Sunday, 12 August 2018

SHAHNAM FERDOWSI



Mchango wa Shahnam Ferdowsi katika Ushairi wa Kiswahili

Eric F. Ndumbaro
Chuo Kikuu cha Kikatoliki Mwenge
Ikisiri
Shahnam (Kitabu cha Wafalme) ni utendi mrefu duniani ulioandikwa katika karne ya 5 na mshairi maarufu wa Kiajemi Hakim Abul-Qasim Mansur (940-1020Ad) ambaye baadaye alijulikana kama Ferdowsi Tusi. Utendi huu umepewa hadhi ya kitaifa na kuwa utendi wa taifa la Iran kutokana na maudhui yake. Shahnama ni utendi unaoelezea historia ya kale tangu kuumbwa kwa ulimwengu, historia ya Dola ya Uajemi mpaka kuingia kwa utawala wa Kiislam katika karne ya 7. Utenzi huu ni mojawapo ya kazi zinazonasibishwa na fasihi ya upinzani. Fasihi ya upinzani ni muundo fasihi unaojipambanua kwa kuonesha upinzani wa watu dhidi ya maadui, wanyang’anyi, wavamizi au wageni. Hata hivyo, fasihi hii haijitanabaishi na kipindi chochote au taifa fulani na imechipuka kutokana na historia ya mwanadamu. (Taheri na Kafi, 2017). Matamanio na malengo ya mwandhishi au mshairi yaliyofichika ndani mwake hujitokeza katika hali ya mtonesho na kudhihirisha uhusiano wake na ung’amuzi na jinsi gani unahusiana na kazi zake za sanaa. Kwa mantiki hiyo ukinzani wa kitafaifa unaojitokeza katika kazi mbalimbali za washairi ni matokeo ya mfifizo wa hapo awali. Utafiti huu una lengo la kuchunguza mashairi ya Kahigi kama yana mhamisho wowote wa mtonesho unaodhihirisha vipengele/elementi zozote zinazoashiria uendelevu wa Shahnameh Ferdowsi kama miongoni mwa fasihi kinza katika ushairi wa Kiswahili.

No comments:

Post a Comment