KUIBUKIA KWA NADHARIA YA MOFOFONEMIKI
Katika mada hii tumeangalia fasili ya
mofofonemiki kwa mujibu wa wataalam mbalimbali, kisha tukaangalia kwa ufupi
historia ya nadharia ya mofofonemiki na katika kiini cha mada tumejadili sababu
zilizopelekea kuibuka kwa nadharia ya mofofonemiki.
Kwa kuanza na fasili ya mofofonemiki kwa mujibu wa mtandao wa Wikipedia wanafafanua
mofofonemiki kuwa ni tawi la isimu linalojishughulisha na mwingiliano wa
mishakato ya kimofolojia na kifonolojia au kifonetiki. Pia hujishughulisha na
mabadiliko ya sauti yanayotokea katika mofimu wakati zinapoungana kuunda
maneno. (Tafsiri yetu).
fasili hii ina mapungufu fulani kwani,
mofofonemiki haijishughulishi na michakato yote ya kifonolojia na kimofolojia
bali ni baadhi tu ya michakato hiyo ambayo ilishindwa kufafanuliwa kwa kutumia
data za kifonolojia au kifonetiki peke yake.
The
New Oxford American Dictionary inafafanua kwamba, mofofonolojia/mofofonemiki ni tawi la isimu
linalojishughulisha na uwakilishi wa kifonolojia wa mofimu.
Hivyo basi tunaweza kusema kuwa, mofofonemiki
ni tawi la isimu linaloshughulikia matumizi ya kimofolojia katika kueleza
baadhi ya tofauti za kifonolojia ambazo isingewezekana kuzielezea kwa kutumia
data za kifonetiki au kifonolojia peke yake.
Baada ya kuangalia fasili ya neno
mofofonemiki ifuatayo ni historia fupi ya nadharia ya mofofonemiki. Kwa mujibu
wa Massamba (2010:82) akimrejelea Martnet (1965) anafafanua kwamba, istilahi
hii mofofonemiki/mofofonolojia ilipendekezwa kwa mara ya kwanza na N.S.
Trubetzkoy (1929). Trubetzkoy alitumia istilahi hii kwa maana ya tawi la isimu
ilinaloshughulikia matumizi ya mafolojia katika kuelezea baadhi ya tofauti za
kifonolojia ambazo isingewezekana kuzielezea kwa kutumia data za kifonolojia au
kifonetiki peke yake.
Baada ya kuangalia historia fupi ya mofofonemiki
yafuatayo ni mambo yaliyosababisha kuibuka kwa nadharia ya mofofonemiki.
Kuchunguza
ubadilikaji wa sauti ambao usingeweza kuelezwa kwa kutumia data za kifonolojia
peke yake. Baadhi yao wakapendekeza kuwapo kwa kiwango cha kimofofonemiki
pamoja na kipashio umbo kiini kama kiwakilishi cha mofimu, kwa hiyo
walipendekeza hivyo baada ya kushindwa kujua ipi ni alofoni ya fonimu ipi kwa
kutumia kigezo cha kifonetiki pekee Kwa
mfano; walishindwa kujua /k/ ni alofoni
ya /c/ au /c/ ni alofoni ya /k/ Kwa mfano hata katika lugha ya kurusi –
ruka = “mkono”
ručnoj = “a
mkono”
Mzizi ni – ruk na ruč
Wanamofofonemiki walichunguza wakagundua
kuwa katika mazingira fulani /k/ hubadilika kuwa /č/ baada ya kufuatiwa na “noj”.
Hivyo wakapendekeza umbo kiini la maneno haya ni ruKa au ruČnoj umbo kiini lake
lilitambulika kama {K} au {Č}
Katika lugha ya
Kiswahili kuna mabadiliko ya sauti yanayotokea katika baadhi ya maneno baada ya
sauti fulani kufuatiwa na kiambishi cha unominishaji (i) kwa mfano katika
maneno yafuatayo;
Fuata – fuasi
Penda – Penzi
Cheka – Cheshi
Pika – Pishi
Pia wanamofofonemiki walichunguza
ubadilishanaji huu wa sauti kwani walishindwa kujua ipi ni alofoni ya fonimu
ipi. Ndipo wakagundua kuwa katika mazingira fulani /t/ hubadilika kuwa /s/
baada ya kufuatwa na mofimu ya unominishaji “i” pia sauti /d/ hubadilika na
kuwa /z/ baada ya kufuatwa na mofimu ya unominishaji “i”
Baada ya kupendekeza umbo kiini maneno
haya yakaandikwa kama ifuatavyo: kwa mfano neno {fuaTa} umbo {T} likawa umbo
kiini ambalo linawakilisha sauti zote mbili yaani /t/ na /s/, pia neno {piKa}
umbo kiini lake ni {K} ambalo linawakilisha sauti /k/ na /ʃ/
Kuchunguza mabadiliko ya sauti
yanayotokea mofimu zinapoungana. Kwa mfano; katika lugha ya Kiswahili,
U + ima – wima
I + etu – yetu
Mu + alimu – Mwalimu
U + imbo – wimbo
Vi
+ ake –
vyake
Wanamofofonemiki wakagundua kuwa sauti
fulani huweza kuungana na kuunda sauti moja na kubadili umbo la neno.
Chunguza muundo wa kifonolojia wa mofimu katika
lugha. Kwa mfano katika lugha ya Kiswahili;
Mu + huni – Mhuni
Mu + gonjwa – Mgonjwa
Mu + guu – Mguu
Mu + uguzi – Muuguzi
Mu
+ tu – Mtu
Wanamofofonemiki wakagundua kwamba
mofimu fulani huweza kuungana na mofimu nyingine na kuunda umbo la neno.
Kuchunguza ubadilishanaji wa sauti ambao
una una uamilifu wa kimofolojia lakini husababisha mabadiliko fulani ya
kifonetiki. Kwa mfano katika lugha ya kiingereza;
Play + s – [pleiz]
Dog + s – [dogz]
Since
– [sins]
Else – [els]
Place
– [pleis]
Wanamofofonemiki wakachunguza kinachosababisha
kuwepo na maumbo tofauti tofauti ya mofimu ya wingi. Kwa mfano; /s/, /iz/, /z/
Wakagundua kuwa kuna mchakato zaidi ya ule wa kifonolojia ambao ni wa
kimofolojia unaosababisha umbo ‘s’ kutamkwa /z/ au /iz/ au /s/
MAREJEO:
The New Oxford American Dictionary. (2005), (2ndEdit), Oxford University
Press. New York.
imenisaidia sana hii passage katika jujiandaa na mtiihani wangu wa kumaliza semista.....nawashukuru sana walio andaa hii
ReplyDelete