MADA ZA KONGAMANO LA KISWAHILI LA KIMATAIFA LITAKALOFANYIKA
KIGALI-RWANDA KUANZIA 29-08 HADI 31-08-2013.
|
Kongamano lililofanyika Bujumbura-Burundi 2012. Hawa ni baadhi ya wanachama kutoka Tanzania na Rwanda. |
UBUNILIZI KATIKA
KISWAHILI NA ATHARI CHANYA KWA JAMII
UKWELI KUHUSU CHIMBUKO
LA KISWAHILI.
MCHANGO NA ATHARI ZA
JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUKIFANYA KISWAHILI KIWE LUGHA MOJA KWA AFRIKA
NZIMA.
KISWAHILI KAMA CHOMBO
CHA UKOMBOZI WA AFRIKA.
KUWASILISHA UTAMADUNI
WA MSWAHILI KWA NJIA YA IGIZO.
URARI WA VINA NA MIZANI
NDICHO KITOVU NA UTI WA MGONGO WA USHAIRI WA KISWAHILI” KUBALI AU KANUSHA DAI
HILI KWA MIFANO YENYE MASHIKO.
LUGHA YA KISWAHILI
HAIKIDHI MATAKWA YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA INAYOKUA KWA KASI KUBWA BARANI
AFRIKA.JADILI DAI HILI KWA MIFANO KUNTU.
1. Wahadhiri na washiriki wengineo
wanaweza kuandaa mada zao tofauti na hizi ili kuleta vionjo zaidi.
2. Pia, mada hizi zinaweza kuwasilishwa
kwa njia ya maigizo,ushairi,Tenzi,Vitushi n.k.
KAULI MBIU YA MWAKA 2013.
KISWAHILI NI TUNU NA JOHARI YA AFRIKA.
No comments:
Post a Comment