SINONIMIA
(UWASILISHAJI)
Neno sinonimia limeelezwa na wataalamu mbalimbali na kwa namna tofauti kama ifuatavyo;
Habwe na Karanje (2004:209), sinonimia ni uhusiano wa kileksia ambapo huwa kuna maumbo katika lugha ambayo maana zake ni sawa. Maumbo haya yanaitwa sinonimu. Basi sinonimu ni visawe vya sinonimia moja.
Yule (1985:95), sinonimia ni maneno mawili au zaidi yenye maumbo yanayohusiana ambayo huweza kubadilishana nafasi katika mazingira fulani lakini sio mazingira yote katika sentensi.
Linsky (1952), sinonimia ni ile hali ya maneno mawili ya lugha kufanana endapo yatakuwa na maana zinazofanana.
· Fedha, hela na pesa· Mwizi na mhujumu.· Shimo, tobo, tundu na upenyo
Sinonimia imegawanyika katika makundi mawili;1. Sinonimia za kimantiki. mfano; wadia na fika, aina na kategoria, anuwai na mbalimbali.2. Sinonimia kuntu.
Katika lugha zote duniani ni muhari kupa sinonimia kuntu kama inavyojibainisha kwa kuvitzama visawe tofauti tofautti kama ifuatavyo hapa chini:
1. [Asili, chanzo, chimbuko, kisa na usuli]
a) Daktari alitueleza asili ya ugonjwa huo na athari zake usipotibiwa mapema.b) Waziri wa fedha aliwaeleza waandishi wa habari chanzo cha mfumuko wa bei nchini.c) Mwalimu wa lugha alitufundishanchimbuko la kugha ya Kiswahili.d) Tulielewa kisa cha aliyekuwa waziri mkuu kujiuzuru.e) Professa Issa Shivji alitueleza usuli wa katiba mpya.
Istilahi zote zilizotumika katika sentensi hizi si visawe kuntu kwani haviwezi kubadilishana nafasi pasipo kuathiri maana ya msingi kwa maana nyingine hutumika kwenye weledi na nyingine kufuatana na muktadha.
2. [ Fedha, pesa, hela, senti na faranga]
a) Waziri mpya wa fedha ameanisha mikati ya kuondoa mfumuko wa bei nchini.
b) Thamani ya hela ya Tanzania kwa sasa iko chini ukilinganisha na ile ya Kenya.
c) Kalamu ya risasi huuzwa kwa senti mia moja tu.
d) Wachezaji wa mpira wa miguu katika klabu za Ufaransa hulipwa faranga laki tano kwa wiki kama sehemu ya mshahara wao.
e) Mtoto wa Rais ana pesa za kutosha kununua timu ya Liverpool.
Seti za sinonomia zilizotumika hapo juu haziwezi kubadilishana nafasi kwa kila sentensi hii ni kutokana na sababu kuwa baadhi ni rasmi na nyingine si rasmi katika mazingira Fulani, pia nyingine zimekopwa katika lugha za kigeni hazitumiki katika lugha yetu, mfano Faranga
3. [Fedheha, aibu, soni, twezo na kashfa]
a) Kilikua kitendo cha fedheha kwa mwalimu kulewa wakati wa kazi.b) Ni jambo la aibu kwa mwanamuke kukamatwa ugoni na mwanaume mwingeni.c) Mwanahewa hakuona soni kutukana matusi machafu hadharani.d) Kijana wake alionyesha twezo kwa kutotekeleza maagizo ya Baba yake.e) Mkurugenzi wa udhibiti wa ubora wa bidhaa nchini amesimamishwa kazi kwa kashfa ya ufujaji wa mali za shirika.
Maneno ya kisinonimia katika sentensi hizo juu sio sinonimia kuntu kwani hayawezi kubadilishana nafasi na kutoathiri maana ya msingi kwani hutofautiana matumizi katika miktadha mbalimbali
4. [ Habari, maelezo, ripoti, taarifa na ujumbe]
a) Musa alitupasha habari kilichojiri katika kikao cha madiwani.b) Mwalimu alitoa maelezo jinsi ya kufanya kazi ya nyumbani aliyotupatia.c) Mhandisi alisoma ripoti mbele ya Rais ju ya utafiti kuhusu upatikanaji wa vyanzo vya nishati ya umeme.d) Taarifa iliyosomwa na afisa kilimo mbele ya madiwani ilihusu maandeleo ya kilimo katika kata yetu.e) Mkuu wa shule yetu alipokea ujumbe kutoka kwa afisa elimu wa wilaya ukitaka shule ifungwe kwa kukosa vyoo.
Seti ya visawe hivi si sinonimia kuntu kwani hazibadilishani nafasi pasipo kuathiri dhana ya msingi kwenye sentensi kwani hutumika katika mazingira tofauti ya kidhima. Hivyo hakuna sinonimia kuntu katika lugha yoyote ile duniani ambazo huweza kubadilishana nafasi pasipo kuathiri maana ya msingi ya neno au sentensi kwa ujumla .
5. [Hafifu, nyonge, duni, dhaifu na goigoi]
a) Bidhaa za viwanda vya nchini Tanzania ni hafifu.b) Watoto wa mitaani walikua na hali duni sana tulipowatembelea.c) Ugonjwa wa UKIMWI umemfanya Juma awe dhaifu.d) Hasani alikuwa mnyonge alipougua ugonjwa wa kifua kikuu.e) Waziri wa kazi aliwataka wakulima wasiwe goigoi katika kufanya kazi
Istilahi zilizotumika katika katika sentensi hapo juu si visawe kuntu,kwani haziwezi kubaadilishana nafasi bila kubadili ile maana ya msingi. kwa mfano; istilahi hafifu na nyonge haziwezi kubadilishana nafasi katika sentensi
6. [hakimu, mwamuzi, jaji, kadhi na refa]
a) Migogoro baina ya wakulima na wafugaji ilitatuliwa na hakimu watatu.b) Mwamuzi alipigwa sana na mashabiki katika mchezo kati ya simba na yanga.c) Mahakama ilikua na jaji mmoja tu aliyesikiliza makosa ya jinai.d) Mkutano wa waislam uliongozwa na kadhi kutoka jiji la Arusha.e) Watazamaji wa mchezo wa ngumi walifurahia maamuzi ya refa
Maneno yaliyotumika katika sentensi hapo juu yanadhihirisha kutokuwepo kwa visawe kuntu kwa sababu hayawezi kubadilishana nafasi katika sentensi bila kuathiri maana kuu. Mfano; neno kadhi na refa hayawezi kubadilishana nafasikatika sentensi bila kuathiri maana.
7. [Hamaki, hasira, ghazabu, uchungu na uchu]
a) Ashura alihamaki baada ya kuibiwa mkufu.b) Juma alionyesha hasira sana katika ugomvi ule.c) Kikao kilikua na wajumbe wenye ghadhabu sana dhidi ya mwenyekiti wao.d) Joyce alikua na uchungu wakati alipopelekwa hospitali kujifungua.e) Nyumbani kwetu tumefuga mori watatu
Katika sentensi hizo hapo juu, istilahi zilizotumika si visawe kuntu kwa sababu haziwezi kubadilishana nafasi katika sentensi bila kupotosha maana ya msingi. Mfano; maneno, ghadhabu na mori kama yalivyotumika hapo juu hayawezi kubadilishana nafasi katika sentensi bila kubadili maana.8. [Hamu, shauku, tamaa, nyege na uchu]a) Bibi alikua na hamu ya kula nyama ya bata.b) Vijana wa chuo cha ufundi walikua na shauku ya kutaka kujua asili ya binadamu.c) Josephat aliuawawa sababu ya tamaa zake mwenyewe.d) Halifa alikua na nyege ya kufanya mapenzi na mke mtu.e) Vijana walikua na uchu wa kutaka kujua ukweli juu ya sayansi za angaIstilahi zilizotumika katika sentensi hapo juu si visawe kuntu kwa kua haziwezi kubadilishana nafasi katika sentensi bila kupotosha maana. Mfano Maneno kama uchu na nyege hayawezi kubadilishana nafasi katika sentensi bila kubadili maana ya msingi ya sentensi husika.9. [Hifadhi, ficha, funika, sitiri na gubika]a) Amina amehifadhi fedha zake benki ya CRDB.b) John amejificha chini ya godoro.c) Wema amejifunika mwili mzima.d) Nguo yake Amina imemsitiri vizuri.e) Aisha amejigubika kichwa kizimaVisawe hivi si sinonimia kuntu, kwasababu haviwezi kubadilishana nafasi katika mazingira yote na maana yake ikabaki ileile. mfano; kiisawe sitiri na gubika, sitiri mtu anaweza kuvaa nguo ambayo imesitiri baadhi ya viungo vya mwili lakini gubika ni pale ambapo mtu amefunika kabisa mwili mzima bila ya kuacha hata sehemu ndogo ya mwili wake.
10. [Hohehahe, masikini, fukara, mkata na kabwela]a) Watu wengi vijijini ni hohehahe.b) Vikongwe walio wengi vijijini ni maskini.c) Amina ni fukara sana.d) Baba Paulini ni mkata.e) vijana wengi vijijini ni makabwelaVisawe hivi vyote sio sinonimia kuntu kwasababu haviwezi kubadilishana nafasi katika mazingira yote na maana ikabaki ileile, lazima maana itabadilika. mfano; kisawe fukara na maskini katika sentensi zifuatazo; Amina ni fukara na Amina ni maskini. Sababu fukara ni mtu aliye maskini kabisa asiye na pato la kutosha, hivyo mtu anaweza kuwa maskini lakini sio fukara.11. [Jamii, ingilia, najisi, lala na zini]a) Anna amejamiiliwa na John.b) Frank amemwingilia Asha.c) John amemnajisi Paulini.d) Khadija amelaliwa na juma.e) Wanafunzi wengi wa vyuo vikuu ni wazinifuVisawe hivi sio sinonimia kuntu kwasababu haviwezi kubadilishana nafasi katika miktadha yote na maana ikabaki ileile zinapo badilisha nafasi maana hubadilika, mfano; Frank amemwingilia Asha ni tofauti na John amemnajisi Paulina kwani kisawe ingilia ni fanya kitendo cha kujamii hata walio oana mmoja anaweza kumwingilia mwingine lakini kunajisi ni kule kujamiiana na mtu bila hiari yake ( Baka).
12. [Kejeli, dharau, simanga, dhihaki na tania]a) Juma amemkejeli mwalimu wa fasihi.b) Eva aliwadharau wanaume wa kijijini kwao.c) Neema alimsimanga Jane kuhusu hela yake.d) Wayahudi walimdhihaki Yesu msalabani.e) Eva na Franki walitaniana kuhusu jambo laoHizi si sinonimia kuntu kwasababu hazibadilishani nafasi katika miktadha yote, na zinapobadilishana maana hubadilika. Mfano; kejeli, unaweza kumsema mtu kwa kumtania na kumdharau mtu ni kumshushia mtu heshima yake.13. [Kishindo, kelele, ghasia, zahamu na vurugu]a) Tito ameingia chaumbabi kwa kishindo kikubwa sana kilichozua ugomvi.b) Wanafunzi walipiga kelele darasani.c) Wanakijiji walileta ghasia kubwa dhidi ya polisi.d) Mgomo wa walimu ulileta zahama kubwa kwa taifa letu.e) Wapemba walizua vurugu sokoni siku moja kabla ya kifo cha baba wa TaifaVisawe hivi si sinonimia kuntu kwa kua baadhi ya maneno hayawezi kubadilishana nafasi katika sentensi hiz. Mfano kisawe kelele na ghasia haviwezi kubadilishana nafasi na maana ikabaki vilevile.14. [Kosa, dosari, hitilafu, walakini na kasoro]a) Asha alifanya kosa kuiba mayai ya Blandina.b) Binti nimpendaye ana dosari kiunoni.c) Gari la diwani wa kata ya Mengo lina hitilafu katika injini.d) Mbonde alikua na walakini na matokeo ya mtihani wa Neema.e) Nguo niliyo nunua jana ina kasoro kwenye mfukoSeti hii ya visawe si sinonimia kuntu kwani baadhi ya maneno hayawezi kubadilishana nafasi, mfano; kisawe kosa na walakini hivi haviwezi kubadilishana nafasi na sentensi ikawa na maana ileile.15. [Kung'uta, nyuka, dunda, twanga na timba]a) Mwanafunzi amekung'utwa na mwalimu wa nidhamu mbele ya wageni.b) Mama amemnyuka mdogo wangu fimbo tatu.c) Masha anamdunda Tande ngumi za usoni.d) Lema amenitwanga hadi nimepoteza fahamu.e) Wezi walimtimba mlinzi getini na kufanikiwa kuingia ndaniManeno haya ni sinonimia kuntu kwani yanaweza kubadilishana nafasi katika sentensi zote zote pasipo kuathili maana ya sentensi husika.16. [Laumu, karipia, kemea, fokea na shutumu]a) Wanafunzi walimlaumu mwalimu kwa kuwapa alama za chini katika mtihani wa historiab) Bosi alimkaripia mfanyakazi wake na hatimaye akamfukuza kazi.c) Mchungaji atakemea pepo la uzinzi kanisani.d) Mpenzi wangu amenifokea kama mtoto.e) Wazee walimshutumu Tenga alipomwaga pombe ya kutambikiaManeno haya si sinonimia kuntu kwasababu baadhi ya maneno hukataa kubadilishana nafasi.Mfano, kisawe laumu na kemea haviwezi kubadilishana nafasi na vikaw na maana ileile moja .
17. [Liwaza, burudisha, poza, tuliza, na fariji]
a) Tumaini aliwaliwaza wanae siku ya sikukuu ya krismas kwa kuwaandalia chakula kitamu na vinywaji baridi ambavyo hawakuvitumia kwa muda mrefu.b) Juma Nature aliwaburudisha watu na nyimbo zake za muziki siku ya sikukuu ya uhuru kwenye uwanja wa Taifa.c) Mafisadi hupoza wananchi kwa zawadi ndogondogo ili kuwazima vidomodomo vyao.d) Polisi walitumia mabomu ya machozi kutuliza ghasia za wananchi siku ya uchaguzi wa rais na wabunge mwaka mwaka 2010.
e) Wanafunzi wa shule ya msingi ya Miembeni warimfariji Asha baada ya kuibiwa fedha yake ya kununulia daftari
Seti hizi za maneno ni sinonimia kuntu kwa sababu zinaweza kubadilishana nafasi na kuleta maana ileile.
18 .[ Maafa, misiba, majanga, matatizo na balaa]
a) Meli ya mv bukoba ilileta maafa makubwa sana kwa nchi ya Tanzaniab) Kati ya majanga yaliyowahi kuikumba Tanzania ni njaa ya miaka ya 1997 na 1998 kutokana na mvua ya Elinino.c) Familia yam zee Mweta imekua ikikumbwa na matatizo ya misiba kila mwishoni mwa mwaka.d) Mnamo mwaka 1995 kijijini kwetu ilitokea misiba mingi sana.e) Mwaka huu Chuo Kikuu cha Dar es salaam kilikumbwa na balaa la ugonjwa wa redi eyes.
Maneno haya si sinomia kuntu kwa sababu hayawezi kubadilishana nafasi katika sentensi na maana ikabaki ile ile.
19. [Madaha, maringo, mbwembwe, majivuno, mado]
a) Kiongozi wa wanafunzi aliongoza kwa madaha alipokua akiwashukuru wanafunzi wenzake baada ya kupita katika uchaguzi wa wabunge.b) Asha alitembea kwa maringo kwa sababu aliambiwa na wanaume kwamba yeye ni mzuri.c) Hamisi aliongea kwa mbwembwe mbele ya wasichana wazuri.d) Amina alijivuna kwa kujiona kuwa yeye ni kipanga wa darasa baada ya kupata “A” ya Kiswahili.e) Kaseja aliweka madoido wakati wa kufunga goli la 3 siku ya mchezo.Maneno haya si sinonimia kuntu kutokana na kwamba hayawezi kubadilishana nafasi na maana ikabaki ile ile.20. [Madhumuni, nia, lengo, shabaha na dhamira]a) Hamis aliamua kumuoa Asha kwa madhumuni ya kumkomoa Ali.b) Walilima mazao mengi wakiwa na nia ya kupata fedha nyingi za kigeni.c) Osama aliipiga marekani akiwa na shabaha ya kuangamiza .d) Wanafunzi walimzomea mwalimu kwa lengo la kumtaka aache kutoa adhabu kali.e) Wasichana wengi hufanya ufuska huku dhamira zao zikiwashitaki.Maneno haya si sinonimia kuntu kwa sababu hayawezi kubadilishana nafasi katika sentensi na maana ikabaki ileile.21. [Majuto, majonzi, simanzi, masikitiko na huzuni]a) Majuto ni kijana mtukutu.b) Kifo cha Kanumba kilileta majonzi makubwa sana kwa wasanii wote.c) Baada ya kutalikiwa na mumewe Ana alipata simanzi kubwa moyoni mwake.d) Watanzania wengi walipata masikitiko walipo pata taarifa ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) kuhusu ufisadi ulio kithiri kwa viongozi wa ngazi za juu.e) Waathilika wa mabomu Gongo la mboto waliongea kwa huzuni jinsi walivyotelekezwa na serikali kutowalipa fidia zao
Seti hii ya visawe si sinonimia kuntu na haviwezi kubadilishana nafasi pasipo kuathiri maana ya msingi katika sentensi, kwani baadhi ya istilahi zimetumika kama nomino. Mfano; masikitiko na zingine zimetumika kama vielezi mfano; majonzi. Kwa maana hiyo katika sentensi (a) hapo juu haiwezi kubadilishana nafasi ya kisawe chake na sentensi nyingine pasipo kubadili maana ya neno hilo au kisawe hicho.
22. [Malaya, kahaba, mzinzi, mwasherati na fuska]
a) Mtaa wa Buguruni ni makazi ya wasichana malaya katika jiji la Dar es salaam.b) Binti tuliye mwona jana ni kahaba maarufu jijini.c) Mwanafunzi mzinzi amesimamishwa masomo.d) Mwalimu aliyetufundisha sana ni mwasherati mkubwa.e) Muhubiri yule maarufu sana ni fuska wa kwanza katika mtaa wetu.Istilahi za kisinonimia zilizotumika si kuntu kwa sababu haziwezi kubadilishana nafasi na kuwa na maana ile ile ya msingi, kwani matumizi yake hutofautiana. Mfano; kisawe malaya hakiwezi kubadilishana nafasi na kisawe kahaba pasipo kuharibu maana ya msingi.
23. [Mapenzi, mahaba, upendo, pendo na mapendo]
a) Wanaharakati wa Tanzania wameonyesha mapenzi ya dhati kwa Taifa lao kwa kuwakemea viongozi wasiowajibika.b) Mwanaisha hakuonyesha mahaba ya dhati kwa mumewe hivyo alipelekea ndoa yao kuvunjika.c) Wazazi wengi wana upendo wa dhati kwa wanao.d) Pendo la Kanumba kwa Lulu lilipelekea kifo chake.e) Askofu Kilaini alihubiri habari ya mapendo miongoni mwa waumini wa dhehebu la Lutherani siku ya uzinduzi wa kanisa lao
Seti hizi za kisinonimia si kuntu kwani haziwezi kubadilishana nafasi na kuwa na maana ileile kwani utumizi wake huzingatia muktadha husika. Mfano; kahaba na upendo haviwezi vikabadilshana nafasi na ikamaanisha maana ileile.
24. [ Mpumbavu, fala,
bwege, zuzu na mjinga]
a) Mwalimu alifafanua dhana ya mpumbavu wakati wa ufundishaji wa msamiati katika kipindi cha kiswahili.b) Juma alionekana fala katika mabishano yale.c) Abdalah alionyesha ubwege kwa kushindwa kujibu misamiati kwa kuogopa kuchekwa darasani.d) Mgambo wa jiji la Dar es salaam walionekana mazuzu baada ya kushindwa kutumia njia sahihi kudai stahiki zao.e) Wanasiasa wa Tanzania wamewaona wapiga kura wao ni wajinga kwa kuwapa ahadi zisizotekelezeka na wao kuwapigia kura.
Visawe vilivyotumika katika sentensi hizi si kuntu kwani haviwezi kubadilishana nafasi pasipo kubadili maana ya msingi na matumizi yake hutofautiana kwa kujikita katika muktadha, maudhui na ulasimi wa jambo. Mfano; zuzu na mjinga haviwezi kubadilishana nafasi vikaleta maana ileile.
25. [Msukosuko, kizaazaa, ghasia, fujo na uvumilivu]
a) Wananchi walipatwa na msukosuko mkubwa baada ya viongozi kukinzana madarakani.b) Asha alipigwa nondo, mama yake aliibua kizaazaa katika kulipiza kisasi kwa walio mpiga.c) Meli ilizama majini baada ya ghasia kubwa kuikumba na upepo mkali.d) Sara anapenda fujo.e) Mtoto yule ana uvumilivu sana.Mneno hayo si sinonimia kuntu kwasababu hayabadilishani nafasi katika miktadha yote, usinonimia huo upo katika istilahi.
26. [Mwandani, rafiki, mwenzi, mwenzana msiri]
a) Fausta alimwomba mwandani wake fedha za kujikimu.b) Juma na Neema ni marafiki wa muda mrefu.c) Oriva ana mwenzi wa darasa la saba.d) Sara na Suzi ni wake wenza.e) Juma ni msiri sana akipatwa na shida.Maneno hayo si sinonimia kuntu kwa sababu usinonimia wake upo katika istilahi tu na hayawezi kubadilishana nafasi katika miktadha yote.27. [Nywea, dhoofika, sinyaa, gofuka na konda]a) Miche yake ilinywea baada ya kukosa maji.b) Esta alidhoofika baada ya kuugua kwa muda mrefu.c) Majani yamesinyaa.d) Waliwashinda magoli matano katika mchezo wa gofu wa leo.e) Sala amekonda hadi sketi zake zote zinamshuka.
Visawe hivi sio sinonimia kuntu kwa sababu istilahi hizi hazibadilishani nafasi katika miktadha yote bali sinonimia hizi zipo kiistilahi zaidi na sio katika maana ileile wakati wote na katika miktadha yote.
28. [Ogopa, tukuza, abudu, tii na nyenyekea]a) Jane aliogopa sana alipositushwa na Jumapili.b) Nitamtukuza mungu siku zote za maisha yangu.c) Waumini wanamwabudu Mungu.d) Wanafunzi wana mtii mwalimu wao.e) Kunyenyekea wakubwa kunaongeza heshima kwako.Maneno hayo si sinonimia kuntu kwa sababu usinonimia wake upo kiistilahi, kimaana lakini hayabadilishani nafasi katika miktadha yake yote.
29. [Piga, chapa, charaza, tandika na zaba]
a) Baba amempiga mama.b) Mama amemcharaza mtoto viboko.c) Mwalimu amemtandika Asha viboko.d) Baba alimzaba mtoto kibao.e) Mwalimu amemchapa mwanafunzi.
Hii sio sinonimia kuntu kwa sababu sio leksimu zote katika hii orodha ya maneno zinaweza kubadilishana nafasi katika sentensi zote na katika miktadha yote. Mfano; katika sentensi " Baba amempiga Mama" Huwezi kusema Baba amemcharaza mama kwa sababu katika hali ya kawaida Baba hawezi kumcharaza mama.
30. [Potea, yoyoma, kosekana, toweka na adimika]a) Mtoto aliyepotea jana ameondoka.b) Juma ameyoyoma na kupotea gizani.c) Wajumbe wawili walipokosekana mkutano uliahilishwa.d) Mtoto aliye fika jana ametoweka.e) Mafuta yaliyopo adimika nchini serikali iliagiza mafuta toka nje.
Seti hii sio sinonimia kuntu kwa kuangalia sentensi zote, sio maneno yote ambayo yanayoingiliana na kubadilisha nafasi katika miktadha yote, Mfano; " Mtoto aliye potea jana ameonekana" haiwezi kubadilishana nafasi na neno adimika.
31. [Safu, mstari, foreni, msururu na mlolongo]a) Juma amepanga vitabu katika safu mbili.b) Mwalimu aliwaambia wanafunzi wapigie mstari jibu sahihi.c) Foreni ya magari imeanza kimara mpaka ubungo.d) Kulikua na msururu mkubwa wa watu kwenye msiba wa msanii wa filamu.e) Hadi alipofika kwa meneja alipitia mlolongo mrefu.Visawe hivi sio sinonimia kuntu kwa sababu sio maneno yote yanaweza kubadilishana nafasi katika sentensi zote kutokana na orodha yote ya maneno yaliyoorodheshwa. Mfano " Mwalimu aliwaagiza wanafunzi wapigie mstari jibu sahihi" huwezi ukasema mwalimu aliwaambia wanafunzi wapigie safu jibu sahihi.
32. [Sambaratika, momonyoka, vunjika, vurugika na tawanyika]a) Bomu lilipopigwa watu walisambaratika.b) Mwamba ulimomonyoka baada ya mvua kubwa kunyesha.c) Mtoto alipoangusha kikombe kilivunjika.d) Nywele za Asha zilivurugika baada ya kupigwa na upepo.e) Wanafunzi walipomaliza mtihani walitawanyika.Visawe hivi sio sinonimia kuntu kwa kuangalia sentensi zote sio leksimu zote zinaweza kubadilishana nafasi katika miktadha yote. Mfano; mtoto alipoangusha kikombe kilivunjika, huwezi kutoa neno vunjika na kuweka neno vurugika na kuachiana nafasi.
33. [Sifu, tukuza enzi, faharisha na himidi]a) Baba alimsifu mwanae kwa uhodari wa kazi.b) Wanakwaya walimtukuza mungu kwa nyimbo na mapambio.c) Tarehe 14 kila mwaka ni siku ya kumwenzi Baba wa Taifa.d) Kufaulu kwangu katika mitihani yangu kulimfaharisha Baba yangu.e) Wanakwaya walimhimidi mungu kwa nyimbo na vigelegele.Visawe hivi si sinonimia kuntu kwani badhi ya visawe kama sifu tukuza na himidi vinauhusiano wa karibu ambao kinapoingizwa katika sentensi ya kisawe sifu huweza kubadilisha nafasi na kisawe tukuza. Pia kuna visawe kama enzi na faharisha haviwezi kubadilishana nafasi na visawe sifu au tukuza.
34. [Tangazo, ilani, taarifua, notisi na onyo]a) Tangazo la waziri mkuu liliwafurahisha wananchi.b) Ilani iliyotelewa na jeshi la polisi iliwafanya watawanyike.c) Taarifa zilizotolewa jana zilikua ni za kweli.d) Notisi zilizo tolewa ziliwashitua wapangaji.e) Onyo lilotolewa na shirika la Tanesco limewafanya wanyabiashara kutorudia.Visawe kama tangazo, ilani, taarifa ni visawe ambavyo vina uhusiano wa karibu ambapo vinaweza kubadilishana nafasi katika muktadha tofauti. Lakini vilevile kuna baadhi ya visawe ambavyo havina uhusiano na vingine kama notisi na onyo (visawe hivi sio sinonimia kuntu kwani haviwezi kubadilishana nafasi)
35. [Tobo, tundu, shimo, pango na upenyo]a) Mwanga ulipenyeza katika tobo.b) Ukubwa wa tundu la sindano ulifanya uzi upite kwa urahisi.c) Shimo lilochimbwa lilikua na futi 24.d) Wezi walijificha pangoni.e) Upenyo mdogo uliwafanya wezi washindwe kukimbia na hatimaye kukamatwa.Visawe kama tobo, tundu na upenyo vina uhusiano wa karibu (yaani vinaweza kubadilishana nafasi ) lakini kwa upande wa visawe shimo na pango vina uhusiano wa karibu kwani vina uwezo wa kubadilishana nafasi. Mfano; Katika sentensi pango limejaa maji pia waweza sema shimo limejaa maji. Hivyo visawe hivi kwa ujumla havina uhusiano wa karibu kwani vimejitenga kimakundi.
36. [ Tosheleza, ridhisha, tosha, kidhi na kifu]a) Mofimu huru ni ile inayojitosheleza kimaana.b) Mapenzi anayonipa mpenzi wangu yananiridhisha.c) Mavuno tuliyo yapata yatatosha mpaka mwaka ujao.d) Mpenzi niliye naye hakidhi kabisa haja zangu.e) Kula chakula cha aina moja kila siku kunakifu.Visawe hivi havina uhusiano kuntu kabisa kwani vinajitegemea kimakundi , Mfano; tosheleza, ridhisha na tosha ni visawe ambavyo vinauhusiano yaani vina uwezo wa kubadilishana nafasi . Pia katika kundi la kidhi na kifu ni visawe ambavyo haviwezi kubadilishana nafasi . Kwa ujumla visawe hivi si sinonimia kuntu kwani vinasigana kimakundi kutokana na matumizi.
37.[Tuna, vimba, tutumuka, umuka na nenepa]a) Vijana wengi siku hizi wametuna vifua vyao utadhani wacheza mieleka.b) Umemwona Mwajuma amevimba tumbo utadhani ana ujauzito wa kujifungua.c) Wacheza mieleka wengi wametutumuka miili yao hii ni kwasbabu ya mazoezi mazito wanayofanya.d) Uso wa Asha umeumka kutoka na matumizi mabaya ya vipodozi vyenye kemikali.e) Siku hizi Jumanne amenenepa hii ni kwa sababu anafanya mazoezi kila siku asubuhi na jioni.Hizi ni sinonimia kuntu kutokana na kubadilishana nafasi katika miktadha yote na maana ni ileile.38.[Uvumi, tetesi, fununu, dokezi na unong'ono]a) Kuna uvumi uliotandikwa kila kona ya jiji la Dar es salaam kuwa idadi ya wasichana hapa chuoni imeongezeka.b) Zimesikika tetesi kuwa wanavyuo wanaongoza kwa kujiuza mitaani.c) Nimefikiwa na fununu kuwa mwaka huu wahitimu wa vyuo vikuu wote watapata ajira mapema sana.d) Asha amewadokeza rafiki zake kuhusu ujio wa rais Joel Mseveni nchini Tanzania.e) Imesikika minong'ono kwamba Makete ni wilaya inayoongoza kuwa na waathilika wengi wa ukimwi mkoani Iringa.Hizi ni sinonimia kuntu kutokana na kubadilishan nafasi au mazingira ya utokeaji bila kupoteza au kubadili maana iliyo kusudiwa.
39. [Uvumilivu, ustahimilivu, subira, imani na kifua]a) Uvumilivu umemshinda Subira kwa kichapo anacho kipata toka kwa mumewe hatimaye ameukimbia mji wake.b) Hatimaye John amepoteza nafasi yake kutokana na kutokuwa na subira katika harakati za kugombea nyadhifa za uongozi wa kijiji.c) Unatakiwa ustahimilivu wa hali ya juu sana ili kupata Shahada katika Chuo Kikuu cha Dar essalaam.d) Watanzania wengi hawana imani na viongozi wao kutokana na ahadi zao za uongo wanazozitoa.e) John haogopi kitu chochote kutokana na kifua alicho nacho.Hizi si sinonimia kutokana na sababu kwamba neno kifua haliwezi kubadilishana nafasi na neno imani kisha maana ikabaki kuwa kuwa ileile vivyo hivyo hata neno subira na imani haviwezi kubadilishana nafasi katika mazingira ya utokeaaji na maana ikabaki kuwa ileile.
40. [Wadhifa, madaraka, cheo, daraja na mamlaka]a) Wadhifa wa Amina katika chuo chetu ni waziri wa michezo.b) Asha kama mwanafunzi hana madaraka ya kumpiga Anna kwani wote ni wanafunzi.c) Mesia siku chache zilizopita alipandishwa cheo kutoka makamu mkuu wa chuo na kuwa mkuu wa chuo.d) Moses ameshuka darasa na hivyo imemlazimu kurudi masomoni tena.e) Mamlaka aliyopewa Mesia ni tofauti na kiwango cha elimu aliyonayo hivyo kufanya utendaji kazi wake kuwa mgumu.Hizi ni sinonimia kuntu kwani zinaweza kubadilishana nafasi mazingira ya utokeaji bila kupoteza maana iliyokusudiwa.Pamoja na kuwa visawe vilivyotumika katika sentensi hizo hapo juu kuwa na mahusiano ya karibu, lakini lugha zote duniani hakuna visawe kuntu ambavyo huweza kubadilishana nafasi katika sentensi bila kuathili maana ya msingi au ya awali, uwepo wa visawe viwili au zaidi lazima pia maana ya msingi katika sentensi zilizobadilishana kubadilika.
MAREJEO
Habwe, J. na Karanje, P. (2004) Misingi ya sarufi ya kiswahili, phoenix publishers Ltd.Nairobi-kenya.
TUKI (2004) Kamusi ya kiswahili sanifu, Oxford University press, Dar es salaam.
vizuri sana maana nimejua maana ya sinonimia na mifano yake
ReplyDeleteAthari za sinonimia
ReplyDeleteNimeelewa vizuri mno maana ya sinonimia
ReplyDeleteUmuhimu wa sinonimia?
ReplyDeleteIpo vizur sana hii makala
ReplyDeleteTofauti kati ya sinonimu na sinonimia ni gani
ReplyDelete