ltd.

SWALI:
Je kuna tofauti yoyote kati ya nyanja za isimu na matawi ya isimu katika Kiswahili? Fafanua jibu lako kwa mifano isiyopungua mitano kwa kila upande.
·         Maana ya Isimu
·         Nyanja za Isimu
·         Matawi ya Isimu
·         Mzizi/Kiini cha swali: Tofauti za nyanja za isimu na matawi ya Isimu.
Kwa mujibu wa Mgullu, R. (2010) kama alivyomnukuu Richard na wenzake (1985) anasema kuwa isimu ni mtalaa ambao huchunguza lugha kama mfumo wa mawasiliano ya wanadamu.
Habwe, J na P. Karanja, wanasema kuwa lugha isimu ni taaluma inayochunguza lugha ya mwanadamu kisayansi.
TUKI (1990) wanasema isimu ni sayansi ya lugha.
Msanjila na wenzake (2011) wanasema kuwa isimu ni taaluma ya sayansi ya lugha inayoshughulika na nadharia, uchunguzi na uchambuzi wa vipengele mbalimbali vya lugha.
Kwa ujumla, tunaweza kufasili isimu kuwa ni taaluma ya kuchunguza lugha ya binadamu kisayansi, usayansi wa uchunguzi huu unajitokeza kwa sababu hufuata sifa za kisayansi ambazo ni utoshelevu wa kiuteuzi, utoshelevu wa kiuchunguzi, kiufafanuzi, uchechefu na uwazi.
TUKI (2004) Kamusi Sanifu ya Kiswahili, inasema kwamba Nyanja ni wingi wa uwanja, ambapo uwanja ni maeneo ya fani za kitaaluma. Hivyo tunaweza kusema Nyanja za isimu ni taratibu zinazomwezesha mtu kujua lugha au ni taarifa ya lugha. mfano; fonolojia, mofolojia, sintaksia
Besha, R. (2004) anasema matawi ni tanzu za kiisimu zinazotumika katika kufafanua lugha, mfano; Isimu fafanuzi, Isimu jamii, Isimu Linganishi, Isimu Nadharia, Isimu Historia, Isimu Kompyuta, Isimu Nurolojia, Isimu Nafsia, Isimu Hisabati na Isimu tumizi.
Hivyo matawi ya Isimu ni mikabala inayochanganua sayansi ya lugha. Zipo tofauti mbalimbali baina ya Nyanja za Isimu na Matawi ya Isimu. Tofauti hizo ni kama ifuatavyo;
Maana: maana za Nyanja na Matawi ya Isimu zinatofautiana. Kwani Nyanja za Isimu ni fani za kitaalima au uwanja unaomwezesha mtu kujua lugha au maarifa ya lugha. Mfano; fonolojia, mofolojia, sintaksia, na pragmatiki. Wakati Matawi ya Isimu ni kama tanzu za tanzu za Isimu zinazotumika katika kufafanua lugha. Kwa mfano; Isimu fafanuzi, Isimu Jamii, Nafsia, Hisabati, Kompyuta na Nurolojia nk.
Idadi: idadi ya Nyanja za Isimu ni chache na zijulikana kwani zipo tanu “5” ambazo ni fonolojia, mofolojia, sintaksia, semantiki na pragmatiki. Wakati matawi ya Isimu ni mengi, hayana idadi maalum. Mfano; Isimu jamii, Isimu Nadharia, Kompyuta, Historia, Isimu Falsafa, nk. Hutegemea ubunifu, udadisi katika uainisho wa wanaisimu.
Malengo: malengo ya Nyanja za Isimu ni kumwezesha mtumiaji wa lugha fulani kujua kanuni na taratibu za utumiaji wa lugha husika. Mfano; maumbo, miundo, matamshi, na maana, wakati Matawi ya Isimu yanalengo la kuchunguza, kuchambua na kufafanua lugha kulingana na tawi husika;- mfano Isimu jamii huchunguza uhusiano uliopo kati ya lugha na jamii husika. Isimu nafsia huelezea jinsi binadamu anavyojifunza lugha. Isimu kiafrika imejikita katika kuchunguza lugha mbalimbali zinazozungumzwa barani Afrika.
Utegemezi: hatuwezi kujifunza matawi ya Isimu bila kuwa na ujuzi wa Nyanja za Isimu Ila tunaweza kujifunza Nyanja za Isimu bila kuwa na ujuzi wa Matawi ya Isimu. Wakati matawi ya Isimu hutegemea Nyanja za Isimu ili kuweza kufafanua lugha mfano Isimu fafanuzi inategemea uwepo wa Nyanja za Isimu; kama vile fonolojia, mofolojia, sintaksia, semantiki na pragmatiki ili uweze kufafanua lugha husika katika vipengele hivyo.
Ujifunzaji Umilisi au Umahiri: Nyanja za Isimu kujifunza kwake hutegemea kawaida za jamii juu ya kanuni na taratibu za utumizi wa lugha husika. Mfano; kiswahili: Msichana   mzuri.
                       N          V                                                                                      kiingereza: Beautiful   girls 
                                                   P           N       
Hivyo tunaona katika Kiswahili nomino huweza kutangulia kivumishi, ni kawaida za jamii ya waswahili na taratibu zao zinazoitofautisha na jamii vyingine kama zile za kizungu zinazoweza kuruhusu kivumishi kiwe kabla ya nomino. Wakati matawi ya Isimu ujifunzaji, umilisi na hatimaye umahiri watasnia ya matawi mbalimbali ya Isimu hutegemea udadisi na ubunifu binafsi wa mhusika/mchunguzi. Mara nyingine huwa hakuna uhusiano wa moja kwa moja kwa baadhi ya matawi baina ya jamii na tawi husika ambalo mdadisi hudadisi. Mfano; Isimu Kompyuta na Kiswahili.
Mpangilio wa kingazi: Nyanja za Isimu ziko katika mpangilio wa kingazi yaani kuanzia fonolojia mpaka pragmatiki na zote hutegemeana, huhusiana na hukamilishana kuanzia ngazi ya chini kabisa mpaka ngazi ya juu kabisa.
Hivyo tunaona kwamba fonolojia, mofolojia, sintaksia, semantiki na pragmatiki ni taaluma zinazotawala msingi wa lugha mahususi na hizi ndizo Nyanja za Isimu. Nyanja za Isimu na Matawi ya Isimu vinauhusiano ambao unatimiliza kukamilishana baina yake. Kwa mfano;
Mofolojia inahusiana na Isimu changanuzi kwani zote huchunguza maumbo ya maneno. a-na-pig-a. Sintaksia inahusiana na Isimu fafanuzi kwani zote huangalia muundo wa sentensi katika lugha. Semantiki na Pragmatiki zinauhusiano na Isimu jamii kwani zote huangalia jinsi lugha inavyotumika, nani amesema, kwa nini, wakati gani, juu ya nini. Maswali haya yote hushughulikiwa na Semantiki, Pragmatiki na Isimu jamii.    
         
SWALI:
Mitindo ni nini? Inasaidiaje katika kufanikisha au kutofanikisha
          Mawasiliano.
DONDOO
Utangulizi.
            -Maana ya mtindo.
            -Maana ya mitindo ya lugha.
            -Fasili ya mitindo mbalimbali ya lugha.
Kiini.
            - Mitindo ya lugha inavyofanikisha au kutofanikisha mawasiliano.
Hitimisho.
Marejeo.
Katika kujadili swali hili tutaanza kwa kufasili dhana ya mtindo, mtindo wa lugha na mitindo mbalimbali ya lugha kama vile jagono, lahaja, misimu, agoti na rejesta kutokana na wataaalamu mbalimbali. Pia tutatalii kwa kina juu ya jinsi au namna au miundo hiyo ya lugha inavyofanikisha au kutofanikisha mawasiliano na mwisho ni hitimisho.
Kwa mujibu wa TUKI (2004) wanafasili mtindo kuwa ni jinsi ya kufanya kitu kwa kufuata taratibu fulani.
King’ei K (2010) wakimnukuu Davy Crystal (1969) anafasili mtindo wa lugha kuwa ni njia au tabia matumizi ya lugha fulani kwa kipindi maalumu katika historia.
Hivyo basi tunaweza kufasili mtindo  kuwa ni uwasilishaji wa kitu fulani kwa namna tofauti tofauti hivyo katika lugha mada moja inaweza kuwasilishwa kwa namna tofauti tofauti. Baadhi ya mitindo ya lugha ni jagoni, agoti. Misimu. Lahaja na rejesta.
Wataalamu mbalimbali wamefasili mitindo mbalimbali ya lugha kama ifuatavyo.
King’ei K(2010) anafasili jagoni kuwa ni lugha ya kitaaluma au isiyoeleweka kwa watu wa kawaida.kila mojawapo ya taaluma hii hutumia msamiati maalumu usioeleweka na wale ambao sio wanataaluma husika, taaluma hizo ni kama vile matibabu, dini, sheria, sayansi, teknolojia, uchumi, siasa, isimu au fasihi.
Pia king’ei (2010) anafasili misimu au simo kuwa ni matumizi ya lugha ambayo hudhihilisha kiwango cha juu cha ubunifu na mara kwa mara ucheshi. Pia misimu huvunja kanuni za lugha sanifu.
Kwa mujibu wa Msanjila na wenzake(2010) wanafasili misimu kuwa ni aina ya misemo katika lugha ambayo huzuka na kutoweka, sifa kuu ya misimu ni kwamba hudumu kwa  muda mfupi tu na siyo lugha sanifu.
Hali kadhalika halliday anafasili rejesta kuwa ni mtindo wa lugha kulingana na kazi au shughuli.
Hivyo basi rejesta ni mtindo wa lugha kutegemeana na kazi fulani,muktadha  wa matumizi, lengo na uhusiano wa mawasiliano.
Hali kadhalika oxford, advanced learner’s dictionary wanafasili lahaja kuwa ni aina ya lugha ambayo huzungumzwa katika eneo moja ambayo hutofautiana kisarufi, msamiati na matamshi na lugha kuu.
Pia king’ei (2010) anafafanua lahaja kuwa ni tofauti za kimatamshi yanayodhihilika miongoni mwa wanajamiilugha wanaoishi katika maeneo mbalimbali ya kijiografia.
Vilevile  Mkude D.J (2010) anafasili lahaja kuwa  ni usemaji unaoangukia katikati ya mtu binafsi na usemaji wa jamii ya wasema lugha moja.
Baada ya kuona fasili mbalimbali kutokana na wataalamu  sasa tuone namna au jinsi mitindo hii ya lugha inavyoweza kufanikisha au kutofanikisha mawasiliano.
Tukianza na jinsi mitindo hii inavyoweza kufanikisha mawasiliano kama ifuatavyo.
Misimu kama moja ya mitindo ya lugha hutumika kufupisha mawasiliano miongoni mwa wazungumzaji. Baadhi ya misimu hutumika kupunguza idadi ya maneno hivyo kufanya mazungumzo yawe mafupi na yanayoeleweka kwa urahisi mfano neno “daladala” kwa dar es salaam linaweza kueleweka kwa urahisi zaidi kuliko kusema magari madogo yanayotumika kuchukua abilia chini ya 50 kutokea eneo moja hadi jingine kwa nauli ya shilingi 300.
Hali kadhalika mitindo mbalimbali ya lugha kama vile misimu na agoti husaidia kuficha jambo la kundi fulani lisieleweke kwa wengine mfano rejesta za mitaani ambazo zimesheheni misamiati mingi ambayo hutambulika na kundi hilo tu la watu. Mfano wa maneno yanayotumika ni kama yafuatayo
Maneno ya mitaani      maana katika lugha sanifu
Demu                          -           msichana
Mkwanja                     -           pesa
Kama kawa                 -           kama kawaida
Pia mitindo ya lugha hususani lahaja hutumika kusanifisha lugha ili kurahisisha mawasiliano miongoni mwa jamii husika. Lahaja ya  kiunguja iliteuliwa miongoni mwa lahaja nyingi  ili itumike katika mawasiliano  uteuzi huu ulitetewa na kuongozwa na Steere, walidai kwamba kiunguja kilikuwa bora zaidi na kilishakuwa na maandishi mengi zaidi kuliko kimvita (Msanjila na wenzake 2010:82). Hivyo kusanifishwa kwa lahaja hii kuliweza kufanikisha mawasiliano kwa urahisi kwani watu waliweza kutumia lugha kwa namna moja.
Pia baadhi ya mitindo ya lugha kama vile misimu husaidia kwa kiasi kikubwa katika kukuza lugha kwani maneno ambayo hapo awali yalikuwa ni misimu na sasa yamesanifiwa na kuwa maneno ya lugha sanifu. Msanjila na wenzake(2010:20) wanaainisha baadhi ya maneno ambayo yalikuwa misimu na hivi sasa ni sanifu maneno hayo ni kama yafuatayo,
Daladala - Basi la mtu binafsi linalotumika kusafirisha abiria mjini,
       linatumika zaidi Tanzania, jina lililotokana na nauli yake hapo
                 mwanzo kuwa sawa na thamani ya dola moja ya marekani.
Matatu -    Basi dogo linalobeba abilia mjini, linatumika zaidi Kenya, jina
                 lililotokana pia na nauli iliyokuwa inatozwa wakati huo.
Kasheshe - Hali ya kutoelewana inayotokana na watu kutokubaliana
                   jambo fulani.
Hivyo basi maneno hayo yote yanatumika katika jamii na huweza kufanikisha mawasiliano miongoni mwao.
Vilevile baadhi ya mitindo ya lugha kama vile misimu na lahaja husaidia kuwaunganisha watu mbalimbali wanapowasiliana. Watu mbalimbali hutumia mitindo mbalimbali ya lugha kama vile misimu,rejesta na jagoni bila kujali tofauti zao, mfano maneno kama vile
Ondoa mchuma - Kuwasha gari na kuiruhusu iondoke au kuanza safari
Msaada kwenye tuta   - Ninaomba kushuka kwenye tuta.
Nipe wali kuku - Nipatiwe wali na nyama ya kuku.
Maneno haya hutumika na watu katika usafiri na mengine hoterini na watu tofautitofauti bila kujali tofauti zao hivyo kufanikisha mawasiliano miongoni mwao.
Pia mitindo ya lugha huokoa muda miongoni mwa wazungumzaji katika mawasiliano. Baadhi ya mitindo ya lugha huokoa muda  kwani hutumia misamiati ambayo kimsingi hufanya maongezi yawe mafupi na yanayoeleweka mfano matumizi ya rejesta, rejea mfano ufuatao.
Muuzaji: wapi wali kuku?
Mteja: hapa
          Muuzaji: wapi chai mbili?
          Mteja: lete ugali mbuzi.
Hali kadhalika mitindo ya lugha husaidia katika kupamba lugha hasa katika mazungumzo. Wazungumzaji wengi wanapozungumza hapa na pale hupenda kutumia maneno tofautitofauti kama vile misimu ili kufanya mazungumzo yawe ya kuvutia. Pia baadhi ya watu wanaona kuwa matumizi ya mitindo ya lugha ndio ujuzi wa lugha hivyo hupenda sana kutumia mitindo hii ya lugha ili kuweza kurahisisha mawasiliano.
Pia baadhi ya mitindo ya lugha husaidia kuokoa muda wakati wa mawasiliano. Mitindo ya lugha huweza kufanya mazungumzo kuwa mafupi hivyo kuokoa muda wa kuzungumza, mfano mtindo wa lugha unaotumiwa hospitali baina ya muuguzi na mgonjwa au hotelini baina ya muuzaji na mteja ambao hutumia muda mfupi katika mazungumzo ili kuweza kuhudumia wateja wengi zaidi.
Pia mitindo ya lugha huweza kutumika kama kitambulisho cha jamii au watu husika mfano lugha inayatumiwa na watu wa taaluma fulani huweza kukujulisha kuwa hawa ni watu wa taaluma fulani kama vile wanasheria,madaktari au wanasiasa.
Licha ya mitindo ya lugha kufanikisha mawasiliano lakini kwa upande mwingine inaweza kukwamisha au kutofanikisha mawasiliano. Hali hii huweza kutokea kama ifuatavyo.
Mitindo ya lugha hupunguza hadhira. Kutokana na maneno ambayo si sanifu na kimsingi hufahamika na kundi hilo maalumu, wakati mwingine hupunguza hadhira kama mtu siyo wa kundi hilo husika ni ngumu kuwaelewa wanaozungumza wanazungumza nini na wana maana gani hivyo hukwamisha mawasiliano  miongoni mwao.
Hali kadhalika mitindo ya lugha huharibu lugha kwani si sanifu, kwa maneno ambayo si sanifu kama vile misimu matumizi ya agoti na rejesta husababisha kuibua maneno au msamiati tofauti miongoni mwa wazungumzaji wanaozungumza lugha moja. Baadhi ya maneno ambayo si sanifu ni kama vile maneno ya mitaani yenye maneno kama vile
Nipotezee -  Achana na mimi
Nipe buku -  Nipe shilingi elfu moja
Usinibanie - Usininyime
Vunga -       Nyamaza
Mtindo wa lugha huchochea uhalifu mfano agoti. Kwa matumizi ya agoti miongoni mwa wahalifu husababisha uhalifu kwani huweza kuwasiliana kwa kutumia lugha yao na ambayo inaweza kufahamika kwa kundi hilo tu ambayo kwa namna moja au nyingine huweza kuathiri jamii.
Hali kadhalika matumizi ya mitindo ya lugha kama vile misimu huleta msamiati wa matusi katika mawasiliano. Watumiaji wa misimu huibua misamiati wa matusi ambao hutumika katika mawasiliano baina yao hivyo huharibu lugha, baadhi ya misamiati hiyo ni kama  vile.
Kula mavitu    - kufanya mapenzi
Goma  - mwanamke
Kitunguu - makalio
Maziwa - manii
Mashine - uume
Kwa kuhitimisha tunaweza kusema kuwa jamii katika mawasiliano tofauti tofauti lazima kuzingatia mambo makuu kadhaa katika kukidhi haja ya mawasiliano ambayo ni kuzingatia unaongea nini, unaongea na nani, na unaongea wapi.

MAREJEO.
Halliday M.A.K (1989)Spoken and written language.UK. Oxford university press.
King’ei K (2010) Misingi ya isimujamii.. Dar es salaam. TUKI
Msanjili na wenzake (2010) Isimujamii: Sekondari na vyuo. Dar es salaam. TUKI
Oxford (2010) Advanced learner’s dictionary.UK. . Oxford university press
Mkude  D.J (2010) Mtawanyiko wa lahaja za Kiswahili: katika Makala za semina ya kimataifa ya waandishi wa Kiswahili. Dar es salaam. TUKI


SWALI: 
Je kuna tofauti yoyote kati ya nyanja za isimu na matawi ya isimu katika Kiswahili? Fafanua jibu lako kwa mifano isiyopungua mitano kwa kila upande.
Katika kueleza dhana nzima ya swali, tutatoa fasili ya isimu kwa mujibu wa wataalamu  mbalimbali. Tutatoa utofauti uliopo baina ya nyanja za isimu na matawi ya isimu na uhusiano  uliopo baina ya nyanja za isimu na matawi ya isimu kisha kumalizia na hitimisho  kuhusiana na swali kama linavyojieleza. Kwa kuanza na maana ya isimu kwa mujibu wa wataalamu.
Kwa mujibu wa Habwe na Karanja (2007) wanasema swala isimu ni nini?, limejadiliwa na wataalamu wengi wa lugha kwa  njia  tofauti. Hata hivyo wote wanakubaliana kuwa isimu ni taaluma inayochunguza lugha ya mwanadamu kisayansi. Lakini wataalamu wanajiuliza swali sayansi ni nini? kwani tumeshazoea sayansi ni kama vile kemia, fizikia au bayolojia kuitwa sayansi. Maana ya kusema    isimu ni sayansi  matumizi ya alama kama vile;
              S    KN + KT      au       KN      N + (KV)
Alama hizi huifanya isimu ionekane kuwa ni sayansi kama vile kemia, fizikia na  bayolojia.
Vermal na wenzake (1989;26) wanasema kuwa isimu ni sayansi tu kama vile kemia, fizikia au bayolojia kwa sababu hufuata mbinu za kimsingi za utafiti wa kisayansi. Mbinu hizi huhusisha sifa zifuatazo kama vile uchunguzi uliothibitiwa, uundaji wa haipothesia, uchunguzi , ujumlishi, utabiri, majaribio na uthibitishaji, urekebishaji  au ukataaji wa haipothesia kama walivyonukuliwa na Habwe na Karanja (2007). Hivyo kutokana na fasili hii ya Vermal na wenzake (1989:26) tunaweza kusema kuwa isimu haichunguzi lugha kiholela bali kwa utaratibu na mwelekeo maalumu.
 Hivyo kutokana na fasili hizo na mawazo haya ya wataalam kutoa fasili ya isimu hiyo basi isimu tunaweza kufasili kama ni taaluma ya sayansi ya lugha inayoshughulika na nadharia, uchunguzi na uchambuzi wa vipengele mbalimbali vya lugha kwa kutumia mbinu za kisayansi.
Baada ya kuangalia fasili ya isimu ilivyofasiliwa na wataalamu mbali mbali, zifuatazo ni tofauti zilizopo baina ya nyanja  za isimu na matawi ya isimu.
Maana, vipengele vya isimu vinavyoshughulikia maarifa ya lugha mfano fonolojia inashughulikia jinsi sauti zinavyopangiliwa katika kuunda kipashio kikubwa zaidi mfano sauti /l/, /i/, /m/, /a/ zikiunganishwa unapata kipashio kikubwa ambacho ni lima cha kimofoloji. Wakati matawi yanayohusu uchanganuzi wa  taarifa mbalimbali za isimu mfano isimu historia inachanganua mabasiliko mbalimbali yanayotokea katika lugha fulani viwango vyote mofoloji, fonolojia, sintaksia na semantiki.       
Idadi, kwa mujibu wa Habwe na Karanja (2007) wamejaribu kuainisha  nyanja kuu nne za isimu ambazo ni fonolojia, mofolojia, sintaksia na semantiki. Lakini kwa upande wa Mgullu (1999) ameainisha nyanja kuu mbili za isimu ambazo amezishughulikia katika kufanya uchambuzi,  nyanja hizo ni  fonolojia, na mofolojia. Kwa ujumla nyanja za isimu zipo nne ambazo ni fonolojia, mofolojia, sintaksia na semantiki. Kwa upande wa matawi ya isimu  Mgullu (1999) amebainisha matawi tisa ambayo ni isimu historia, isimu linganishi, isimu jamii, isimu fafanuzi, isimu tumizi, isimu tiba,isimu nafsia, isimu afrika na isimu falsafa. Besha (2007) amejadili baadhi ya matawi ambayo ni isimu saikolojia, isimu fafanuzi, isimu jamii na isimu historia. Vilevile  matawi  mengine ni kama vile isimu hisabati na isimu kompyuta. Kwa hiyo idadi ya matawi ya isimu yaliyojadiliwa kwa kiasi kikubwa na wataalam ni kumi na mbili ambayo ni isimu historia, isimu jamii, isimu linganishi, isimu fafanuzi, isimu tiba, isimu nafsia, isimu afrika, isimu falsafa, isimu saikolojia, isimu kompyuta na isimu hisabati.
Upangilifu, katika nyanja za isimu huwa kuna mpangilio maalumu wa kingazi kuanzia kiwango cha chini au cha juu mfano fonolojia, hufuatwa na mofolojia, sintaksia na  semantiki  licha ya kuwa maana huweza kupatikana katika viwango vyote yaani katika fonolojia, mofolojia na sintaksia. Mfano sauti /b/, /a/, /b/, /a/ unapata neno baba katika kiwango cha mofolojia baba + anacheza + mpira tunapata sentensi ambayo ni baba anacheza mpira katika kiwango cha sintaksia wakati matawi ya isimu hayana mpangilio maalumu wa kingazi.
Kiwango cha ufafanuzi na uchunguzi, Nyanja za isimu huangalia uwanja maalumu mahususi mfano fonolojia hushughulikia  sauti za lugha mahususi, , mofolojia hushughulikia na maumbo ya maneno na sintaksia hushughulikia  miundo ya sentensi na semantiki hushughulikia  maana katika lugha. Kwa maana hii ni kwamba nyanja za isimu zinajitosheleza katika ufafanuzi wa dhana katika  uwanja husika. Wakati  matawi ya isimu huhusisha  nyanja zote za isimu  katika ufafanuzi wake. Mfano isimu  historia huchunguza mabadiliko yanayotokea katika viwango mbalimbali vya  lugha fulani katika vipengele mbalimbali vya historia ya lugha hiyo. Ili  kuweza kujifafanua zaidi kwa ukamilifu itachunguza mabadiliko ya kifonolojia, kimofolojia,  kisintaksia na kisemantiki au isimu linganishi  inayofanya  ulinganisho na  utofauti wa lugha mbali mbali katika vipengele vya fonolojia, mofolojia, sintaksia na semantikia  hii ni kwa mujibu wa Mgullu (1999).
Ukongwe, nyanja za isimu ni kongwe, hii inajidhihirisha kwenye historia kwa  mfano fonolojia ambayo ilianzishwa miaka ya 520-460 kabla ya kristo huko India ya kati na Panin (baba wa isimu) alianzisha dhana mbalimbali kama vile fonimu na dhana zingine za mofolojia kama mofimu na mzizi. Taaluma ya fonimu ilipotea na kuibuliwa na wataalam wengine karne ya 19 kama vile Kruszewski (1873) De Courtenary (1876) na Trubetzkoy (1876) kama walivyonukuliwa na Massamba (2010) wakati matawi ya isimu yalianza miaka ya 1950 hadi 1960  na kuendelea  na ambapo tafiti nyingi  zilifanywa na wanaisimu, wanasosiolojia na  wanaathropolojia  mfano Hymes (1972) mwanaathropolojia aliyehariri  kitabu cha “Direction of  social linguistics”  na wengine kama Fishman (1971), mwanasosiolojia, na wanaisimu kama Gumperz (1972), Labov (1972) na  Bright (1965) kama  walivyonukuliwa na Msanjila na wenzake (2011). Matawi  mengine kama vile isimu linganishi iliyofanyiwa utafiti na Lehman (1973), isimu falsafa na TUKI (1990) na isimu nafsia  na Whorf(1953) walivyonukuliwa na Mgullu (1999)
Mawanda, nyanja za isimu huwa na mawanda finyu sana , kwani kila uwanja huwa unashughulikiwa kipekee mfano fonolojia hujishughulisha na sauti, mofolojia ni maumbo ya maneno, sintaksia yenyewe ni muundo wa maneno katika sentensi na semantiki hujishughulisha na maana. Wakati matawi ya isimu yanamawanda mapana, katika uchunguzi, hushughulikia nyanja zote mfano, Isimu historia huchunguza zaidi mabadiliko katika katika viwango mbalimbali vya lugha fulani katika vipindi mbalimbali  na mabadiliko haya hudhihirika  katika viwango vya fonolojia , mofolojia, sintaksia, na semantiki, hii ni kwa mujibu wa Mgullu(1999)
Licha ya nyanja za isimu na matawi ya isimu kutofautiana, lakini pia kwa upande mwingine  zinahusiana. Kwani katika uchunguzi , uchambuzi, uchanganuzi na ufafanuzi wa matawi ya isimu hutegemea nyanja za isimu. Mfano isimu historia ambayo inachunguza mabadiliko katika vipindi mbalimbali katika viwango vya fonolojia, mofolojia, sintaksia na semantiki na  isimu fafanuzi ambayo inafanya ufafanuzi wa lugha fulani kutegemea vipengele vya lugha husika ambavyo ni mofolojia, fonolojia, sintaksia na semantiki, hii ni kwa mujibu wa Mgullu(1999). Maelezo haya ni dhahiri kuwa  uchambuzi wa matawi ya isimu lazima utegemee nyanja za isimu
Hivyo basi nyanja za isimu na matawi ya isimu kama taaluma za isimu zinaweza kufanana katika lengo kuu la isimu ambalo ni kuchunguza, kuchambua, kuchanganua na kufafanua lugha. Taaluma hizi za isimu zinawawezesha wanaisimu kufanya utafiti wa lugha kiundani zaidi na kutoa hoja zenye mantiki na mashiko zaidi za kuthibitisha kuwa isimu ni sayansi.

MAREJEO.
Besha, R.M (2007) Utangulizi wa  Lugha na Isimu. Dar es Salaam University  Press. Dar es Salaam

Habwe, J na Karanja, P (2007) Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Phoenix Publishers. Ltd. Nairobi.
Massamba, D.P.B (2010). Phonological Theory: History and Development. IKS Dar es salaam.

Mgullu R.S (1999) Mtalaa wa Isimu: Fonetiki, Fonolojia na Mofolojia.Longhorn Publisher Ltd.Nairobi.
Msanjila na wenzake. (2011). Isimujamii: Sekondari na Vyuo. TUKI. Dar es salaam.

SWALI:
Kwa kutumia mifano ya kutosha eleza jinsi fonimu inavyoweza kuvuka mpaka wa fonimu na kuingia katika fonimu nyingine.
Dhana ya fonimu ni dhana ambayo imejadiliwa na wataalamu mbalimbali wakitumia mitazamo tofauti tofauti. Wataalamu hao ni hawa wafuatao:-
Massamba, (2004) anasema fonimu ni kipande kidogo kabisa katika mfumo wa sauti za lugha ambacho kina sifa pambanuzi  kuweza kukitofautisha na vipande vingine vya aina yake. Sauti pambanuzi katika mfumo wa lugha.
Massamba na wenzake, (2004) wanasema fonimu ni katamkwa kilicho bainifu katika lugha fulani maalumu.
Mgullu, R.S akimnukuu Jones, (1975). Fonimu ni kundi la sauti katika lugha fulani, lenye sauti muhimu (phonemes) pamoja na sauti zinazohusiana na ambazo hutumiwa mahali peke katika muktadha maalumu.
Tunasoma kuwa wataalamu hawa wametofautiana katika kuelezea dhana nzima ya fonimu, wakati Massamba (2004), anasema fonimu ni kipande kidogo kabisa katika mfumo wa sauti za lugha, Jones (1975) akinukuliwa na Mgullu anasema kuwa fonimu ni kundi la sauti katika lugha fulani.
Kwa mujibu wa wanakikundi tunasema kuwa fonimu ni kipashio kidogo cha kifonolojia kinachoweza kubadili maana ya neno katika lugha fulani (mahususi) kwa mfano pata – baba.
Dhana ya fonimu kuvuka mipaka na kuingia katika fonimu nyingine ni pale fonimu fulani inapoliacha umbo lake asilia na kuingia katika umbo jingine. Dhana hii imenukuliwa na Massamba (2010) kutoka kwa mtaalamu Bloch (1941).
Bloch (1941) anashawishi kwa kiasi kikubwa kuwa fonimu kuvuka mipaka ni tukio la kawaida katika lugha ya asili kutokana na ushahidi kuwa alofoni za fonimu moja zinaweza kutofautiana kwa kiasi kikubwa kifonetiki. Wakati mwingine zinakuwa na uhusiano na alofoni za fonimu nyingine tofauti na fonimu zilimotokea vile vile kifonetiki, sauti fulani inaweza kutokea kuwa katika fonimu mbili au zaidi katika lugha moja.
Bloch anaendelea kusema kuwa kuna aina mbili za fonimu kuvuka mipaka ambazo ni:-
Uvukaji mipaka usiokamili, unaamanisha hali ya fonimu ya aina moja kutokea katika fonimu mbili katika mazingira ya hali tofauti.
Kwa mfano:
Sauti [x] inaweza ikawa /a/ katika mazingira fulani na sauti [x] katika mazingira tofauti inaweza ikawa /b/, katika lugha ya Kidenimaki ( Jakoboson, Fant na Halle 1952) fonimu /t/ na /d/ zinakuwa na tabia tofauti mwishoni mwa silabi /t/ kutamkwa kama /d/ zinakuwa na mfano /hat/ kwenda /had/ wakati fonimu /d/ inakuwa / ð / kwa mfano /had/ inakuwa /hað/ japokuwa katika Kidenimaki neno roof (paa) ni sawa sawa na tag wakati day (siku) ni dag. Hii inamaanisha kwamba mwanzoni mwa silabi fonimu /t/ na /d/ hazibadiliki kwa maana nyingine kuna /d/ inayotokana na /t/ pia kuna /d/inayotokana na /d/ yenyewe. Katika lugha ya Kiswahili uvukaji wa mipaka usiokamili wa fonimu hutokea katika hali zifuatazo:-
Udogo             Ulimi               Loa
Undugu           Ndimi              Ndoana
Ndugu
Hivyo katika Kiswahili sauti /d/ hujitokeza kama /d/ wakati mwingine huvuka mipaka na kuwa /l/. sauti /l/ huwa /d/ endapo inatanguliwa na nazali /n/. endapo tutajikita kifonetiki ni ngumu kutabiri /d/ kama ni alofoni ya fonimu /d/ au fonimu /l/ itakuwa rahisi.
Mfano mwingine wa Kiswahili ni pale:
Ki + ti  = ki+eusi (kiti cheusi) katika mifano ya Kiswahili tutaona mabadiliko ya kifonimu yakijitokeza katika mfano wa fonimu /k/ inapofuatiwa na irabu halafu kuwa na mpaka wa mofimu kisha ikafuatiwa na irabu /e/ hubadilika na kuwa /ch/ (ki+eusi) = cheusi.
Mfano mwingine katika Kiswahili ni:-
N + buzi  (mbuzi)
N+dama  (ndama)
N+gombe (ng’ombe)
Pia tunaona kuwa nazali /n/ inapofuatiwa na kitamkwa /b/ hubadilika na kuwa /m/ inapofuatiwa na kitamkwa /d/ hubakia kuwa /n/ inapofuatiwa na kitamkwa /g/ hubadilika na kuwa [ ŋ ], hii inamaana kuwa katika mazingira haya sauti /m/, /n/ na [ŋ] ni alofoni za fonimu /N/
Uvukaji wa mipaka uliokamili. Huu ni uvukaji wa mipaka wa sauti moja kwenda sauti nyingine katika mazingira ya aina moja.
Kwa mfano:-
Katika lugha ya kiingereza uvukaji wa mipaka uliokamili unahusisha fonimu /t/ na /d/ inapotokea katikati ya irabu. Wamarekani hutamka sawa sauti ya ufizi [d].
Mfano:- Butter, Betting, Kitty ukiyatofautisha na Budden, Bedding, Kiddy katika mifano yote hiyo fonimu /t/ na /d/ hutamkwa sawa.
Kwa mfano:- /betting/ - [ beDiŋ] na /bedding/ = [beDiŋ]. Unapotamka haya maneno hautamki moja kwa moja /d/ wala /t/ bali inakuwa sauti katikati ya /t/ na /d/. kwa msingi huo fonimu /t/  na /d/ hupoteza uhalisia wake katika matamshi. Baada ya ule uhalisia kupotea sauti inayokuja huziwakilisha haizitofautishi sauti  /t/ na /d/. aina hii ya uvukaji ndio huitwa uvukaji wa mipaka wa fonimu uliokamili.
Kutokana na mifano tajwa hapo juu ni dhahiri kuwa fonimu inaweza kutokea katika umbo lake asilia na kwenda katika umbo jingine la fonimu au alofoni ambazo hutokana na fonimu moja. Hii husababishwa na mazingira ya utokeaji wake au sifa za kifonolojia.

MAREJEO:
Massamba, D.P.B. (2004). Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha. Taaasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili. Dar es salaam.
Massamba, D.P.B na wenzake. (2004). Fonolojia ya Kiswahili Sanifu. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili. Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Massamba, D.P.B. (2010). Phonological Theory: History and development. Institute of Kiswahili Studies. UDSM.
“Kwa hakika hakuna tofauti kati ya vivumishi na vikumushi.”
Vikumushi na vivumishi ni dhana mbili ambazo zimekuwa zikileta mkanganyiko mkubwa sana katika taaluma ya isimu. Maneno haya huweza kufanana na kufanya kazi sawa, lakini kwa upande mwingine huweza kutofautiana. Kama inavyojadiliwa hapa chini.
Chuo kikuu cha Oxford (2005) wamefasili kikumushi kuwa ni neno ambalo linaweza kuwa kivumishi au kielezi ambacho kinaelezea neno au kundi la maneno mengine (tafsiri). Katika fasili hii maana ya kikumishi imetolewa kiupana kwa kiasi fulani, lakini bado kikumushi kinaweza kuwa zaidi ya kivumishi au kielezi, na kuwa kitenzi na aina nyingine za maneno.
Khamisi na Kiango (2002:58) wameeleza maana ya kikumishi kuwa ni maneno ambayo siyo vivumishi asilia, lakini hufanya kazi kama vivumishi, yaani kazi ya kukumusha (kuongeza sifa au taarifa muhimu) nomino. Wanaendelea kusema kuwa vikumishi siyo vipashio vilivyo katika kiwango cha neno tu, bali ni pamoja na makundi ya maneno ambayo yamo katika kiwango cha kirai au kishazi.
Mfano; Kikumushi nomino: baba watoto; Kikumushi Kirai: baba wa taifa (KH) Kikumushi Kishazi: mtoto aliyeshinda.                                    
Hivyo basi kutokana na fasili hizo mbili zilizotolewa tunaweza kusema kuwa kikumushi huweza kufasiliwa katika mawanda finyu na mawanda mapana.
Katika mawanda finyu; kikumushi ni maneno yanayotoa taarifa ya ziada kuhusu nomino. Mfano; watoto wangu, mtoto wa juma. Maneno wangu na wa Juma ni vikumushi vya nomino watoto na mtoto.
Katika mawanda mapana: kikumushi ni maneno yanayotoa taarifa ya ziada kuhusu aina nyingi ne yoyote ya maneno yaani nomino, kitenzi, kielezi. Mfano; aliyeimba kwa madaha, Mfano wa pili; Anacheza      vizuri sana. Neno kwa madaha  na vizuri sana yanakumumusha vitenzi aliyeimba na anacheza vizuri.
Kwa upande mwingine kivumishi kama aina mojawapo ya aina za maneno imefasiliwa na wataalamu kama ifuatavyo; Matei (2009:43) anasema kuwa “kivumishi ni neno ambalo hutoa maelezo zaidi kuhusu nomino au kiwakilishi cha nonimo. Ni neno ambalo huonesha sifa mojawapo ya nomino/kiwakilishi cha nonimo.” Fasili hii inajitosheleza kwani mara nyingi kazi kubwa ya kivumishi ni kutoa sifa juu ya nonimo au kiwakilishi. Mfano, Mtoto mzuri. Neno mzuri ni kivumishi kinachovumisha nomino mtoto.
Baada ya kuelezea fasili mbalimbali za maneno makuu, maelezo yafuatayo huelezea kwa kina ni jinsi gani kivumishi ni kikumushi.
Katika fasili ya kivumishi na kikumushi, huweza kuleta ufanano fulani kwani kivumishi hutoa maelezo zaidi kuhusu nomino. Pia kwa maana finyu ya kikumushi ni kwamba kinatoa taarifa ya ziada kuhusu nomino. Hivyo basi kivumishi na kikumushi huelezea juu ya nomino. Mfano, Kijana mtanashati, mchezaji mashuhuri. Kwa muktadha huu neno mtanashati na mashuhuri huelezea juu ya nomino, hivyo maneno hayo yote ni vikumushi au vivumishi kwani vivumishi na vikumushi vyote hufanya kazi ya kutoa maelezo ya ziada juu ya nomino. Kutokana na kufanya kazi sawa katika sentensi, tofauti inaweza isiwepo. Mfano, mwanafunzi msafi. Mwanafunzi aliyeugua amepona. Hivyo neno msafi katika sentensi ya kwanza ambayo ni kivumishi na aliyeugua katika sentensi ya pili ambayo ni kikumushi hufanya kazi sawa ya kutoa taarifa juu ya nomino.                                                                                                                                  
Hata hivyo ufanano unaoonekana kati ya kivumishi na kikumushi ni pale tu kikumushi kitakapofasiliwa kiufinyu, lakini kikumushi kwa maana pana hudhihirisha tofauti kubwa sana kati ya kivumishi na kikumushi kama inavyooneshwa hapa chini.
Kivumishi huwa ni neno moja lakini kikumushi huwa ni neno moja au zaidi. Mfano; ng’ombe mweusi anakunywa maji. Neno mweusi ni kivumishi ambapo ni neno moja. Mwalimu aliyenipa kalamu ameondoka. Katika sentensi hii neno aliyenipa kalamu ni kikumushi chenye zaidi ya neno moja. Hivyo kivumishi ni neno moja tu lakini kikumushi huweza kuwa neno moja au zaidi, kirai au kishazi.
Kivumishi hutoa taarifa kuhusu nomino au kiwakilishi tu lakini kikumushi hutoa taarifa zaidi juu ya nomino, viwakilishi na aina zingine za maneno. Mfano; kiongozi muadilifu huongoza kwa busara, wewe ni msafi kuliko wote. Maneno muadilifu na msafi hutoa taarifa juu ya nomino na kiwakilishi. Mfano; anayetembea kwa maringo. Neno kwa maringo ni kikumishi kirai kihusishi ambacho hutoa taarifa juu ya kitenzi anayetembea.
Mara nyingi neno kivumishi hutumika kuelezea aina ya maneno hayo katika muktadha wa kimuundo na kileksika lakini kikumushi hutumika kuelezea maneno hayo hayo (ambayo ni kivumishi) na maneno mengine katika muktadha wa kidhima, huangalia kazi ya neno hilo. Mfano; mtoto mpole hulelewa vizuri. Neno mpole katika muktadha wa kimuundo ni kivumishi lakini katika muktadha wa kidhima ni kikumushi kwani hufanya kazi ya kutoa taarifa juu ya nomino mtoto. Mfano mwingine, mwanafunzi mtukutu hafaulu vizuri. Neno mtukutu ni kivumishi kimuundo na kikumushi kidhima.
Kivumishi huweza kuwa katika ngazi ya neno na kirai katika tungo. Mfano; mchezaji mashuhuri. Neno mashuhuri ni aina ya tungo neno ambalo ni kivumishi na ni aina ya tungo kirai ambalo ni kirai kivumishi. Hivyo kivumishi hakiwezi kuvuka ngazi hizo mbili za tungo, lakini kikumushi huweza kuwa katika ngazi ya tungo neno, kirai, kishazi na hata sentensi. Mfano; mwanafunzi anayesoma kwa bidii atafaulu mtihani. Neno mtihani limesimama kama kikumushi cha kitenzi atafaulu kama tungo neno. Kwa bidii ni kikumushi kirai, anayesoma ni kikumushi kishazi.
Utofauti mwingine hujitokeza katika dhana kwamba kila kivumishi ni kikumushi, lakini si kila kikumushi ni kivumishi. Hivyo basi kwa muktadha huu siyo dhahiri kuwa kivumishi ni kikumushi. Mfano; kijana mtukutu anaadhibiwa na mwalimu. Neno mtukutu ni kivumishi na ni kikumushi, lakini neno na mwalimu ni kikumushi na siyo kivumishi, hivyo ni kwa kiasi kidogo sana juu ya ufanano wa kivumishi na kikumushi.
Kwa kuhitimisha, kauli kuwa kivumishi ni kikumishi huthibitika tu endapo fasili ya kivumishi itakuwa katika muktadha wa maana finyu ambapo vyote huelezea juu ya nomino na hufanya kazi ya kutoa taarifa ya ziada juu ya nomino. Lakini kwa upande mwingine wa fasili ya kikumushi katika muktadha wa maana pana, kuna utofauti mkubwa kimuundo na kazi kati ya vikumishi na vivumishi. Hivyo basi kwa kiasi fulani vivumishi ni vikumushi na kwa kiasi fulani vikumushi si vivumishi.

MAREJEO:
Khamisi, A.M na John, G.K. (2002). Uchanganuzi wa Sarufi ya Kiswahili. TUKI. Dar es salaam.
Chou Kikuu cha Oxford (2005). Advanced Learners Dictionary. Oxford University Press. U.S.A.
Matei, A.K. (2008). Darubini ya Sarufi. Phoenix Publishers. Nairobi.
TUKI. (2010). English – Swahili Dictionary. (3rd Edition). MSM L.t.d. Mauritius.


22 comments:

 1. tafadhali fafanua uhusiano uliopo baina ya isimu na matawi mengine ya kielimu

  ReplyDelete
  Replies
  1. Asante sana kwa kutembelea blog hii. Nitajitahidi kufafanua hivi punde.

   Delete
 2. Tafadhali naomba ujadili uhusiano uliopo baina ya semantiki na matawi mengine ya isimu

  ReplyDelete
 3. Kwa kutumia dhana /mitazamo mbalimbali jadili asili ya lugha ya binadamu.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Soma;
   Habwe, J na Peter K. (2007). Msingi ya sarufi ya Kiswahili. Phoenix Publishers. Nairobi.

   Delete
  2. Soma kwa makini:
   Habwe, J na Peter K. (2007). Msingi ya sarufi ya Kiswahili. Phoenix Publishers. Nairobi.

   Delete
 4. Fafanua dhana ya Utawala wa kiuambajengo,kutawala na kutawala kwa karibu, mahusiano ya kutangulia; na mahusiano ya mama, binti, na madada.

  ReplyDelete
 5. This comment has been removed by the author.

  ReplyDelete
 6. hongera kwa kazi nzuri,,,nakushauri sherehesha zaidi katika dhana ya UAMBISHAJI na MAUMBO YA VITENZI.,,ahsante

  ReplyDelete
 7. Nashukuru kwa uelekezi huo mwafaka

  ReplyDelete
 8. eleza kwa kutoa mifano mwafaka umuhimu wa isimu

  ReplyDelete
 9. heko,tafadhali nieleze malengo ya isimu

  ReplyDelete
 10. NINI UHUSIANO KATI YA MOFOLOJIA NA NENO

  ReplyDelete
 11. asssssssaaaaaaateeeeeeeeeeeeeeeeeeee kwa kazi nzuri........................

  ReplyDelete
 12. Naomba mnielezee dhana nzima ya unominishaji na aina za unominishaji

  ReplyDelete
 13. asante sana kwa mada hizi.zimenifaa sana

  ReplyDelete
 14. Kuntu! Kazi nzuri kwa kweli.
  Naomba huzungumzie suala la mshikamano katika Diskosi.

  ReplyDelete