Thursday, 1 November 2018

AMRI KUMI ZA USHAIRI

AMRI KUMI ZA USHAIRI
  1. Ushairi ndiye mungu wako katika shida na katika raha, hakuna mbadala.
  2. Usitunge shairi bure; pasina haja yoyote wala tija.
  3. Shika utakatifu wa ushairi (tunga tungo zenye heshima na taadhima).
  4. Heshimu milango yako ya fahamu upate kutunga tungo zenye mvuto na zilizotukuka siku zote za utunzi wako.
  5. Usiue (heshimu uhai, uumbaji pamoja na tunu za utu katika mashairi yako).
  6. Usidhalilishe utukufu wa Mungu (usitunge tungo zisizo na staha dhidi ya viumbe vya Mungu).
  7. Usiibe (usichukue ubunifu wa mtu mwingine).
  8. Usidanganye (usitunge mashairi yenye maudhui yanayopotosha jamii).
  9. Usitamani sifa zisizokuwa zako (tungo zako ndizo zitakazotangaza sifa zako).
  10. Usitamani shairi la mtu mwingine bali tamani kuwa malenga bora.


© Eric F. Ndumbaro
Mwenge Catholic University (MWECAU)

No comments:

Post a Comment