Thursday, 24 October 2013

KAMUSI



DONDOO KATIKA KAMUSI (CITATION FORMS)

Kulingana na Newell (1995) amebainisha nduni zifuatazo za Kongoo
a.       Maumbo yasiyo na mnyambuo ambayo hutokea katika hali ya Kifonolojia (Matamshi) ndiyo huingizwa katika kamusi mfano; mama, shangazi, sana, suri n.k
b.    Maneno ambayo hayana  viambishi ndiyo hudondolewa katika kamusi mfano; adhimisha, piga, adhimu vinaweza kuwa kidahizo.
c.       Maumbo huru yenye sifa za kifofonemiki huweza kuorodheshwa kama kidahizo. Umbo lenye mkazo mmoja tu.
d.      Maumbo yanayotambuliwa na wazungumzaji asilia wa lugha hiyo kama neno, yanaweza pia kuingizwa katika kamusi kama kidahizo. Hapa ni muhimu kupata tajiriba kutoka kutoka kwa wazawa.
e. Maumbo ambayo ni rahisi kuyabainisha kama neno yanapokuwa katika sentensi, huingizwa katika kamusi kama kidahizo: Kijana mdogo sana amesafiri leo asubuhi kwa ndege ya fastjet
f.      Maumbo yanayotokea mara kwa mara mfano mtoto Vs Kitoto hutumika mara kwa mara katika maandishi na mazungumzo. Katika kongoo ya Kiswahili kuna maneno yapatayo milioni kumi (10,000,000/=).
g. Maumbo yote yale yanayowakilisha maana ya msingi (Basic meaning) ya leksimu huingizwa katika kamusi kama kidahizo mf. Askarikanzu, mpigambizi, amevaa miwani n.k
h. Maumbo ya mashina ambayo maneno nyambulishi mengine yanaweza kuundwa, yanaweza kuorodheshwa pia kama kidahizo
i.       Maumbo yanayoweza kutumika kupata vitomeo vidogo (sub-entry) yanaweza kuingizwa katika kamusi kama kidahizo.

Mambo ya kuzingatia katika Uteuzi wa Vidahizo vya kamusi
1.      Umbo la neno: ni lile umbo ambalo mtumiaji wa kamusi anatarajiwa kulitafuta, mfano: pig.a, stahimili, dada, askari (askarikanzu).
2.      Muundo wa neno: neno linaweza kuundwa na:
-         Mofimu huru moja mf. Kalamu, Nyoka, Baba na mama
-      Mofimu zaidi ya moja kwa pamoja mf. Mchezaji (m-chez-a-ji), mkulima (m-ku-lim-a) n.k
-      Maneno mawili au zaidi ambayo yameambatana na kuwa na maana moja mf. Kifungua kinywa (kifunguakinywa), mwana mapinduzi (mwanamapinduzi), askari kanzu (askarikanzu).
-         Nahau, nahau ina hadhi ya neno kwa hiyo nayo inaingizwa katika kamusi kama kidahizo mf. Piga maji, vaa miwani, zunguka mbuyu.
3.     Uingizaji wa viambishi: wasomaji wa kamusi hawatafuti viambishi, hata hivyo husaidia kuelewa maana zalishwa. Vioneshwe mbele ya shina la neno husika kwa kutenganishwa na alama ya mawimbi. Mf. To.a ~ le, ~lew,~an, ~lesh n.k
4.   Tahajia: ni muhimu kufanya uamuzi wa tahajia itakayotumika kwa maneno yenye tahajia zaidi ya moja, kwa mf. Tasinifu Vs Tasnifu, Theatre Vs Theater, Burangeti Vs Blanketi, Kula Vs Kura
5.  Majina ya Pekee: majina ya pekee huwa hayaingizwi katika kamusi kama kidahizo isipokuwa kwa yale ambaya yanahusishwa na uvumbuzi au mwanafalsafa fulani mf. Umaksi, Kanuni ya Newton. Maneno haya lazima yaingizwe katika kamusi kama kidahizo kutokana na sifa za ziadi yaliyonazo yanaondoka kuwa majina ya pekee tu.
6.    Uingizaji wa Maneno ya Mkopo: tahajia ya maneno ya mkopo iingizwe kwa kufuata tahajia ya lugha lengwa. Mfano Editor – Edita – Editori, radio- redio- radio, machine-mashini – mashine. Baada ya kuwa mtunga kamusi umeamua ni tahajia ipi itatumika, chagua moja na itumike kwa kamusi nzima.



No comments:

Post a Comment