Monday, 28 October 2013

MAKUTANO YA FASIHI


FASIHI SIMULIZI NA FASIHI MAMBOLEO YA KIAFRIKA

UTANGULIZI:
Maswali ya Udadisi
  1. Fasihi Simulizi ni nini?
  2. Fasihi Mamboleo ni Fasihi ya namna gani?
  3. FS na FM zinahusianaje? (ni tofauti?, ni sawa?,….) Je upo mpaka bayana baina ya FS na FM?
FM……..Fasihi andishi. Huitwa FM kwa sababu kiumri FS ni kongwe zaidi ya FA. Hujumuisha sanaa mbalimbali ziliwasilishwa kwa njia ya maandishi, kama vile riwaya, ushairi, tamthilliya na hadithi fupi. Mijadala mingi ya wanazuoni wa mwanzo kuhusu FS na FA….ilichunguza sana tofauti kati ya sanaa moja na sanaa nyingine. Katika hatua hiyo ya uchunguzi, walidiriki kunena kuwa FA ni fasihi imara na thabiti zaidi ya FS, kwa upande mwingine, wapo walioeleza kuwa FS ni kongwe zaidi ya FA. Katika mjadala wetu, hatutajihusishi sana na majadiliano ya utofauti wa sanaa hizi mbili, bali tunachochunguza ni MWINGILIANO ULIOPO BAINA YA FS NA FA.

Hii haina maana kuwa FS na FA hazitofautiani! Tunakiri kuwa hizi ni sanaa mbili tofauti lakini jambo la msingi hapa ni kuwa licha ya kuwepo kwa toafuti hizo, sanaa hizi zinaingiliana na zinakamilishana. Kwa Yule anayetaka kujikumbusha kuhusu tofauti zilizopo baina ya FS na FA, ajaribu kuzingatia dondoo zifuatazo:
Ø  Uwasilishwaji kwa hadhira
Ø  Vijenzi vyake: mwandishi, mchapaji na msomaji……… mambo sita (Mulokozi)
Ø  Idadi ya tanzu
Ø  Umiliki: jamii nzima….sio
Ø  Aina ya hadhira: hai na isiyo hai
Ø  Upokeaji wa mabadiliko; rahisi au la
Ø  Aina za wahusika: binadamu au wanyama, mazimwi, miungu, mapepo
Ø  Uhifadhi: kichwani, njia ya mapokeo … tofauti hii ni ya kimapokeo kwani sasa hivi kuna mabadiliko.
MWINGILIANO BAINA YA FA na FS
a)    Dhana ya mwingiliano…….:
b)  Suala hili linawezekanaje? Mbinu gani wanatumia watunzi katika kuzichotarisha FA na FS? Kuna mbinu mahsusi au huu ni mchakato wa kiholela unaotokea bila mantiki yoyote?
c)      Je, ni kwanini mambo haya yanatokea?
d)    Je, ujitokezaji wa hali hii (Maingiliano na Makutano ya FS na FA) una athari gani katika sanaa husika (kiwima na kimlalo)
MAINGILIANO/MAKUTANO………Ujitokezaji wa vipengele vya sanaa moja katika sanaa nyingine. Kwa mfano, ujitokezaji wa mbinu za fs katika fa. Wapo baadhi ya watunzi wa FA wanaotumia vipengele vya FS katika kuunda kazi zao. KAZI HIZO ndizo tunazoziita FM. Pia, kwa muda mrefu FS imekuwa ikitumia nyenzo mbalimbali za FA katika KUUNDA, KUSAMBAZA NA KUHIFADHI sanaa yake.
JUKUMU LETU:
·         Kubainisha vipengele vya FS katika FA
·         Kutathmini mbinu zitumikazo kuchotarisha sanaa hizi
·         Kujadili athari ya uchotarishaji huo katika sanaa husika.
Vipengele vya FS katika FA
Kazi na Watunzi wao
Kwa kuchunguza kazi za watunzi mbalimbali waliotumia vijenzi vya kifasihi simuizi kuunda kazi zao. Kuna idadi kubwa ya watunzi waliotumia mbinu hii;
·         Song of Lawino na Song of Ocol….. Okot p’ Bitek
·         The Forest of a Thousand Demons,
·         The Forest of God,
·         Expedition to the Mount of Thought.,,,,,,zote ni riwaya za Daniel O. Fugunwa
·        Palm Wine Drinkard
·        My Life in the Bush of Ghost…….. za Amos Tutuola
·        Nguzo Mama…….P. Mhando
·        Jogoo Kijijini na Ngao ya Jadi…….E. Hussein
Mbinu za Kifasihi Simulizi
Watunzi hawa wametumia mbinu mbalimbai za kifasihi simulizi katika kuunda sanaa zao za kimamboleo. Ingawa maudhui ni mapya, lakini mbinu ni za kijadi. Mbinu hizo ni pamoja na hizi zifuatazo
·         Toni,
·         Methali,
·         Nahau,
·         Takriri,
·         Nyimbo,
·         Hadithi,
·         Wahusika kama vile: mizimu, miungu na wafalme, mahoka….
·   Mbinu za kiutendaji kama vile: Maigizo, Muziki, Uchezaji wa dansi, Utambamji wa hadithi
Mbinu katika Maingiliano haya (Mbinu za Kiuchotarishaji)
Kimsingi watunzi wa kisasa wametumia mbinu za kijadi kama ilijadiliwa hapo awali. Mbinu hii iliwawezesha kuchanganya mbinu za kijadi na maudhui ya kisasa ili kuunda kazi mpya za kimamboleo. Tunaweza kusema kuwa ili kufanukiwa lengo lao waliongozwa na mbinu kuu tatu: TAFSIRI, UBADILIDHAJI na UUMBAJI UPYA.
TAFSIRI:
Kuchukua kazi za fs zilizoandikwa na kuzihamishia katika lugha nyingine, wakati huohuo maudhui hufanyiwa maboresho
UBADILISHAJI
Kuchukua vionjo vya kijadi kama vilivyo na kuvihamishia katika fasihi ya kimamboleo. Mfano: Tutuola anatumia hadithi ya kijadi na kuandika katika mtindo wa kimamboleo
UUMBAJI UPYA
Utumizi wa baadhi ya fani za kijadi katika kazi za fasihi za kimamboleo. Kwa mfano; katika Wimbo wa Lawino na Okoli,  kuna matumizi ya fani za nyimbo za kabila la Kiacholi.
Athari ya Utunzi wa Namna hii
Kulikuwapo na athari za namna mbili: kutukuzwa kwa watunzi husika na kupuuzwa kwa utunzi huo.
KUTUKUZWA
  • Mbinu hizi zilifanya au zilisababisha kazi husika kupendwa au kusomwa zaidi barani Afrika.
  • Baadhi ya watunzi walipewa tuzo.
  • Kutokana na umaarufu na kukubalika kwa kazi husika zilitafsiriwa katika lugha nyingine za kigeni….kingereza, kifaransa, 
KUPUUZWA
·      Kazi husika zilikosolewa; kwa sababu ya kutumia lugha au kingereza kibovu na pia kwa kutumia mbinu za kijadi (miungu, mahoka na mizimu wenye nguvu za ajabu)
·   Maudhui yake yalionekana ya kijinga: jamii ya Kiafrika ilisawiriwa kuwa inaabudu  mizimu na hatimaye basi kushadidiwa kuwa maudhui haya yaliunga mkono hoja za wamagharibi kuwa kabla ya ukoloni waafrika walikuwa washamba na wasiostaarabika
HITIMISHO
Mwisho tunahitimisha kwa kusema kwamba, Masimulizi ya kijadi yanaweza kubadilishwa katika lugha ya mawasiliano ya kiulimwengu bila kupoteza mvuto wake. Katika kufanya hivyo, kunakuwa na maudhui mapya yanayowasilishwa kwa kutumia mbinu za kijadi. Kwa kiwango kikubwa kazi nyingi za kimamboleo tulizonazo leo hii hazina tofauti na visakale vya fasihi simulizi. Hata hivyo, ni vyema pia kudokeza kuwa suala hili bado linaitaji utafiti wa kina.

No comments:

Post a Comment