Karl Marx
(1818-83) na Friedrich Engels (1820-95
-Hawa ndio waasisi wa mtazamo huu. Hata hivyo wao wenyewe
hawakuandika sana kuhusiana na fasihi.
·
Hoja tatu Muhimu
- 1. Katika
historia ya mwanadamu, jamii na mahusiano yake, taasisi zake namna yake ya
kufikiria; mambo yote hayo hutegemea mabadiliko ya mfumo wa uzalishaji mali.
Yaani jinsi uchumi, uzalishaji, mgawanyo na umilikaji mali unavyoendeshwa
2. Mabadiliko
ya kihistoria katika msingi wa uzalishaji mali yanaathiri mabadiliko ya muundo
wa matabaka ya jamii, na hivyo kutokeza (kwa kila wakati) tabaka tawala na
tawaliwa ambayo huwamo katika mapambano na harakati za kugombea uchumi, siasa
na faida za kijamii.
3. Urazini wa
mwanadamu umeundwa na itikadi, Imani, thamani ya kitu (value), na namna za kufikiri
na kuhisi
· Ni kupitia katika hivi, mwanadamu huuona ulimwengu wake, na
huelezea yale yaliyomzunguka na yale anayoyaona kuwa ukweli.
ATHARI KATIKA FASIHI
Waandishi wa
Ki-Marx huandika kwa kutumia falsafa ya Ki-Marx na jinsi alivyoiona historia
ambapo wazo kuu ni kuwa: harakati za matabaka ndio msingi mkuu unaofanya mambo
yawe kama yalivyo.
Nguvu ya Historia
Jinsi gani
wanavyoweza kuufahamu ulimwengu uliopita kwa kutumia vielelezo na uthibitisho
wa kihistoria.
Mfano: Matini km. Riwaya inawakilishaje ukweli? Ukweli
huo ni usahihi wa mambo ktk Jamii. Usanii ni uumbaji wa Ukweli ktk maisha?
UHALISIA WA KISOSHALISTI
Mwandishi au
msanii yeyote, ajitoe kuandika na kulielimisha kuhusu tabaka la wafanyakazi. Na
kwamba, fasihi ni lazima iwe ya kimaendeleo, na ioneshe mtazamo wa kimaendeleo
katika jamii
Georg Lukács (1885-1971) Hungary
Nadharia yake: Kiakisiko
Kwamba mambo
yote huakisi ukweli fulani wa maisha. Kazi ya fasihi huakisi mfumo fulani
unaofumbuka polepole. Kutuonesha mivutano, mikizano na au migogoro iliyomo
katika maisha ya jamii inayoakisiwa.
KIAKISIKO
Kilicho cha
msingi ni maudhui na sio fani yake. Fani inachukua nafasi ndogo sana katika
kazi ya fasihi.
Mgogoro wa Ushairi wa Kiswahili.
Brecht
alipingana naye kwa kusema hatuwezi kushikilia sheria za sanaa katika muda wote
kwani ukweli wa jamii hubadilika.
MKABALA WA
FRANKFURT 1923-1950
Nadharia Hakiki
Theodor
Adorno, Max Horkheimer na Herbert Marcuse.