Thursday, 1 November 2018

AINA ZA WASOMAJI MATINI (TEXT)

Wapo wasomaji wa aina nne (4) katika usomaji wa matini. Wasomaji hao ni: Kenge, Nyoka, Kinyonga na Kobe.
  1. Msomaji Kenge: msomaji huyu ni mkurupukaji mkubwa kwani husoma matini kwa kasi kubwa bila kuzingatia alama za uandishi wala kutafakari maudhui ya matini husika. Ni rahisi sana kuingiza maneno yake mwenyewe.
  2. Msomaji Nyoka: msomaji huyu husoma kwa madaha na mbwembwe nyingi bila kuzingatia maana na mantiki ya kila neno katika matini. Matokeo yake hupotosha kwa urahisi maudhui ya matini.
  3. Msomaji Kinyonga: huyu ni msomaji mzuri sana, si mvivu wa kurudia kusoma tena na tena kwa lengo la kutafakari zaidi. Hata hivyo katika usomaji wake ni rahisi sana kutekwa na hisia za mwandishi. Mara nyingi hubadilisha badilisha maneno na maudhui kutokana na hisia, vionjo na mihemko wakati wa usomaji.
  4. Msomaji Kobe: huyu ni msomaji makini na hana papara, ni mwaminifu katika huzingatia alama zote za uandishi. Daima hutafakari kila akisomacho tena hushirikisha milango yake ya ufahamu.

No comments:

Post a Comment